USHIRIKISHWAJI WA VIJANA WANAWAKE KATIKA SIASA,NGAZI ZA UONGOZI NA MAAMUZI.
Na Riziki Abdalla KATIKA karne ya 21, adhma ya kufikia usawa wa kijinsia imekuwa ni agenda inayotiliwa mkazo kimataifa na kitaifa kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika ngazi za uongozi na za maamuzi hususani ndani ya vyama vya siasa. Takwim u zinaonesha kuwa idadi ya wanawake imekuwa ikiongezeka zaidi kuliko ya wanaume. Katika sensa ya mwaka 2022, Zanzibar ina jumla ya watu 1,889,773 kati ya hao wanawake ni 974,281 sawa na asilimia 52 ya watu wote. Takwimu hizi zinaonesha kwa kiasi gani suala la kuzingatia ushirikishwaji wa wanawake katika mambo ya maamuzi na uongozi ni jambo lisiloweza kuepukika. Pamoja na uwepo wa idadi kubwa ya wanawake bado ushiriki wao katika ulingo wa uongozi umekuwa ni mdogo sana , ila dhana hii imeanza kufanyiwa mageuzi makubwa kupitia Jimbo la Fuoni Katika Jumuiya Ya Umoja Wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kuwa na idadi kubwa ya viongozi wanawake hususani katika nafasi ya katibu kuanzia matawi, wadi ...