USHIRIKISHWAJI WA VIJANA WANAWAKE KATIKA SIASA,NGAZI ZA UONGOZI NA MAAMUZI.


Na Riziki Abdalla

KATIKA  karne ya 21, adhma ya kufikia usawa wa kijinsia imekuwa ni agenda inayotiliwa mkazo kimataifa na kitaifa kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika ngazi za uongozi na za maamuzi hususani ndani ya vyama vya siasa. 


Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wanawake imekuwa ikiongezeka zaidi kuliko ya wanaume. Katika sensa ya mwaka 2022, Zanzibar ina jumla ya watu 1,889,773  kati ya hao wanawake ni 974,281 sawa na asilimia 52 ya  watu wote. Takwimu hizi zinaonesha kwa kiasi gani suala la kuzingatia ushirikishwaji wa wanawake katika mambo ya maamuzi na uongozi ni jambo lisiloweza kuepukika. 

Pamoja na uwepo wa idadi kubwa ya wanawake bado ushiriki wao katika ulingo wa uongozi umekuwa ni mdogo sana , ila dhana hii imeanza kufanyiwa mageuzi makubwa kupitia Jimbo la Fuoni Katika Jumuiya Ya Umoja Wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kuwa na idadi kubwa ya viongozi wanawake hususani katika nafasi ya katibu kuanzia matawi, wadi hadi Jimbo.


Jimbo la Fuoni lina jumla ya matawi tisa (9) wakiwemo makatibu 5 wanawake, wadi tatu (3) ikiwa na makatibu wanawake watatu na Jimbo kukiwa na katibu hamasa mmoja mwanamke ukilinganisha na majimbo mengine yanayopatikana ndani ya wilaya ya Dimani kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi. ‘’ moja ya sababu zilizopelekea kuwa na wanawake wengi kwa nafasi ya utendaji katika jumuiya ua vijana ndani ya jimbo la Fuoni ni hamasa walizonazo wanawake wa jimbo langu katika ungozi”. Alisema Moh’d Simai Saleh ambae ni Mwenyekiti wa UVCCM Jimbo la Fuoni.

BAADHI YA MAKATIBU WA UVCCM JIMBO LA FUONI WAELEZA JINSI WALIVOPATA NAFASI HIZO NA USHIRIKISHWAJI WAO KATIKA UONGOZI NA MAAMUZI

 Nayla Juma Ali ambae ni katibu wa UVCCM tawi la Fuoni Migombani alieleza kuwa “kujiaminisha na uthubutu wa utendaji kazi kwa weledi katika uongozi ndio uliotufanya tuaminiwe na wajumbe tunaowaongoza katika matawi yetu bila kujali utofauti wetu wa kijinsia”

Nae Sabrina Hashir Mussa ambae ni katibu wa UVCCM wadi ya Fuoni Kibondeni alisema kuwa “jambo pekee lililonifikisha hapa ni utayari pamoja kujitambua kwa kile nilichokusudia kukifanya ndani ya wadi yangu” pia aliongeza kwa kusema kuwa “ kutokana na ushirikishwaji wetu kwenye sehemu za maamuzi kumepelekea maendeleo makubwa sana ndani ya jimbo la Fuoni na kwa vijana wenzetu kwa ujumla”

Miongoni mwa mambo waliyoyafanya kwa vijana wenzao wa jimbo la Fuoni ni pamoja na kuanzisha hamasa na makongamano mbalimbali kwa vijana ili kuwashirikisha vijana hao hususani wanawake kwenye nafasi za uongozi pamoja na kujiendeleza kimaisha “tumeweza kuanzisha kikundi cha DIRA YA MAFANIKIO ambacho kinajishuhulisha na ufugaji wa majongoo, mapishi na kilimo ili kumsaidia kijana kujikomboa na umaskini” alisema Sharifa Haji Suleiman ambae ni katibu wa UVCCM Wadi ya Fuoni Mambosasa.

Licha ya mafanikio ya kimaendeleo yanayofanywa na uwepo wa ushirikishwaji wa viongozi hao wanawake katika Jimbo la Fuoni, bado wanakumbana na changamoto nyingi sana katika harakati za uongozi wao “ changamoto kuu tunayokumbana nayo ni  kutoaminiwa kutokana na mtazamo hasi watu walionao kwa kudhani kuwa wanawake hawawezi kuongoza kama wanavowaamini wanaume kwenye uongozi” alisema Sabrina.

Nae katibu wa UVCCM Jimbo la Fuoni ndugu Paul Semon Buchumi alimalizia kwa kusema kuwa “tutahakiksha tunashirikiana nao bega kwa bega kwenye kila changamoto wanazopitia makatibu wetu kwenye harakati zao za utendaji pamoja na kufikisha changamoto hizo sehemu husika pale ambapo kwa ngazi ya Jimbo zitashindikana”  

Kwa kutambua umuhimu wa mwanamke sera na sheria mbalimbali za Zanzibar zimeeleza kuhusu haki ya wanawake kushiriki katika uongozi na maamuzi, sera na sheria hizo ni pamoja Katiba ya Zanzibar, Dira ya Zanzibar 2020, sera ya jinsia ya Zanzibar, sheria ya vyama vya siasa ya uchaguzi ya Zanzibar nakadhalika.


Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI