Posts

Showing posts with the label habati

KUPASUKA BARABARA KUFANYIWA UTAFITI PEMBA

Image
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.  WIZARA  ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi   Zanzibar imesema itaendelea kuchukua hatua za dharura kuzifanyia marekebisho ya haraka   barabara zote za kisiwani  Pemba zilizoharibika kutokana na mvua  zinazoendelea kunyesha  ili kuwaondoshea Usumbufu wananchi wake.   Waziri wa wizara hiyo Khalid Salum Mohamed  ameyasema hayo  huko Makombeni  Darajani wilaya ya Mkoani alipokuwa  akizungumza na  kutoa ufafanuzi  kwa kamati ya Mawasiliano  Ardhi na nishati  iliofika na kutembelea ujenzi wa  barabara mbali mbali  na kujionea mtengenezo kwa baadhi ya barabara zilizokatika kutokana na mvua ikiwemo barabara hiyo.  Amesema kupasuka  na kukatika kwa barabara nyingi kisiwani Pemba mara zinapopata mvua ni kutokana na aina ya udongo uliopo katika ardhi nyingi kisiwani humo jambo ambalo wizara linaendelea kuzifanya utafiti wa kitaalamu kujua chanzo has...