KUPASUKA BARABARA KUFANYIWA UTAFITI PEMBA

NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA. 

WIZARA  ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi   Zanzibar imesema itaendelea kuchukua hatua za dharura kuzifanyia marekebisho ya haraka   barabara zote za kisiwani  Pemba zilizoharibika kutokana na mvua  zinazoendelea kunyesha  ili kuwaondoshea Usumbufu wananchi wake.


  Waziri wa wizara hiyo Khalid Salum Mohamed  ameyasema hayo  huko Makombeni  Darajani wilaya ya Mkoani alipokuwa  akizungumza na  kutoa ufafanuzi  kwa kamati ya Mawasiliano  Ardhi na nishati  iliofika na kutembelea ujenzi wa  barabara mbali mbali  na kujionea mtengenezo kwa baadhi ya barabara zilizokatika kutokana na mvua ikiwemo barabara hiyo. 

Amesema kupasuka  na kukatika kwa barabara nyingi kisiwani Pemba mara zinapopata mvua ni kutokana na aina ya udongo uliopo katika ardhi nyingi kisiwani humo jambo ambalo wizara linaendelea kuzifanya utafiti wa kitaalamu kujua chanzo hasa kinachopelekea kupasuka kwa barabara mbali mbali, huku matengenezo ya dharura yakiendelea kuchukuliwa kuzitengeneza  . 

 Aidha amesema  licha ya kukamilika kwa hatua ya kwanza ujenzi wa barabara ya Kipapo Mgelema wambaa, na kushindwa kukamilika moja kwa moja barabara hiyo kwa    wizara inaendelea na ujenzi ili kukamilika kwa hatua zilizobakia ndani ya bara bara hiyo. 

"Wizara inaendelea na hatua mbali mbali za ujenzi wa barabara hii  tumeshakamilisha kwa asilimia 90 baadhi ya maeneo na mengine yaliobaki ni  hatua za mwisho kwajili ya kuweka lami ili kukamilika, Changamoto  mbali mbali zilijitokeza lakini wizara zimesimamia kuzipatia ufumbuzi na wananchi  hivi karibuni watazidi kuitumia barabara hii ikiwa imeshakamilika". 

Amesema  kuchelewa kukamilika  kwa ujenzi wa barabara mbali unguja na Pemba  kumetokana na  changamoto mbali mbali ambazo wizara imeshazichukulia hatua ili kuzikamlisha kwa wakati na wananchi kuweza kuzitumia kwa shughuli mbali mbali. 

Alisema  kwa upande wa ujenzi wa barabara za vijijini kisiwani humo  wizara inaendelea na ujenzi   katika maeneo mbali  ili kuendelea kufikisha huduma za usafiri katika vijiji na kurahisisha upatikanaji wa maendeleo ambapo asilimi 98 ya barabara hizo upande wa kusini zimeshafanyiwa usafi kwajili ya  matengezo . 

 Hata hivyo  Dk Khalid   amesema kuwa wizara imetoa zaidi  kipaumbele kwa barabara 3 kisiwani humo katika kuhakikisha zinajengwa na kukamilika kwa wakati. 
 
 Hata hivyo  alisema kuwa Matengenezo ya barabara hizo ni pamoja na uwekaji wa mitaro, pamoja na alama za barabarani  katika kuhakikisha haziathiriki  na kuharibiwa na mvua. 

 Akizungumza makamo mwenyekiti wa kamati  ya Mawasiliano  Ardhi na nishati ya baraza la wawakilishi Aza Januar Joseph ameipongeza wizara hiyo kwa kuendelea  na ujenzi wa barabara mbali mbali  na nyengine kukamilika licha ya kukabiliwa na changamoto za fedha pamoja na  baadhi ya vifaa vya kutendea kazi. 

Aidha Aza Amesema kamati hiyo imeridhishwa na majibu  sambamba na kujionea maendeleo yaliofikiwa na wizara hiyo katika  ujenzi wa barabara mbali mbali kisiwani Pemba  .
 
Tumeona mambo mbali mbali tumeona shughuli zinavyokwenda za ujenzi  wa matengenzo ya barabara tunaipongeza sana wizara kwa kazi wanazofanya, Tumeona kwamba hatua za dharura zinachukuliwa za kudhidbiti tatizo ambalo limeonekana limaweza likaleta athari  ambazo zinaweza kuzuia njia zisiweze kupitika. 


 Kwa Upande wake Afisa mdhamini wizara ya Mawasiliano Ujenzi na uchukuzi Pemba Ibrahim Saleh Juma   Amesema kuwa ucheweshwaji  wa ujenzi wa barabara mbali mbali kisiwani Pemba kunatokana na uhaba wa vifaa pamoja na rasilimali fedha ambapo hatua za kulipatia ufumbuzi suala hilo zimeshachukuliwa kiwemo  kuwasilisha mpango kazi  wizara ya fedha na mipango kwajili ya upatikanaji wa fedha na mara zitakapokamilika suala hilo litapatiwa ufumbuzi kwa muda mfupi. 

Kamati hiyo imetembelea barabara mbali mbali kusini Pemba ikiwemo  Ukutini Mtangani, Ole Kengeja, Makombeni  Mkoani, Chanjaani Puniji. 




Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.