GOMBANI FITNESS KUJA NA BONANZA MAALUM KUHAMASISHA USAWA WA KIJINSIA .
NA HANIFA SALIM, PEMBA KLABU ya mazoezi Gombani (Gombani Fitness Club) katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 10 ya klabu hiyo, imeandaa bonanza la michezo kwa lengo la kuhamasisha masuala ya michezo kwa jamii kwa kuzingatia usawa wa kijinsia. Akisoma taarifa kuhusu maadhimisho hayo katika mkutano wa waandishi wa habari Kisiwani Pemba, huko ukumbi wa (TAMWA) Mkanjuni Chake chake, Katibu wa Klabu hiyo Khalfan Amour Mohamed alisema, bonanza hilo litahamasisha ushiriki wa wanawake katika mazoezi. "Bonanza hilo linatarajiwa kuchezwa michezo ya aina tatu ikiwemo mbio za magunia, mazoezi ya viungo na mchezo wa kuvuta kamba, kuanzia Julai 20 hadi Julai 28 mwaka huu, viongozi wa serikali na taasisi watashiriki matembezi kuanzia Madungu hadi uwanja wa michezo Gombani", alisema. Alieleza, kuelekea shamra shamra za kilele cha maadhimisho hayo, waandaaji wa bonanza hilo watapita skuli na katika shehia mbali mbali kuhamasisha usawa wa kijinsia katika michezo pa...