WAANDISHI ,WAMILIKI WA VYOMBO WAHIMIZWA KUANDIKA HABARI ZA MICHEZO KWA WANAWAKE HUKU VIONGOZI WA SERIKALI WAKIASWA KUTEKELEZA KWA VITENDO SERA YA MICHEZO KWA WOTE ILIYOWEKWA NA SERIKALI ZANZIBAR.
. Na , AMINA AHMED PEMBA. WAMILIKI na waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari wametakiwa kutoa kipaumbele katika kuandika na kutangaza habari zinazo gusa maendeleo na changamoto katika sekta ya michezo kwa wanawake ili kukuza ushiriki wa kundi hilo katika michezo kisiwani Pemba . Kauli hiyo imetolewa na Mwandishi mwandamizi Zanzibar Hawra Shamte,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali kisiwani humo wanaoendelea kushiriki katika mafunzo ya siku 5 ya kujengewa uwezo juu ya kuandika habari za ushiriki wa michezo kwa wanawake yaliondaliwa na TamwaZanzibar katika ukumbi wa ofisi za chama hicho Mkanjuni Chake Chake . Amesema bado mchango wa waandishi na vyombo vya habari Zanzibar umekuwa hauridhishi katika suala la utoaji wa habari zinazogusa michezo kwa wanawake jambo ambalo lina...