UHABA WA VITUO VYA POLISI WILAYA CHAKE CHAKE NI SABABU INAYOCHANGIA KUWEPO KWA VITENDO VYA UHALIFU NA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINAADAMU .
- Get link
- X
- Other Apps
NA AMINA AHMED MOH’D - PEMBA.
Chake Chake ni wilaya iliyopo katika Mkoa wa Kusini Pemba Zanzibar Tanzania ambayo kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 ina idadi ya wakaazi 97,249 na anuani za makazi 74200 .
Hadi kufikia mwaka huu 2022 wilaya hiyo ina jumla ya shehia 32 ambazo wakaazi wake hulazimika kutumia kituo kimoja pekee cha Polisi katika kuripoti matukio mbali mbali ya kihalifu ikiwemo udhalilishaji, wizi wa mazao mifugo pamoja na kesi mbali mbali huku baadhi ya wananchi wakikwazika zaidi kukifikia kituo hicho bila kujua hatima na ufumbuzi wa suala hilo.
Licha ya baadhi ya wananchi hao waliowengi kuwa na matumaini kusogezewa kwa karibu vituo vya polisi katika shehia zao.
" Tuna matumani na serikali pamoja na watu wenye uwezo kutusaidia kutuongezea vituo wilayani kwetu na kwa vile tukionana na viongozi tunalalamika suala hili ni imani yetu watalipa uzito suala hili"Alisema Pascal Mkubwa mwanaharakati wa dini juu ya kupinga udhalilishaji wa kijinsia.
Aliendelea kuzungumza na habari hizi maalum kuongeza kuwa
" Tupo tayari kujitolea nguvu zetu kufanikisha ujenzi wa vituo vya polisi endapo wadau watajitokeza tupo tayari tushike pauro tubebe mabero sisi uwezo wa kujenga hatuna lakini uwezo kujitolea nguvu kusaidia tuko tayari".
"Suala hili linarudisha nyuma mapambano dhidi ya udhalilishaji na Matukio mengi huishia njiani kutokana na wahusika kuwa mbali na vyombo vya sheria." Alisema kiongozi huyo mkaazi wa Gombani chake chake.
Baadhi ya wananchi wanasema kuwa umbali huo umbali wa vituo vya polisi katika maeneo yao ni chanzo cha kufanyika suluhu na kuishia majumbani baadhi ya kesi za udhalilishaji zinazojitokeza.
" Suluhu zinapita majumbani kesi za udhalilishaji lakini ingekuwa vituo vipo karibu matukio yakitokea yanaripotiwa uongo mtu anogopa kusuluhisha kwa vile itakuwa tayari ashapeleka kesi atahofia kumaliza kesi mjumbani lakini saivi mtoto anasoma skuli kadahlilishwa kesi hayendi popote anakatishwa masomo anaolewa siku mbili anaudishwa haki yake ya kusoma ashaikosa na kwa mume hajakaa. alisema Bi Saumu Ali mkaazi wa Ole.
" Watoto sikuizi wazazi hawatuogopi tena unamkataza kitu hichi kibaya anafanya hicho hicho wilaya nyengine zikiona mtoto kawa msugu anapelekwa polisi ijapo kutishiwa kama alikiwa haendi skuli ndio inakuwa dawa anaogopa kiupande wetu hilo ni gumu tunawaacha tu mana mpka ukifunga safari kuenda uko kituoni si leo".
Tunaibiwa mifugo yetu inachinjwa usiku huko huko tulikoilaza mtu ata akipiga kelele muibaji anaacha kisu na mapolo apo apo anakimbia Tusubiri asubuhi tuende Kutoa tarifa polisi mana uwezo wa kuenda kwa miguu kutoa taarifa hatuna kituo mpka uende chake mjini ".
" Tunamuomba Rais wetu wa zanzibar atusaidie kusogeza huduma hizi karibu kutuondolea usumbufu tunaoupata sisi akina mama mifugo yetu inaibiwa tunakosa haki zetu kutokana na kushindwa kufikia kwa wakati sahihi vituoni kutoa taarifa za kuibiwa".
"Binafsi mwanzoni mwa mwaka huu nimeibiwa ng'ombe wangu akachinjwa lakini kesi nikaenda polisi siku moja zilizobakia sijaenda kufuatilia mpka kesho inabaki kumbukumbu tu nilichoka kwenda na kurudi kila siku Nimerudia nyuma kimaendeleo " .
Ni maneno ya bi Asha Bakari Juma mkaazi Wa Kijiji Cha Simaongwe Shehia ya Mjini Ole wilaya ya chake chake.
"Haki za binaadamu hazipo zinakosekana kabisa kuna nyakati tumekuwa tukiogopa hata kukatisha njia na watoto Vurugu za vyombo vya miguu miwili nyakati za jioni na usiku wale hawana kofia ngumu, wale wanaendesha wanavyojua" .
"kwa sababu hakuna polisi vijana wanapoteza nguvu ajali barabara wengine wanakufa wengine wanakatika viungo huku kwetu zaidi, kungekuwepo na kituo hakuna kijana angeendesha chombo ovyo akapita mbele ya kituo anajua atachukuliwa hatua lakini hakuna anafanya anavyojiskia ".
" Serikali tunaomba itusaidie huki wesha kuwekwe kituo na sehemu nyengine zenye barabara za ndani vijana wanapoteza maisha kizembe wallah.
"Bi Mkasi Haji Mkaazi wa Wesha. Kwa upande wake Mzee Hassan Yakoub alisema kuwa Baadhi ya vijana wasiopenda amani wamekuwa wakiutumia mwanya huo kufanya vitendo vya uhalifu .
" Wanajua kama kwa mda huu naweza kuiba nikakimbia bila konekana na hata nikionekana ata nikifikishwa polisi sio leo wala kesho naweza nikababaisha nikaachiwa huru madhali hawakunikamata pale pale".
"Tunaomba Tusogezewe karibu vituo vya polisi Sababu vitendo vya uhalifu vinavunja amani na watu hujichukulia sheria mikononi mwao kwa vile vyombo vya sheria havipo karibu yao". Alisema Mzee huyo mkaazi wa ole.
Hemed Abeid Hemed Ni sheha wa shehia ya Mbuzini wilaya ya chake chake amesema kuwa shehia yake ni moja kati ya shehia ambayo serikali inahitaji kuweka kituo cha polisi ili kudhibiti usalama wa watu wa aina mbali mbali.
"Mbuzini ndio shehia ambayo ina lango kuu la kuingilia na kutokea chake chake hapa ndio kuna umuhimi mkubwa wa kuwepo kituo cha polisi kudhibiti uhlifu Tunaiomb serikali na wahisani itusaidie suala hili tunataka chake chake ambayo haina uhalifu".
Bi mafunda hamad Rubea Sheha wa shehi ya Madungu anasema Matukio mengi ya kiuhalifu yanayoripitiwa kwake yamekuwa na urahisi kufikishwa kituoni kutokana na kuwa karibu na kituo hicho kwa upande wake jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi wa mazao na mifugo.
"Kesi dha udhalilishaji zinaporipotiwa kwangu dakika tumezifikisha kituoni ufuatliaji unaanza zinapelekwa mahakamani hazina nenda uje ambayo itawasumbua wananchi wangu labda mtu hna nauli anamudu kuenda kituoni hata kwa miguu ni jambo la kujivuna kuwa karibu na kituo, lakini hata uhalifu sio mara nyingi kuskia kumeibiwa nguo mara mifugo mara mazao ni vile tu shehia ipo karibu na kituo cha polisi ".
kila siku zinavyozidi wakaazi wilaya ya chake chake wanazidi kuongezeka katika maeneo ya miji na vijiji na hii inasababishwa na kuwepo kwa mjii mkuu wa kibiashara wilayani humo ambao takribani wilaya zote zilizopo kisiwani Pemba Hulazimika kufuata mahitaji mengi katika mji huo.
Kwa upande wa Ofisi Ya Mkurugenzi wa Mashtaka Mkoa wa kusini Pemba imesema inapokea kesi nyingi zaidi za makosa na vitendo mbali mbali vya uhalifu h kutoka wilaya ya Chake Kuliko wilaya ya Mkoani.
"Wilaya ya Chake tunapokea kesi nyingi zaidi kuliko Wilaya ya Mkoani na zinatokea kesi na jalada linaletwa Ofisini lakini kutokana na ushahidi kuwa dhaifu tunaelekeza kufungwa kutokana na kukosa ushahidi zipo ambazo Walifunguwa kshindwa kurudi tena kufuatilia Zipo kesi ambazo aliefanya kosa hajulikani alieripoti kaja siku moja tu harudi tena".
"Sababu zinaweza kuwa nyingi zinazopelekea tofauti hiyo kiwilaya kwanza Wilaya ya Chake ina idadi kubwa ya watu kuliko mkoani lakini Wilaya ya Chake ni Wilaya yenye mji kuliko mkoani, na wilaya zote ambazo zina miji makosa ni mengi kuliko ambazo hazina miji kifupi mjini makosa ni mengi na wahalifu ni wengi".
Sababu nyengine ni "Wilaya ya Chake ina upungufu wa vituo vya Polisi, kipo kimoja tu tofauti na Wilaya ya Mkoani yenye Vituo vitatu vya Polisi, pia inapelekea kupungua kwa makosa endapo vituo vikiwa karibu na wahalifu kwani huingiwa na hofu lakini pia Jamii zinazoishi wilaya ya Mkoani wanaishi kijamii kwa maana wengi ni ndugu tofauti na Wilaya ya Chake yenye wahamiaji wengi". Alisema Wakili wa serikali kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Ali Amour Makame Aliookuwa akizungumza na mwandishi wa makala hii maalumu "
Kwa upande wa jeshi la Polisi limesema kuwa licha ya changamoto hiyo Hulazimika kutumia Askari wakaguzi ambao wamekuwa mbadala wa kuimarisha ulinzi na usalama katika shehia ambazo zipo mbali na kituo hicho cha polisi" Tunao maafisa wakaguzi kutoka jeshi la polisi ambao tumewaweka maalum katika kila shehia kuona kwamba wanaimarisha na kutoa mashirikiano juu ya kutatua changamoto mbali mbali katika kuimarisha ulinzi"
" Changamoto iliyopo kwa sasa ni uhaba wa askari hao
jambo ambalo tunalishughulikia kuona kwamba wanatosheleza kwa vile kutokana na uhaba huo askari mmoj hulazimika kusimamia shehia zaidi ya tatu".
" Kuhusu Suala la vituo ni jambo la Jamii husika watakapoona kuna ulazima wa kuwepo Jeshi halitosita kupeleka askari vituoni humo ni jambo la kukaa na kujadilina uongozi wa wilaya kuona namna gani wanafanikisha hilo sababu jukumu letu ni kuimarisha ulinzi na usalama naaskari wetu wapo tayari".
Alisema Kamishna Wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad.
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali amekiri na kusema kuwa Suala la uhaba wa vituo vya polisi katika wilaya yake lipo ambapo tayari Umeanza kulifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kulifikisha suala hilo uongozi wa mkoa kujadiliwa zaidi.
ABDALLA RASHID ALI - MKUU WA WILAYA YA CHAKE CHAKE PEMBA.
"Masheha waliowengi mara kwa mara katika vikao vyetu wamekuwa wakiliwasilisha suala hili na wilaya tumeshafanya juhudi za kulifikisha suala hili uongozi wa juu zaidi kupatiwa ufumbuzi ".
Aidha Mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya inajukumu la kuhkikisha masuala ya ulinzi na usalama katika maeneo ya utawala yanaimarika mda wote wilaya na mkoa.
" Wenye dhamana ya usalama ni wananchi wote kwa ujumla wao licha ya serikali kuweka taasisi za kusimamia masuala ya kiusalama miongoni mwao ni jeshi la polisi Tunashukuru jeshi hilo linatoa mashirikiano vizuri katika kudumisha ulinzi na usalama wa kulinda na mali na raia wake".
Alisema " kutokana na ukuaji wa miji, na ongezeko la idadi ya watu kwa wilaya yetu ya chake chake sasa ivi bado tuna kituo kimoja tu cha polisi, katika hatua hiyo miji yetu kutanuka zaidi, watu kuongezeka, harakati za kiuchumi za kijamii pia kukua, ni kiri kuwa kituo hichi hakitoshelezi hivyo ni wazi kuwa ipo haja ya kuongeza vituo hivyo ili kudhibiti zaidi usalama .
Alisema kuwa bado uongozi wa wilaya mpaka sasa haujafanikisha suala hilo la ujenzi wa vituo vyengine vya polisi katika maeneo mbali mbali ya mji wa chake chake.
"Tayari ndani ya wilaya yetu tumebahatika kupata barabara kubwa hii yabole kengeja ambayo imekuwa na tija kubwa na wananchi wameanza kuvutika kuanza kuishi katika ukanda wa barabara hiyo na bado utakuta kutok hapo ole mpka kufika kengeja bado hakuja kuwa na kituo cha polisi ni maeneo muhimu ambayo pia yana umuhimu na ulazima wa kuwepo na kituo".
Katika hatua nyengine mkuu wa wilaya huyo Alisema kuwa Serikali ya wilaya tayari imetenga maeneo maalum ambayo itakuwa tayari kuyatumia kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya polisi katika wilaya hiyo endapo serikali itaridhia na wadau watajitokeza kujenga vituo hivyo katika wilaya yake.
Aidha amesema uongozi wa wilaya unaendelea kuzungumza na wadau na wazalendo wa nchi hii ili kupata msaada wa kujengewa vituo vya polisi katika badhi ya maeneo muhumu na yenye ulazima wa kuwepo vituo vya polisi .
Tunaendelea vizuri na mazungumzo kwa wadau wanaopenda amani na maendeleo kuona na wao wanatoa nhuvu zao katika kutusaidia jambo hili na mmoja ameahidi kushirikiana kupata kituo katika maeneo ya wilaya yetu.
Aidha Mkuu wa wilaya amesema kuwa endapo wilaya hivyo itaweza kupata vituo vingi vya polisi kutasaidia kudhibiti uhalifu unaoendelea kutokea katika maeneo mbali mbali.
" Chake Chake ina zaidi ya bandari Zisizo rasmi 88 ambazo wahalifu huzitumia katika kufanya mambo ya kiuhalifu jeshi la Polisi linaendelea kudhibiti na kukamata wahalifu wanaotumia maeneo hayo lakini endapo kutakuwa na vituo vya uhakika kutarahisisha zaidi kudhibiti uhalifu".
"Wezetu wilaya ya Mkoani wana vituo vingi hata kasi yao ya kudhibiti vitendo vya kihalifu inaongezeka maeneo yao ya bandari kuna kituo, Kengeja, Mtambile na mote humo ukaguzi unakuwa unafanyika mda wote na unazuilika unapotokezea kwa upande wa mashariki kituo kipo karibu magharibi lakini pia center ya mji kipo kituo karibu,kadhalika wete na micheweni Alisema".
Alindelea kisema kuwa " Chake Chake ina shehia 32na tunampango wa kuongeza shehia kituo kipo mjini lakini kuna maeneo ambayo ufikiaji wake ni mgumu kwa mfano mgelema, kilindi Ndagoni ni mbali na yote ni maeneo ambayo ni maeneo ambayo kuna bahari, kote huko kwa umuhimu wake kunastahiki kabisa kuwa na vituo vya polisi endapo kutakuwa na uwezekano kujengwe vituo itakuwa ni hatua nzuri ya kudhibiti uhalifu usiingie na usitokee katika wilaya.
Mkuu wa Wilaya huyo amewataka wananchi kutosita kuisadia serikali na jeshi la polisi kudhibiti vitendo vya kihalifu badala yake watoe Taarifa endapo watabaini kuwepo kwa vitendo viovu katika jamii zao.
Aidha Aliwaomba wadau mbali mbali kujitolea kusaidia kuongeza vituo vya polisi katika wilaya yake.
" Tuko Tayari kutoa mashirikiano kwa yeyote atakaekuwa tayari kusaidia suala hili la ujenzi wa vituo vya polisi katika wilaya yetu ikiwa ni wadau wa kupinga udhalilishaji, kulinda haki za binaadamu watu binafsi kikundi cha watu taasisi za fedha na wasamaria wema wajitokeze kufanikisha kupunguza changamoto hii lengo ni kuona tunaendeleza mapambano ya kudhibiti uhalifu wa aina mbali mbali. "
Wilaya ya Chake Chake ina shehi 32 Ambazo ni Shehia ya Wara, Kichungwani, Chanjaani, Matale, Kilindi, Kibokoni, Uwandani, Ng'ambwa, Wawi, Mchanga Mrima, Ndagoni, Wesha, Birikau, Madungu, Shungi, Msingini, Chachani, Mgelema, Tibirinzi, Kwale, Michungwani, Gombani, Vitongoji, Mfikiwa, Mgogoni, Ole, Mjini ole, Mbuzini, Mvumoni, Pujini, Chonga Pamoja na Chanjmjawiri.
MTAA WA AFRIKANA CHAKE CHAKE
Shehia zote hizo zimekuwa zikiendelea kuishi kwa wasi wasi endapo vitajitokeza viyendo vya kihalifi nyakati za usiku ambapo Wananchi wengi wanaoishi katika baadhi y vijiji vilivyomo shehia hizo hushindwa kuripoti matukio ya kiuhalifu huku wengine kuripoti matukio mara moja bila kuyafuatilia sababu ikiwa ni umbali wa vituo vya Polisi.
Suala hili hupelekea kukosa haki zao muhimu huku watoto vijana na wanawake wakiendelea kukosa haki zao muhimu kutikana na kufanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo udhalilishaji jambo ambalo hupelekea kuvunjwa sheria mbali mbali ya usalama wao Huku shehia moja ya Madungu ikibakia kuwa Salama Juu ya mapamabo dhidi ya uhalifu.
Mwisho.
- Get link
- X
- Other Apps
Ni kweli kabisa Chake chake hilo ni tatizo watu wamekuwa free sana yani ao Boda boda Mati one ndio zaidi Bara bara mpya ndo hakufai kazi wanakata wenzao miguu tu usiku Pujini kwa kupiga misere na mavespa Kijengwe tu .
ReplyDelete