WADAU WA KUPAMBANA NA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE NA WATOTO WALIA NA SHERIA NAMBA 7 YA MWAKA 2018 , SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI, WAOMBA KUFANYIWA MABORESHO BAADHI YA VIFUNGU VYAKE.
NA AMINA AHMED MOH’D - PEMBA "USIPOZIBA Ufa Utajenga Ukuta " Ni Msemo Ambao Mara Nyingi unapotumika Huashiria kuwepo kwa Dosari ya Jambo Fulani ambalo waliowengi Wameshindwa kuona Dosari hiyo na Dosari hiyo isipodhibitiwa Mapema huenda Kikaleta Madhara Makubwa Baadae. Dosari ambayo inaendelea Kuumiza Vichwa vya Wadau na Wanaharakati wa Kupambana na Udhalilishaji wa Kijinsia ni Mapungufu ya Kisheria katika Baadhi ya Sheria ambazo zinatumika kupambana na Udhalilishaji. Vifungu mbali mbali vya Sheria hizo Zanzibar ambazo huenda ikawa ni Moja kati ya Visababishi vinavyoendelea Kurudisha Nyuma Mapambano Dhidi ya kumaliza Vitendo Vya Udhalilishaji na kutoa Mwanya kwa wale ambao hutenda Makosa haya bila Aibu kuzidisha kasi. Upelelezi wa kesi za Udhalilishaji Haujawekewa Muda Maalum wa kukamilika Upelelezi wake, Utolewaji Hukumu tofauti kwa Watuhumiwa a...