Posts

Showing posts from July, 2026

SIRI ILIYOJIFICHA YA UDHALILISHAJI KATIKA USAFIRI WA UMMA (BODABODA NA DALADALA.

Image
  HABIBA ZARALI PEMBA Katika mitaa ya Zanzibar na maeneo mengine ya mijini, bodaboda na daladala zimekuwa uti wa mgongo wa usafiri wa kila siku. Ni vyombo vinavyorahisisha maisha, vinavyounganisha watu na shughuli zao za kiuchumi, elimu na kijamii. Hata hivyo, nyuma ya urahisi huo wa usafiri, kuna simulizi zinazoumiza za udhalilishaji, unyanyasaji wa kijinsia, na vitendo vinavyotishia utu wa baadhi ya abiria, hususan wanawake, wasichana na wakati mwingine watoto. Wahanga wengi wamekuwa wakibeba maumivu haya kimya kimya, hofu ya kuaibika, kutoaminiwa au kukosa ushahidi wa moja kwa moja imewafanya wengi wasiripoti matukio wanayokumbana nayo. Katika uchunguzi wa makala haya, umebaini hali hiyo  imejenga mazingira ambayo udhalilishaji unaendelea kujificha ndani ya mifumo ya kawaida ya usafiri wa umma hali inayoendelea kuathiri jamii kimya kimya. SAUTI ZA WAHANGA Saa kumi na moja jioni, Asha mkaazi wa Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba (siyo Jina lake halisi) alikuwa akirejea nyumba...
Image
  KUVUNJIKA KWA NDOA NA HATARI ZA WATOTO WA   KIKE KUKATISHA NDOTO ZAO   Na HABIBA ZARALI PEMBA NDOTO za watoto wengi wa kike huanza kujengwa tangu wakiwa wadogo. Wengine hutamani kuwa madaktari, walimu, wanasheria au wataalamu watakaosaidia familia zao na taifa kwa ujumla. Hata hivyo, kwa baadhi ya watoto wa kike, ndoto hizo zimekuwa zikififia na hatimaye kutoweka kutokana na changamoto zinazotokana na kuvunjika kwa ndoa za wazazi wao. Ingawa talaka huonekana kuwa mwisho wa uhusiano wa wanandoa, ukweli ni kwamba athari zake huendelea kuonekana kwa muda mrefu katika maisha ya watoto. Watoto wa kike ndio huonekana kubeba mzigo mkubwa zaidi, wakikabiliwa na hatari ya kuacha shule, kuozeshwa mapema, kukosa malezi bora au kushindwa kufikia ndoto walizojijengea tangu utotoni. Katika Mkoa wa Kaskazini Pemba Wilaya ya Micheweni na maeneo mengine, simulizi za watoto wa kike walioathirika zinaonesha namna migogoro ya kifamilia inavyoweza kubadili kabisa mweleke...