Posts

Showing posts from April, 2026

PACSO YATETA NA WANANCHI KOJANI

Image
MTANDAO wa Asasi za kiraia wa Pemba (PACSO) umeandaa mkutano maalumu kwa wananchi wa Kisiwa kidogo cha Kojani wenye lengo la kuiwezesha jamii kupata uwelewa mpana juu ya masuala ya kisheria na haki za binaadamu. Mkutano huo uliowashirikisha wananchi wa Kisiwa cha Kojani umeandaliwa na jumuiya PACSO kwa ufadhili wa shirika la UNDP na kufanyika huko ukumbi wa skuli ya msingi Kisiwani humo. Akizungumza na wananchi Mkurugenzi Mkuu wa PACSO Pemba Mohamed Najim Omar katika mkutano huo alisema, mpango huo una lengo la kuiwezesha jamii kupata ufahamu wa kisheria na haki za binaadamu. "Jamii zetu bado zina changamoto nyingi na baada ya kuliona hili tumeamua kuandaa mpango wa kupita kwenye jamii kutoa taaluma ya kuwawezesha watu ufahamu juu mambo haya, elimu zinatolewa nyingi lakini na sisi pia tumeona kuja haja ya kuwafikia", alisema.  Aidha alisema, kutokana na kujitokeza masuala mbali mbali ya unyanyasaji wa kijinsia, watoto kudhalilishwa, wanawake, watu wenye ulemavu na hata wazee ...

UMUHIMU WA LISHE BORA KWA MAKUZI YA AWALI YA MTOTO

Image
  Lishe bora ni msingi wa afya na maendeleo ya mtoto. Katika kipindi cha chini ya miaka mitano, mwili na akili hukua kwa kasi kubwa. Tafiti zinaonyesha karibu nusu ya vifo vya watoto hutokana na ukosefu wa lishe bora. Lishe si hiari bali ni uwekezaji wa maisha ya mtoto na jamii.    JEE KWANINI LISHE BORA NI MUHIMU KWA MAKUZI YA AWALI YA MTOTO?  Ukuaji wa Mwili   Protini, wanga, mafuta, vitamini na madini hujenga mifupa na misuli.   Huimarisha nguvu na uwezo wa mtoto kushiriki michezo.   Maendeleo ya Akili   Chuma, omega-3, vitamini B huendeleza ubongo na uwezo wa kujifunza.   Siku 1,000 za mwanzo ni kipindi cha dhahabu kwa maendeleo ya akili.   Kuimarisha Kinga ya Mwili   Vitamini A, C, D na zinc huimarisha kinga dhidi ya magonjwa.   Lishe duni huongeza hatari ya maradhi ya mara kwa mara.    KUZUIA UTAPIAMLO Utapiamlo hujumuisha:   Upungufu wa virutubishi   Lishe isiyo sah...

Umuhimu wa Lishe Bora kwa Makuzi ya Awali ya Mtoto

Image
  NA,Amina Ahmed    Lishe bora ni msingi wa afya na maendeleo ya mtoto.  Katika kipindi ambacho mtoto yupo chini ya umri wa  miaka mitano, mwili na akili hukua kwa kasi  kubwa, na hatua hii huonekana  ukuaji wa mtoto katika maeneo mbali mbali , afya mwili, pamoja na akili. Tafiti za afya ya jamii zinaonyesha kuwa karibu nusu ya vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano hutokana na ukosefu wa lishe bora. Lishe si suala la hiari bali ni uwekezaji wa maisha ya mtoto na jamii kwa ujumla.uwekezaji ambao humuandaalia kesho iliyo bora mtoto. JEE  kwanini  Lishe Bora ni Muhimu  kwa Makuzi ya Awali ya  Mtoto?  Ukuaji wa Mwili Protini, wanga, mafuta, vitamini na madini huchangia ukuaji wa mifupa, misuli na viungo. Lishe bora huimarisha nguvu na uwezo wa mtoto kushiriki michezo na shughuli za kila siku.   Maendeleo ya Akili Virutubisho kama chuma, omega-3 na vitamini B huchangia ukuaji wa ubongo na uwezo wa ku...