Umuhimu wa Lishe Bora kwa Makuzi ya Awali ya Mtoto

 

NA,Amina Ahmed 



 


Lishe bora ni msingi wa afya na maendeleo ya mtoto.

 Katika kipindi ambacho mtoto yupo chini ya umri wa  miaka mitano, mwili na akili hukua kwa kasi  kubwa, na hatua hii huonekana  ukuaji wa mtoto katika maeneo mbali mbali , afya mwili, pamoja na akili. Tafiti za afya ya jamii zinaonyesha kuwa karibu nusu ya vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano hutokana na ukosefu wa lishe bora.

Lishe si suala la hiari bali ni uwekezaji wa maisha ya mtoto na jamii kwa ujumla.uwekezaji ambao humuandaalia kesho iliyo bora mtoto.

JEE  kwanini  Lishe Bora ni Muhimu  kwa Makuzi ya Awali ya  Mtoto?

 Ukuaji wa Mwili

Protini, wanga, mafuta, vitamini na madini huchangia ukuaji wa mifupa, misuli na viungo.

Lishe bora huimarisha nguvu na uwezo wa mtoto kushiriki michezo na shughuli za kila siku.

 Maendeleo ya Akili

Virutubisho kama chuma, omega-3 na vitamini B huchangia ukuaji wa ubongo na uwezo wa kujifunza.

Siku 1,000 za mwanzo (kutoka ujauzito hadi miaka miwili) ni kipindi cha dhahabu kwa maendeleo ya akili na kinga ya mwili.

 Kuimarisha Kinga ya Mwili

Vitamini A, C, D na madini kama zinc huimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa ya utotoni.

Lishe duni hudhoofisha kinga na kuongeza hatari ya maradhi ya mara kwa mara.

 Kuzuia Utapiamlo  ambao ni Utapiamlo ni hali ya kiafya inayotokea pale mtu kukosa lishe bora ya kutosha na kupelekea :

  • Upungufu wa virutubishi (kama protini, vitamini, madini).
  • Lishe isiyo sahihi (kula vyakula visivyo na uwiano mzuri wa virutubishi).
  • Lishe kupita kiasi (kula chakula kingi kisicho na afya, kinachoweza kusababisha unene kupita kiasi na magonjwa yasiyoambukiza),utapiamlo ni tatizo la lishe linaloweza kuathiri ukuaji, afya, na uwezo wa mwili kufanya kazi vizuri jambo ambalo   husababisha kudumaa kwa ukuaji na matatizo yasiyorekebishika baadaye maishani.

Lishe sahihi husaidia kuepuka udumavu na upungufu wa damu kwa watoto.

Aina za Vyakula Bora kwa Watoto wa awali

Kundi la Chakula 

Mfano wa Vyakula

 

Umuhimu

Protini

Maziwa, mayai, nyama, samaki, kunde

 

 

Hujenga misuli na viungo

 

 

 

 

Wanga

Uji wa nafaka, wali, viazi, mikate

 

Hutoa nishati ya mwili

Mafuta yenye afya

Mafuta ya alizeti, parachichi, karanga

 

 

Husaidia ukuaji wa ubongo na ngozi

Vitamini na Madini

Matunda (ndizi, maembe, machungwa), mboga za majani

 

 

Huimarisha kinga na ukuaji wa mifupa

Chakula cha kuongeza damu

Spinachi, maini, dengu

 

Huzuia upungufu wa damu

  Inashauriwa kumuandalia chakula  cha  Asubuhi mtoto alie chini ya umri wa miaka miatano   kama vile ,Uji wa nafaka (mtama, ulezi au mahindi) uliopikwa kwa maziwa,Tunda moja kama ndizi, embe,papain a matunda mfano wa hayo.

Huku Mchana  aweze kula vyakula kama vile ,Wali au ugali pamoja na mboga za majani  mchicha na nyenginezo),Kipande cha samaki au nyama ndogo dagaa  au supu ya mdagaa  samaki kulingana na uwezo  wa mlo wa siku. Pamoja na e cha juisi ya matunda safi.

na kwa wale  ambao wanautaratibu wa kula jioni  inashauriwa kwa mtoto aliechini ya umri wa miaka  5   kula vyakula kama vile Viazi vilivyochemshwa au mikate ya ngano,Mayai au dengu kwa protini pamoja na Mboga za rangi tofauti (karoti, nyanya, pilipili hoho).

Huku vitafunwa bora kwa mtoto vibaki kuwa ni

Parachichi, karanga au maziwa ya mtindi,Matunda madogo kama chungwa au apple.

Ratiba hii inahakikisha mtoto anapata virutubisho vyote muhimu kwa ukuaji wa mwili, akili pamoja na kinga ya mwili.

CHANGAMOTO KWA WALEZI NA WAZAZI

Ukosefu wa uelewa: Wazazi wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu lishe sahihi.

Umaskini: Familia nyingi hukosa uwezo wa kupata vyakula vyenye virutubisho kamili.

Mila na desturi: Baadhi ya jamii hupuuza ulaji wa vyakula fulani kwa watoto, jambo linalozidisha utapiamlo.

Lishe bora kwa makuzi ya awali ya  mtoto ni nguzo ya afya na maendeleo ya maisha yake yote kwani inahakikisha ukuaji wa mwili, maendeleo ya akili, na kinga ya mwili. Familia, jamii na serikali zinapaswa kushirikiana kuhakikisha watoto wanapata chakula chenye virutubisho kamili.

Kila sahani yenye lishe bora ni hatua ya kujenga kizazi chenye afya, chenye uwezo wa kujifunza na kuchangia maendeleo ya taifa.


 

# Mtoto Kwanza

aminaahmedmohd735@gmailcom

MD  digital


Comments

Popular posts from this blog

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

UHABA WA VITUO VYA POLISI WILAYA YA CHAKE CHAKE BADO MLIMA MREFU KUDHIBITI UHALIFU VITENDO VYA UDHALILISHAJI NA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINAADAMU.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.