Posts

Showing posts from June, 2026

UMUHIMU WA VITUO VYA TUTU KWA MAKUZI YA MTOTO

Image
Katika miaka ya mwanzo ya maisha ya mtoto ndipo msingi mkubwa wa ukuaji wake hujengwa. Mtoto mdogo anahitaji mazingira yatakayomsaidia kukuza akili, afya, hisia na uwezo wa kuwasiliana na watu wanaomzunguka.  Vituo vya TUTU vimekuwa sehemu muhimu katika kuhakikisha watoto wa umri wa awali wanapata malezi na elimu inayowaandaa kwa maisha yao ya baadaye. Najua bado unajiuliza Tutu  ni nini lakini kamwe katika masikio lako sio neon geni TUTU ni kifupi kinachotumika kumaanisha Taaluma ya Uangalizi na Ujifunzaji wa Watoto Wadogo. Vituo vya TUTU ni sehemu maalumu zinazotoa malezi, uangalizi na elimu ya awali kwa watoto wadogo kabla ya kuanza elimu rasmi ya msingi. Vituo hivi vinalenga kumsaidia mtoto kukua vizuri katika maeneo mbalimbali ikiwemo ukuaji wa akili, lugha, afya, hisia, tabia na mahusiano na watoto wengine. Katika vituo vya TUTU watoto hujifunza kupitia michezo, nyimbo, hadithi, mazoezi ya ubunifu na shughuli zinazolingana na umri wao. Lengo kubwa la TUTU ni kuhakikisha ...

IJUWE NAFASI YA BABA NA MSAADA KWA MAKUZI YA MTOTO WA AWALI

Image
NA , Amina Ahmed Moh-d Ikiwa  Dunia inaendelea kuadhimisha siku ya Baba Duniani   , kwa kutambua  mchango wake katika Nyanja zote za maendeleo  ,Makala hii imeona ipo haja ya  kuendelea kuikumbusha jamii ya Zanzibar  Nafasi ya baba katika malezi ya awali ni msingi wa ustawi wa taifa.  Ushiriki wa baba si wa kifamilia pekee iwapo utasimamiwa ipasavyo bali ni bali ni wa kijamii na kitaifa katika maendeleo endelevu yanayotokana na uwekezaji katika rasilimali watu. Miongoni mwa  faida kubwa zinazopatikana katika kesho bora ya mtoto ambayo ndio taifa la kesho iwapo Baba atachangia katika maendeleo ya akili na tabia njema za mtoto, akimfundisha usawa, maadili na nidhamu ni kusirki nae kikamlifu katika makuzi yake  ya awali . Hadi sasa  Zanzibar inaaminika kuwa bado jamii ya akina baba ina uelewa mdogo kuhusu malezi ya awali licha ya kampeni mbali mbali za uhamasishaji kutolewa na wizara ya Afya ZNZ kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa ...