IJUWE NAFASI YA BABA NA MSAADA KWA MAKUZI YA MTOTO WA AWALI
NA,Amina Ahmed Moh-d
Ikiwa Dunia inaendelea kuadhimisha siku ya Baba Duniani , kwa kutambua mchango wake katika Nyanja zote za maendeleo ,Makala hii imeona ipo haja ya kuendelea kuikumbusha jamii ya Zanzibar Nafasi ya baba katika malezi ya awali ni msingi wa ustawi wa taifa.
Ushiriki wa baba si wa kifamilia pekee
iwapo utasimamiwa ipasavyo bali ni bali ni wa kijamii na kitaifa katika
maendeleo endelevu yanayotokana na uwekezaji katika rasilimali watu.
Miongoni mwa faida kubwa zinazopatikana
katika kesho bora ya mtoto ambayo ndio taifa la kesho iwapo Baba atachangia
katika maendeleo ya akili na tabia njema za mtoto, akimfundisha usawa, maadili
na nidhamu ni kusirki nae kikamlifu katika makuzi yake ya awali .
Hadi sasa Zanzibar inaaminika kuwa bado jamii ya akina baba ina uelewa mdogo kuhusu malezi ya awali licha ya kampeni mbali mbali za uhamasishaji kutolewa na wizara ya Afya ZNZ kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa malezi na makuzi ya awali kwa mtoto.
Shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF linasisitiza siku 1,000 za mwanzo wa
maisha ya mtoto kuwa kipindi muhimu zaidi, ambapo asilimia 80 ya ukuaji wa
ubongo na mwili hukamilika.
Mpaka sasa Ukuaji wa watoto Zanzibar umefikia asilimia 47 ikilinganishwa na
asilimia 51 Tanzania Bara, ikionyesha pengo linalohitaji juhudi za baba na mama
kwa pamoja katika makuzi yake ya awali yenye mustakabali mzima wa makuzi bora
kwa maendeleo yake .
Dira ya Maendeleo 2050 imeweka rasilimali
watu kama nguzo kuu ya maendeleo hivyo rasilimali hiyo inahitaji maandalizi
kuanzia hatua za awali za rasilimali hiyo ya mtoto ambae ndio
rasilimali mtu.
Ushiriki wa baba katika malezi unahusiana moja
kwa moja na malengo ya kupunguza umasikini, kuongeza elimu bora na kujenga
taifa lenye ustawi wa kijamii na kiuchumi. Malezi bora ya awali yanahakikisha
Zanzibar inafikia hadhi ya hatuta kubwa ifikapo mwaka 2050 kwa kujenga kizazi
chenye afya na maarifa kitakachosaidia taifa hapo baadae.
Changamoto zinazokwamisha ushiriki wa
baba ni pamoja na mila na desturi zinazomfanya baba aonekane kama mtoaji wa
mahitaji pekee, ratiba za kazi zisizotabirika na ukosefu wa elimu kuhusu
umuhimu wa nafasi ya baba, pamoja na migogoro ya kifamilia inayopunguza uwepo
wa baba katika maisha ya mtoto.
Mapendekezo ya kuimarisha nafasi ya baba
ni pamoja na elimu ya malezi kwa jamii nzima ili kubadilisha mtazamo wa
kijamii, sera za kazi rafiki kwa familia zinazomruhusu baba kushiriki
kikamilifu katika malezi, kampeni za kitaifa zinazosisitiza usawa wa majukumu
ya malezi kati ya baba na mama, na ushirikiano wa taasisi za dini na jamii
kuhamasisha baba kushiriki katika makuzi ya awali.
Nafasi ya baba katika malezi ya awali ya mtoto
Zanzibar ni nguzo ya ustawi wa taifa , Ushiriki wake huongeza ukuaji wa
kihisia, kijamii na kielimu wa mtoto na kuchangia moja kwa moja maendeleo yake.
Kila baba ana wajibu wa kushiriki
kikamilifu katika malezi ya mtoto wake, Ushiriki huu si wa kifamilia pekee, bali
ni mchango wa kijamii na kitaifa. Baba anayeshiriki hujenga mtoto mwenye
kujiamini, mwenye ustawi wa kihisia, na mwenye nidhamu na maadili bora.
Siku 1,000 za mwanzo za maisha ya mtoto ni kipindi cha dhahabu, Baba akishiriki
kikamilifu, mtoto hukua kwa afya njema na maarifa thabiti. Ushiriki wa baba ni
uwekezaji wa taifa, unaosaidia kufanikisha malengo ya Dira ya Maendeleo 2050
kwa kujenga kizazi chenye elimu, afya na maadili.
Malezi si jukumu la mama pekee. Ushiriki wako
ni wajibu wa heshima na ni urithi wa kizazi chenye ustawi wa kijamii na
kiuchumi ni maneno ya Ali yahya Omar,mkaazi wa wawi ambae alizungumza na mwandishi wa habari hizi ikiw a ni maoni maalum katika siku ya baba duniani
#Mtoto Kwanza


Comments
Post a Comment