Zijue Mbinu za Viongozi Wanawake walivyofanikisha maendeleo ya Elimu na udhibiti wa utoro kwa wanafunzi skuli za Msingi Na kupelekea kupata Mafanikio Bora katika ufaulu. .
Na Amina Ahmed Moh’d Pemba. MIKAKATI ya kudhibiti utoro skuli za msingi wilaya ya Micheweni imepelekea kuwepo kwa ufaulu mzuri miaka 4 Mfululizo Zanzibar ni kutokana na viongozi wa wilaya kufanya kazi kwa kushirikiana vyema na jamii . Wilaya Ya Micheweni ipo katika Mkoa wa kaskazini ndani ya kisiwa cha pemba ambayo ni moja kati ya wilaya kumi za Zanzibar . Micheweni inaongoza kwa matokeo ya darasa la nne Zanzibar sambamba na kuvuuka lengo liliowekwa na wizara ya Elimu juu ya kudhibiti tatizo la utoro na kuwarejesha skuli wanafunzi wa skuli za msingi waliotoroka. "Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu". Msemo huu umejidhihirisha mara Mgeni khatib Yahya kuendeleza mikakati hiyo ni pamoja na kukemea sherehe za mikusanyiko, ajira za watoto kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa elimu jambo limefanikiwa kuwa bora matokeo ya kitaifa . ...