Zijue Mbinu za Viongozi Wanawake walivyofanikisha maendeleo ya Elimu na udhibiti wa utoro kwa wanafunzi skuli za Msingi Na kupelekea kupata Mafanikio Bora katika ufaulu. .
MIKAKATI ya kudhibiti utoro skuli za msingi wilaya ya Micheweni imepelekea kuwepo kwa ufaulu mzuri miaka 4 Mfululizo Zanzibar ni kutokana na viongozi wa wilaya kufanya kazi kwa kushirikiana vyema na jamii .
Wilaya Ya Micheweni ipo katika Mkoa wa kaskazini ndani ya kisiwa cha pemba ambayo ni moja kati ya wilaya kumi za Zanzibar .
Micheweni inaongoza kwa matokeo ya darasa la nne Zanzibar sambamba na kuvuuka lengo liliowekwa na wizara ya Elimu juu ya kudhibiti tatizo la utoro na kuwarejesha skuli wanafunzi wa skuli za msingi waliotoroka.
"Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu". Msemo huu umejidhihirisha mara Mgeni khatib Yahya kuendeleza mikakati hiyo ni pamoja na kukemea sherehe za mikusanyiko, ajira za watoto kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa elimu jambo limefanikiwa kuwa bora matokeo ya kitaifa .
"Nilipokuja Katika wilaya hii mwaka 2020 Tatizo la utoro lilikuwa lipo linaumisha kichwa na Lilishapigiwa mbio na mwezangu aliepita nilipofika nikaendeleza pale alipowacha".
ni maneno ya Mgeni Khatib Yahya ambae ni mkuu wa wilaya ya micheweni .
SAbabu zilizopelekea utoro Wilaya ya Micheweni
Changamoto kubwa zilizopelekea kuwepo kwa utoro kwa wanafunzi wa skuli za msingi wilayani humo .
"Wazazi walikuwa hawataki Kutoa mashirikiano kudhibiti utoro, Ajira za watoto zilikuwa kila sehemu wengine wanabanjishwa kokoto, wanauzishwa samaki wanapara wengine wanaokota mwani pia wanakosa mda wa kuenda skuli kutokana na kujishughulisha na mambo hayo ilikuwa".
Mikakati ya wilaya kudhibiti utoro baada ya kuwepo kwa changamoto hizo ni ipi!.
Tumeweka mikakati maalum ambayo inasaidia watoto walio na umri wa kwenda skuli wanaendelea na masomo na huo ulikuwa ni muendelezo tu kwangu jitihada zilianza kwa kiongozi aliepita kabla yangu kupanga mikakati".
"Tumepiga marufuku Ajira za watoto maeneo yote mzazi atakaekiuka tunadili nae Jamii imeungana kukemea utoro kurekebisha maadili ya watoto kwa kuunda kamati maalum katika shehia zao" .
" Tumefanya mikutano kuelimisha kila shehia umuhimu wa elimu na malezi".
Maneno ya Mgeni Khatib YahyaAmbae ni mkuu wa wilaya Ya Micheweni.
Baadhi ya wakaazi wa wilaya a micheweni Waeleza kuwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa kwa mitihani ya darasa la nne kwa miaka minne sasa zimetokana na jitihada za wakuu wa wilaya na kupelekea wazazi waliowengi kubadilika.
" Tuliwekewa mikutano Tukaelimishwa Tukaunda kamati ya maadili ya shehia, na kufuatilia maendeleo ya wanafunzi kusifiwa kwa mambo mema kama haya ni furaha kwetu Hassani Ali Abdalla Mzazi shehia ya Majenzi.
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Micheweni mwaka 2020 Wilaya hiyo ilikuwa jumla ya wanafunzi watoro 7609 kw ambao walikuwa nje ya skuli maeneo ambapo wanafunzi hao 3000 kati yao ni wanafunzi wa skuli za msingi .
Wanafunzi 1240 wamesharudishwa skuli rasmi wanaendelea vyema na masomo wanawake ni 892 na 348 wakiwa ni wanaume. ni maneno ya Mgeni kahtib Mkuu wa wilaya ya Micheweni.
Anaendelea Kusema "Mpaka Mwaka 2021 Nilifanikiwa kuwarudisha Skuli Wanafunzi 1118 ambapo mapambano yaliendelea kwa kushirikiana na wizara husika wazazi na masheha kufika mwezi September Idadi ya imeongezeka na wengine 122 wamerudi skuli hao ni wanafunzi wa msingi kumbuka idadi niliokuambia ilikuwa ni pamoja na Sekondari .
Wilaya ya Micheweni Ina jumla ya skuli za msingi 26 katika maeneo na shehia mbali mbali.
Wahusika wanaona juhudi hizi!.
Asya Msellem Hassan ni Afisa elimu skuli za msingi wilaya Ya Micheweni Anasema kuwa suala la utoro kwa sasa limepunguwa ukilinganisha na miaka iliyopita na ufaulu kuongezeka kuanzia mwaka 2018 .
" Hali ya ufaulu ilibadilika wilayani mwetu baada ya kuongoza wanawake kwa mfululizo Bi salama halafu akaja bi Mgeni"
" Salama Mbarouk Alikuja katika wilaya hii nakumbuka mwaka 2017 na hapo mabadiliko ya kudhibiti utoro na kuongezeka na kupanda kwa ufaulu kulianza kidogo kidogo"mwaka 2018 na 19 nakuendelea.
Ongezeko la ufaulu wa wanafunzi skuli za msingi.
Mwaka 2019 jumla ya wanafunzi 107 walifaulu kati ya wanafunzi 1632 ambao walifanya mitihani ya darasa la sita wilayani humo.
ufaulu uliongezeka zaidi mwaka 2020 ambapo jumla ya wanafunzi 1919 waliofanya mitihani 167 kati yao walifaulu jambo ambalo kabala halijawahi kutokea.
Mwaka 2021 wanafunzi 257 walifaulu kati ya wanafunzi 3255 waliofanya mitihani skuli za msingi wilaya hiyo.
Takwimu hizo ni kwa niaba ya Afisa elimu msingi wilaya ya micheweni Asya Msellem Hassan.
Asya Msellem anadai kuwa utoro uliobaki wilaya ya Micheweni kwa sasa sio ule wa moja kwa moja unatofautiana na ule wa miaka iliyopita huku zaidi ukibaki katika maeneo ya ukanda wa pwani.
"Upo ule utoro wa siku mbili siku moja bhasi na zaidi ni skuli ambazo zipo maeneo ya bahari Makangale, Tumbe, Shumba Maziwa ng'ombe hivyo sio ule wa mtoto kukatisha moja kwa moja mkuu wa wilaya anatusaidia kazo hii ya kumaliza utoro micheweni".
Jamii yaaswa
" Wazazi kutengana, kuwatumikisha ajira zisizo lazima kwao endapo kufuatilia mienendo yao wazazi kuishi pamoja tukiyadhibiti haya kwa pamoja hatutoshuka katika ufaulu wala hatutowaangusha viongozi wetu katika mapambano dhidi ya utoro."
Uongozi imara ni moja kati ya chachu ya maendeleo Wanawake hawa ambao waliongoza kwa mfululizo katika wilaya hiyo kumepelekea kuondoa tatizo la utoro lakini pia kusogeza mbele maendeleo ya elimu .
"Zamani watoto walikuwa wanachelewa kulala wanazifuata ngoma popote zinapopigwa hawakataziki lakini aliekuwa mkuu wa wilaya alipotoa marufuku bhasi
Kidogo watoto walilegeza kamba waliogopa wakaanza kutulia majumbani kusoma". Hassan Omar Mkaazi wa Majenzi."
Mara baada ya kuondoka wilayani humo mkuu wa Tangu Mwaka 2017 wilaya ya Micheweni imebahatika kupata viongozi wanawake Salama Mbarouk khatib mpaka kufikia sasa mwaka 2022 inaemdele kuongozwa na Mgeni khatib Yahya
Wilaya yaweka mikakati endelevu kudhibiti utoro na kuendelea kubaki kileleni matokeo ya kitaifa skuli za msingi.
"Kwanza nitaendelea kusimamia suala hilo ili kuona fursa ya upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi wa skuli za msingi inapatikana ipasavyo"
"Kila ambae anawajibu wa kupata elimu ya msingi bhasi nikiwa kama mama kama mlezi bhasi nitahakikisha anaipata kwa gharama yeyote ile".
"Nitahakikisha utoro hatokuwa sababu ya kukwamisha ufaulu nitaendeleza vyema mashirikiano na wananchi wangu."
Jengine " Nitahakikisha wazazi wa wanafunzi wanaendeleza utayari ambao wameanza kunionesha kuhakikisha watoto wao wanaingia madarasani kudhibiti kwa pamoja tatizo la utoro na kuweza kuendeleza ufaulu mzuri .
Jee viongozi wa Shehia ambazo zinalalamikiwa kuwepo kwa utoro zinamchango gani juu ya hili la kidhibiti na kuendeleza ufaulu!
Miongoni mwa shehia ambazo Asya Msellem afisa elimu msingi wilaya ya micheweni alidai kuwa ni moja kati Ya shehia ambazo bado utoro unaendelea ni Makangale, Shumba Tumbe .
"Utoro ulikiwepo kutokana na suala la maji wanafunzi walikuwa wanatumia mwanya huo kufuata maji ya bomba ndio sababu kushuka baharini"
kupara samaki kuokota mwani na kufanya ucheza mwengine lakini kwa sasa mashirikiano ya kamati iliyoundwa shehiani petu na wanakijiji hasubutu mwanafunzi kutoroka wanagopa wakionekana watachukuliwa hatua".
"Tunashukuru tatizo limepungua sana hata walimu wanatuambia na mkuu wetu wa wilaya anapita pita anatoa maelekezo tunashirikiana nae bega kwa bega"
Na sisi tumeweka sheria haswa mzazi atakaeonekana anamtumikisha mtoto tutamchukulia hatua "
Ni maneno yaliotoka kinywani mwa Said Kombo Said Sheha wa Makangale .
Rahila Ramadhan Juma Shehaw shehia Shumba Mjini alidokeza Hali ilivyokuwa awali kuhusu utoro lakini mikakati ya kudhibiti suala hilo n maendeleo yaliofikiwa
" Suala hilo la utoro ilikuwa ni uelewa mdogo wazazi juu ya umuhimu wa elimu ndio husababisha wanafunzi washindwe kudhibitiwa wanakuwa wapo majumbani mwao".
"Halafu kuna tatizo la waalimu Utakuta mwalimu mmoja anashghulikia darasa moja lenye wanafunzi pengine 70 wale atawadhibiti lakini madarasa mengine huku hayana mwalimu hayasimamiwi wanatoroka kwa vile vipindi zaidi ya vitatu darasa halijaingia mwalimu. "
"Wazazi walikuwa hawako tayari kutoa mashirikiano kumaliza tatizo la utoro wala kusimamia wanafunzi wasome lakini kiongozi wa wilaya hii amejitahidi kufanya vikao tunashirikiana na tumefanikiwa hilo utoro umepungua".
"Hali ya ufaulu mfano awali skuli yaa msingi iliyopo shehiani mwangu skuli ya karume ilikuwa haitoi wanafunzi waliofaulu michipuo lakini mwaka jana 2021 ilitoa ni jambo la faraja" .
Sheha wa shehia ya Micheweni Khadija Abdi Haji Kuhusi masualahaya hakuwa nyuma kutoa ya moyoni.
"Ni kiri utoro kwa wanafunzi wa skuli za msingi limefanikiwa kudhibitiwa ni kutokana na kamati maalum ya kusimamia utoro wa wanafunzi na tumefanikiwa juu ya hilo na leo hii limepungua kabisa. "
Baadhi ya wanafunzi ambao walifanikiwa kurudishwa skuli na uongozi wa wilaya hiyo walitoa duku duku lao walipokuwa nje ya skuli sababu wazitaja wadai ni kutokana na kukosa sare kuumwa pamoja na kukosa ufahamu katika masomo yao.
Heri Omar "Nilijiona sifahamu masomo ya skuli nikawa nje ya skuli lakini kwa sasa nimesharudi nawaambia wanafunzi wengine ambao wametoroka warudi skuli tuje tusome.
" Nilikuwa sina sare kwa sasa nishapata naawambia wanafunzi wenzangu warudi skuli waje tuje tusome elimu ni ufunguo wa maisha
Alisema Mwanafunzi Time Makame.
" Fatma Juma Ali ilikuwa naumwa na Kifua nfio mana nikawa siji skuli kwa sasa nisharudi nawaambia wanafunzi wenzangu wasikae utoro waje skuli tusome tupate kufanikiwa" .
Waalimu kwa upande wao waeleza kuwa jitihada za kudhibiti utoro kwa wanafunzi zimetokana na vikao vya walimu wakuu wa skuli zilizomo ndani ya wilaya kupanga mikakati ya pamoja ili kuona tuna ufaulu haushuki.
"Mikakati ikiwemo y walimu wakuu ikiwemo kambi za kusoma muda wa ziada, kamati maalum za skuli kufuatilia watoro jambo ambalo tumefanikiwa kupunguza taatizo la utoro lakini kuongeza ufaulu."
Alisema Mwalim Salum Mkadam Hamad Mwalimu Mkuu Skuli ya Mkanagale Msingi.
Kai Omar Haji kutoka skuli ya Micheweni B msingi aeleza kambi za kimasomo zina mchango mkubwa na kuwa chachu ya maendeleo ya elimu na silaha ya kudhibiti utoro.
"Yaani lazima tujue mwenendo wa mwanafunzi tunakuwa nao mda wote hilo linasababisha utoro usijitokeze kwa sana" .
Wazazi nao watoa wito kwa Wizara
Haata hivvyo baadhi ya wazazi meiomba serikali ya wilaya hiyo kuzidisha mashirikiano katika kulimaliza suala la utoro ambalo kwa sasa limeanza kuleta matumaini ya kumalizika katika wilaya hiyo.
"Watoto wengine ni wasugu kiasi ambacho unaweza ukamsemesha kuhusu skuli kama hakuskii lakini mikakati. yote inayochukuliwa imekuwa Dawa serikali naiomba iendeleze suala hili wazazi tunafurahia kuskia wilaya inatajwa kwa wema sio kwa ubaya"
Faki kombo Hamadi mzazi kutoka Shehia ya Majenzi wilaya ya micheweni.
Wizara ya Elimu ina mikakati gani nayo juu ya hili?
Wizara ya elimu na mafunzo Ya amali pemba Katika kulipatia ufumbuzi suala la utoro kwa wanafunzi wa skuli za msingi wilaya ya Micheweni pamoja na wilaya nyengine Ofisa mdhamini anabainisha mikakati hiyo.
"Upande wa kaskazini pemba tumejenga zaidi ya madarasa miamoja na nane, tumekarabati skuli hata huko makangale tumejenga gorofa la vymba vya madarasa 21 na madarasa haya mwngine ni mapya kabisa.
" Tumeyapeleka katika maeneo ya vijijini ambako kutokana na mazingira watoto hawasahawisahiki husoma, Lakini pia taasisis ya utumishi serikalini tayari imetangaza nafasi za ajira kwa waalimu na karibuni Serikali inakwenda kuajiri waalim
" kwaio miundo mbinu inaimarishwa ajira zinatengenezwa za waalimu na maslhi ya walimu yanaimarishwa ili ufaulu uengezeke sio Micheweni tu hata katika wilaya nyengine.
"Mkakati wetu wizara ya elimu ni kuona tunaimarisha mfumo wa udhibiti wa wanafunzi maskulini Kwa sasa upo lakini bado haujafikia vile ambavyo tunataka sisi wizara,
hivyo tunaendelea kutoa mafunzo kwa waalimu wa madarasa ili waweke vizuri rikodi nani kaja jana nani hakuja nani kamaliza masomo,
jengine tunawaita wazazi kuuliza kuhusu mahudhurio kwanini fulani hakuja tutaweza kudhibiti utoro moja kwa moja,
" Jengine ambalo ni kubwa zaidi tunatoa hamasa kwa wanafunzi ambao watafanya vizuri kuwapa zawadi, si hivyo tu wizara inampango wa kuboresha na kufufu michezo mbali mbali ili iwe kivutio cha watoto kutokutoroka.
Na mkakati mwengine ni kutumia mfumo shirikishi kushirikisha wazazi, walimu pamoja na wanafunzi wenyewe, tunatafuta msaada wa serikali za shehia wilaya mkoa jeshi la polisi pia ili kuona utoro unakoma na watoto wanapata haki yo ya msingi na mikakati yote hii imefanikiwa.
"Aidha mdhamini huyo alisema kuwa kwa sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa waalimu maskulini jambo ambalo ambalo awali lilikuwa halipo.
" Waalimu tuna mabadiliko makubwa kwa sasa tunajitathmini tunaandaa masomo ambayo hayatowachosha watoto, tunatumia mbinu mbadala ikiwemo ziara za kimasomo watoto wanatembea,
Tunatumia teaching aids ambazo zitakuwa zimo ndani ya mazingira yao ili waweze kufurahia masomo sababu wengine hutoroka kutokana na njia mbovu za ufundishaji zina wafanya kurudi nyuma tumewawekea komputa maskulini hiyo yote ni mikakati ya kuongeza ufaulu na kudhibiti utoro.
Hali ya utoro ipoje Zanzibar!.
" Zanzibar nzima ina watoto 35732 ambao wapo nje ya skuli na mikakati wa wizara ni kuwarejesha wanafunzi hao wote katika kipindi cha miaka mitatu" .
"Baadhi ya wilaya imefanikiwa kuwarejesha zaidi ya idadi iliyowekwa kwa mwaka Micheweni ni miongoni mwao kutokana na mashirikiano yao ni jambo la kujivunia" .
Mashavu Ahmada Fakih Msimamizi mradi wa Urejeshwaji skuli wanafunzi watoro skuli za msingi, sekondari na madarasa ya elimu mbdala Zanzibar.
kwa mujibubwa wa takwimu kutoka kwa afisa elimu msingi wilaya micheweni Asya Msellem Hassan anasema hali ya ufaulu awali kabla ya kuongozwa na viongozi wanawake ilikuwahairidhishi kwa miaka zaidi ya mitano.
Hali ya ufaulu kabla ya miaka minne ya viongozi Wilaya ya Micheweni.
2013 Wanafunzi 1601 walifanya mitihani ya darasa la saba wilayani humo 801 wakiwa ni wanaume na na wanawake 800 ambapo kati yao Wanafunzi 13 pekee ndio waliopasi kuingia michipuo
Mwaka 2014 Wanafunzi 1765 wanaume wakiwa ni 819 na wanawake 946 walifaulu walikuwa ni wanafunzi 63.
Mwaka 215 wanafunzi 2443 walifanya mitihani skuli za msingi wilaya ya Micheweni 1247 wanaume 1196 ni wanawake waliofaulu walikuwa ni jumla ya wanafunzi 35 pekee huku idadi ya wanafunzi watoro ikiongezeka.
Kwa sasa Jamii ya Micheweni imehamasika katika suala la elimu na kudhibiti tatizo la utoro ikiwa ni pamoja na mashirikiano.
Nguvu, ushawishi na uwajibikaji waliono wanawake katika kuleta maendeleo ni kweli Mama ni mama Popote "
.
Comments
Post a Comment