WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .
Na Amina Ahmed Muhamed Pemba.
WAZAZI na walezi wameatakiwa kufuatilia kwa ukaribu nyenendo na tabia za watoto pamoja na vijana wao ili kuwanusuru kujiingiza katika tabia hatarishi za kutumia madawa ya kulevya .
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa nchi ofisi ya makamu wa kwanza wa rais zanzibar Harus Said Suleiman katika ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya duniani lililoanadaliwa na mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya zanzibar katika ukumbi wa makonyo wawi chake chake mapema leo.
Amesema bado kuna changamoto kubwa katika malezi na usimamizi wa watoto hususan ni kundi la vijana jambo ambalo linapelekea kuwa na idadi kubwa ya vijana wanaotumia madawa ya kulevya na kupelekea kuharibu maisha yao kwa kujiingiza katika vitendo viovu ikiwemo wizi .
"Bado kuna tatizo katika kusimamia malezi hususan ni vijana wetu jambo hili limepelekea kuwa na idadi ya zaidi ya watumiaji wa madaa ya kulevya wasiopungua elf 15 visiwani zanzibar hivyo wazazi tuzidishe umakini katika malezi ya vijana wetu. alisema.
Akizungumza katika kongamano hilo Kamishna mkuu wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Zanzibar Kanalli Buruhan Zuberi Nasoro amesema kuwa mamlaka hiyo itaendelea kuchukua hatua kali kwa wauzaji na waingizaji wa dawa za kulevya ikiwemo kutaifisha mali zao kwa watakaobainika kuhusika na masuala hayo hatarishi kwa taifa.
"Tutaendelea kupambana na suala hili kwa dhamira ya kulikemea lisiweze kuendelea niwatake wananchi kuendelea kusaidiana na mamlaka kwa kutoa taarifa watakapoona viashiria vya biashara hii ili jamii iweze kuwa salama ".
Kwa upande wake kaimu katibu mkuu ofisi ya makamu wa kwanza wa rais Iliyasa Pakacha Haji amesema kuwa licha ya jitihada zinazoendelea kuchukuliwa katika mapambano hayo bado janga hili linaendelea kuathiri taifa ambapo madhara yake yanapelekea kuathiri taifa.
Nao baadhi ya washiriki walioshiriki katika kongamano hilo akiwemo Othman kombo Ali pamoja na wameiomba serikali na mamlaka hiyo kuwashirikisha wataalamu wa afya CHV kutoa elimu kwa jamii juu ya athari za madawa ya kulevya pamoja na Thani Salim Said mraibu alieacha madawa ya kulevya wameiomba mamlaka hiyo kudhibiti uingiaji wa pombe pamoja na vilezi vilivyozagaa vinavyotumiwa na watoto .
Kongamani hilo lililowashirikisha wanafunzi kutoka skuli na vyuo mbali mbali, vijana kutoka mabaraza ya vijana ,viongozi wa ulinzi na usalama ,wanasheria ,waath usala,viongozi wa serikali watumiaji waliocha madawa ya kulevya,waandishi wa habari Watendaji wa mahakama pamoja na wanachi na wadau mbali mbali .