Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.
- Get link
- X
- Other Apps
SALMA KHMIS - UNGUJA
KATIKA Uongozi wa taifa hili viongozi ambao wako karibu na wananchi na wanapaswa kuhakikisha maendeleo yanafikiwa na yanafanyika ni Masheha.
KATIKA Uongozi wa taifa hili viongozi ambao wako karibu na wananchi na wanapaswa kuhakikisha maendeleo yanafikiwa na yanafanyika ni Masheha.
Masheha wa Wilaya ya Magharib B wamejipanga kuhakikisha maendeleo na mabadiliko yanapatikana ndani ya shehia zao.
Wilaya ya Magharibi B ni miongoni mwa Wilaya tatu zilizomo katika mkoa wa mjini magharib Unguja ambapo Mkoa huo una jumla ya masheha 121 kati ya hao 19 ni wanawake na 101 ni wanaume.
Wilaya ya Magharibi B ni Wilaya iliyotoa shehia 34 kati ya hizo shehia 6 zinaongozwa na masheha wanawake na shehia 28 zinaongwa na masheha wanaume.
Shehia ya kijitoupele na michungwani ni Shehia maarufu zilizomo katika Wilaya ya Magharib B ambazo zinaongozwa na Masheha wanawake.
Shehia hizo kwa kiasi kikubwa zimepiga hatua za kimaendeleo ikiwemo kueka mazingira safi na kupambana na vitendo vya uchimbaji wa mchanga.
Tukianza na shehia ya kijitoupele ambayo ni shehia yenye eneo kubwa zaidi katika Wilaya ya Magharib B ukilinganisha na shehia nyengine ina idadi ya wananchi elf nane mia nne tisini na tatu( 28493) wanawake ni kumi na nane elfu mia saba tisini na mbili (18792)na wanaume ni elfu tisa mia saba na moja (9701) inayoongozwa na Sheha Mwana kheri Ali Pandu na anaeleza ni kwa jinsi gani ameanza safari yake ya Usheha hatua za maendeleo alizozipiga ndani ya shehia yake ukilinganisha na hapo nyuma
" Uteuzi wangu nmeupata tarehe 27/2/2021 ndipo nlipapat nafasi hii ya Usheha na nliupokea kwa hofu nzito sikutarajia kama kuna siku ntakuja kuiongoza jamii, wakati naingia changamoto kubwa iliyokuwepo ni vitendo vya uchimbaji wa mchanga na mazingira machafu na changamoto ya kwanza nliodili nayo ni suala la taka mpaka sasa tumepiga hatua na saiv tunashkur uchimbaji wa mchanga umepungua na usafi unaimarishwa katika shehia"
Alisema Sheha.
Na kwa upande wa Shehia ya michungwani ambayo ni shehia inayoongoza kwa usafi katika Wilaya ya Magharib B yenye wananchi kumi na mbili elfu mia saba sabiini na saba (12777)inayoongozwa na Fauzia Omar Mahawi ambae yeye safar ya usheha aliianza mwaka 2008 katika shehia ya Mombasa na mwaka 2017 aliteuliwa kuiongoza sheia ya michungwanu na kwa kiasi kikubwa amepiga hatua za kimaendeleo za kuhakikisha shehia hiyo inakuwa katika mazingira safi na salama kama Bi sheha huyo anavyotuelezea.
"Changamoto kubwa hasa ni mambo ya usafi kwa kweli tumepiga hatua kubwa sana na tumeweza kujipambanua na tumefikia hatua nzuri ambayo inaridhisha hata viongozi wanasema kama shehia ya michungwani inaongoza kwa suala zima la usafi na tunaongoza kweli sio kama masihara"
Alisema Sheha.
Ni njia zipi walizotumia Masheha hao mpaka kupelekea kupiga hatua kubwa za kimaendeleo wenyewe wanatueleza.
"Tulikuwa tunafanya vikao kila wiki tunaita wazazi na vijana na tunapanga mikakati nin tufanye na tukakubaliana kuunda vikundi vya usafi vya kuchukuwa taka majumbani na wananchi kila mwezi wawe wanalipa elf tatu na hilo likakubalika na mpaka sasa tunaelea nayo"
Walisema Masheha hawo.
Kwa upande wa wananchi wa shehia ya kijitoupele na michungwani hawakusita kueleza mafanikio waliyoyapata toka kuanza kuongoza Mashea hao.
"Kero kubwa ambazo zilikuwa zinatusumbua ni masuala ya usafi na uchimbaji wa mchana lakini toka wameanza kuongoza masheha hawa afadhali kero hizo zimeweza kutatuka na tunashkuru masheha wetu hawana ubaguzi mda wowote unapomuhitaji anakufanyia shida yako"
Pia wananchi hao wameeleza kabla ya kero hizo kutokupatiwa ufumbuzi walikua wanaathirila vipi.
"Kabla ya kero hizo kutatuliwa tulikuwa tunaathirika sana taka zilikuwa zimezagaaa mtaani uchafu mtindo mmoja na uchimbaji wa mchanga siku za mvua mashimo mengi na kuwa ni hatari kwetu sisi na kwa watoto wetu."
Wamesema wananchi hawo.
Lakini mbali ya kuwa Masheha hao wanajitahidi na kupiga hatua katika kuleta mabadiliko na maendeleo katika Shehia zao bado kuna baadhi ya changamoto zimeendelea kukwamisha harakati zao kama hapa wanavyoelezea na namna watakavyokabiliana nazo kuzitatua.
" Bado kuna baadhi ya changamoto ambazo zinaendelea kuturudisha nyuma kama huku shehia ya michungwani shida iliyobaki saiv ni suala la kukosekana kwa mjia safi na salama na tayari nshaliendea mbio sana ila halijapata ufumbuzi ila bado naendelea kupambana nalo"
Wameendelea kusema.
"Na huku kijitoupele suala gumu lilijitokeza saivi ni vijana hawa wadogo wadogo kufanya vitendo vya kupiga watu mapanga na hata kupora na kuwaibia lakini niseme tuu suala hili nmeshaa na kikundi changu cha ulinzi shirikishi na Polis wangu Shehia kuona ni jinsi gani tunaweza kuliondosha suala hilo."
Wamesema Masheha.
Tukiendelea na makala yetu hii tujue kwamba Nafasi ya Usheha ni ya kuteuliwa na sio kuchaguliwa kwa kupigiwa kura na huteuliwa pale tuu unapokua na sifa ya kukubalika katika eneo husika,kujishughulisha katika harakati za wananchi , wananchi wawe wanakukubali, kua na busara na kuweza kutatua migogoro katika jamii kama anavyotuleza Mkuu wa Wilaya ya Magharib B Hamida Mussa Khamisi.
"Nafasi ya usheha kama nafasi ya ukuu wa wilaya au swala la nafasi nyengine ya uteuzi ni nafsi ya kuteuliwa na ili uwe unatakiwa uwe na sifa nzuri katika jamiii na kuhakikisha shughuli zote za kijamii na kisiasa kwenye shehia za kimaendeleo na kiuchumi awe anazijua"
Amesema DC.
Mkuu wa Wilaya huyo pia ameengezea kwa kusema masheha wanawake wanajitahidi sana kutekeleza majukumu na wajibu wao licha ya kuwa wanakumbana na changamoto mbali mbali katika jamii.
"Niwe mkweli na sio kama nasema hivi kwa vile mimi ni mwanamke hapana ila masheha wanawake wa Wilaya hii wanajitahidi sana sana na tumekuwa tukifanya hafla za kuwapongeza wale wanaofanya vizuri na kuwapa miongozo wale wenye kasoro ndogo ndogo za kiutendaji kama sheha wa michungwani mimi namtathmin ni mwanamke anaejiamini , ana uthubutu na hakubali kuonekana hili limemshinda kiufupi masheha wanawak wa wilaya hii wanajiamini na kufanya kazi zao kwa mujibu wa misingi ya sheria."
Amesema DC.
Katika mwaka 2015 Wilaya ya Magaharib ilikua na jumla ya masheha wanawake wawili tuuu tofauti na sasa ni sita hali hiyo
Inaonyesha mabadiliko ya kueka usawa na kuondosha ile dhana ya kuwa mwanamke hawawezi kuongoza .
Sheha ana jukumu la kuunganisha jamii, kutatua matatizo na migogoro inapotokezea na kua ndio dhamana wa Serikali katika eneo lake.
Mkuuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Idrissa Mustaffa amesema wanawake wengi ambao amewateua wanafanya vizuri ukilinganisha na baadhi ya wanaume katika mkoa wake.
"Wanawake wengi ambao nimewateuwa ndani ya Mkoa wangu wanafanya vizuri ukilinganisha na baadhi ya masheha wanaume na nkilinganisha na wakati niloingia mimi na masheha nlowateuwa idadi ya wanawake imeongezeka na wala sina maana waliokuwepo hawakuwa wakiwatahmini wanawake ila ni kadiri tunavyoenda dunia nayo inatutaka tuongeze idadi ya wanawake kwenye ajira kwaio kama ilikuwa asilimia tano saiv imeongezeka mpaka asilimia ishirini."
Amesema RC.
Hapo hapo Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi kuwa karibu na masheha wao na kuwapa mashirikiano ili kufanya kazi vizuri katika kuhakikisha wanaleta maendeleo katika shehia zao.
Msomaji, lengo la makala hiii ni jamii kufahamu mbinu wanazotumia wanawake kuchochea maendeleo na Mamlaka za uteuzi zihamasike kuteua Masheha wengi wanawake.
MWISHO
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment