BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

NA AMINA AHMED PEMBA.
WANANCHI katika  Manispaa ya Mji wa chake chake na Vitongoji vyake walilazimika kuchelewa kakika harakati zao za kujitaftia riziki baada ya usafiri uliozoeleka kwa siku za hivi karibuni wa Bajajj kutoonekana au kuonekana chache kwenye viunga tofauti mapema leo Machi, 6, 2025.
Baada ya hali hiyo kushika kasi huku wananchi wakipigwa na butwaa, mnamo Majira ya saa 3 Asubuhi  Gari za Daladala ikiwemo za Ole Kianga kuanza kuchukua Abiria hao na kuanza kuwasafirisha.

Hata hivyo wakizumzia kutoonekana katika vijiwe vyao kubeba abiria baadhi ya waendesha Balaji walisema kuwa walilazimika kushiriki katika kikao  cha  dharura  kwa ajili ya kujadili  unyanyasaji wanaopata katika mamlaka za serikali ikiwemo Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kupitia mamlaka ya usafirishaji.
Wamesema Mawasiliano na Baraza  MawasilianoJuu kile walichodai kuwa Wamechoshwa na Udhalilishaji wanaofanyiwa na Mamlaka hizo mbili kila siku  zinazohisika na Usafiri Barabarani .
Vijana na Madereva hao zaidi ya  360 ambao wamejiajiri kupitia sekta hiyo rasmi inayotambuliwa na Serikali wamesema Udhalilishaji huowanaofanyiwa  ni pamoja na Ulipishwaji wa fidia kubwa bila ubinaadamu  wala maelekezo  kwa makosa Madogo ,,Kuzuiliwa vyombo vyao, kutozwa shilingi 1000  kila siku bila kuwepo kwa Maboresho yoyote, sambamba na kulipishwa faini siku za Mapumziko na mamlaka hiyo.

Wakizungumza kwa Masikitiko mbele ya Waandishi wa Habari  Waendesha Bajaji hao  kutoka Jumuia ya waendesha Boda boda na Bajaji Mkoa wa Kusini Pemba Pesboa wamemuomba Dk  Mwinyi kuwasaidia  kuzipatia Ufumbuzi Changamoto hizo ambapo Wamesema imani yao imepunguwa kwa viongozi  na maafisa wa Mamlaka hiyo kisiwani humo kutokana na kukosa huruma nao siku hadi siku bila ya kusikilizwa Changamoto zao wala kupata Mashirikiano wanapowaita katika vikao vyao .

Wamesema licha ya Rais Wa Zanzibar kuitambua sekta hiyo  kuwa ni sekta rasmi  ya vijana kujiajiri  lakini bado   Uhuru wa  kufanya kazi hiyo umekosekana kutokana na kadhia wanaozoendelea kukumbana nazo siku hadi siku kutoka kwa Maafisa wa Mawasiliano .

"Tumechoshwa na Mawasiliano  mafaini Makubwa kosa dogo ubinaadamu gani ,faini gani bila hata kuonywa kwanza,Unapigwa faini Mpka jumamosi,siku ambayo si ya kazi, kosa la kutokuvaa kikoti kweli ulipishwe Laki moja usafiri ambao natumia 1500 kwa abiria watatu huruma iko wapi"

Baraza la manispaa kila siku inayokwenda kwa Mungu tunalipia 1000 Ada ya Mji  lakini uo Mji hata Public Toilet hauna zinakwenda wapi fedha zetu tunazotozwa Dk mwinyi vijana wako tunadhalikika.

Kazi za Serikali hatuna bhasi hata tumeshajikubalisha kutuajiri mnatuwekea vikwazo Faini ya laki 3 na Chombo changu kuzuiwa  Kweli hiyo ni haki nikale wapi jee nikaebeau nivute Bangi mpate kutufunga !

"Muhammed Hamad Iddi  ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Waendesha Boda boda na Bajaji Pesboa Pemba Amemuomba Dk Mwinyi Kuziangalia Upya Sheria ambazo zinakuwa kikwazo kwa Vijana waliojiajiri wenyewe katika Sekta hii  ili wasirudishwe nyuma na changamoto hizo za Mawasiliano na kujiinhiza katika vikundi viovu.

Akizungumza Hamad Salim Hamad Mkaguzi  kutoka Wizara ya Mawasiliano  amewataka Madereva hao kufuata Sheria za Usafiri  Barabarani zilizowekwa ili kuondokana na usumbufu huo wa Faini kubwa ambazo zipo kisheria.

Faini kubwa zinakuja kutokana na kuzikiuka sheria zilizowekwa za usafirishaji niawatake madereva kufata sheria kuepusha usumbufu huo
Aidha amesesema Uongozi wa Mawasiliano Utazifanyia kazi Changamoto hizo  kwa kuzifikisha  kwa Viongozi husika  .

Nae kwa upande wake Mkurugenzi Baraza la  Manispaa Chake chake Amesema kuwa iwapo Bajaji hao watatumia maegesho yaliowekwa na serikali kwajili ya usafiri huo baraza halitoshindwa kuwajengea vyoo vya kutumia.

Aidha ameiomba Jumuiya na Madereva hao kuendelea kushirikiana na Serikali  katika kutimiza malengo yaliyokusudiwa ya kuwasaidia vijana kujiajiri kupitia sekta hiyo.

Nao baadhi ya  Abiria wanaotumia Usafiri huo akiwemo Najma Ameir Haji Wamesema Muda mchache baada ya  maderva hao kufanya mgomo wameapata Usumbufu na kusababisha kuchelewa kufika safari zao kwa Wakati.

Umoja huo ambao mara baada ya Dk Mwinyi kuitambua Sekta a ya Boda boda na Bajaji kuwa ni Sekta rasmi umefanikiwa kuzalisha Ajira 480  kwa  Vijana Waendesha Bajaji .

Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI