BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.
NA,AMINA AHMED MOH'D.
JUMLA ya barabara 19 kutoka maeneo mbali mbali kusini na kaskazini Pemba ambazo zitakuwa na urefu kilo mita 99.4 zinatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami na kukamilika ujenzi wake mwezi Disemba mwaka huu 2024 .
Barabara zenye urefu tofauti ikiwemo kubwa yenye kilo mita 12 kutoka Konde makangale mnarani ni mkakati maalum uliowekwa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar kupitia mwaka mpya wa bajeti unaoanza mwezi july .
Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara maalum ya kuangalia utekelezaji wa sekta ya barabara na bandari kisiwani humo katibu mkuu wizara ya mawasiliano ujenzi na uchukuzi Zanzibar Dk Mngereza Mzee Miraji amesema kuwa serikali imedhamiria kuzikamilisha kwa wakati barabara hizo za kimkakati zilizowekwa na wizara hiyo kupitia bajeti mpya .
KATIBU MKUU -WUMU DK,MNGEREZA MZEE MIRAJI.
Amesema barabara nyingi kati ya hizo ni za muda mrefu na ziliahidiwa kufanyiwa matengenezo na serikali jambo ambalo limepelekea kuwekewa mikakati maalum katika ujenzi wake kutokana na kuchelewa kulikosababishwa na changamoto mbali mbali.
Aidha Mngereza amesema kuwa
ili kuwaondolea usumbufu wananchi wake ambapo barabara hizo ziliahidiwa kufanyiwa matengenezo lakini kutokana na changamoto mbali mbali zimechelewa kufanyika kwa matengenezo hayo.
KATIBU MKUU AKIZUNGUMZA NA WANANCH KUHUSU UJENZI WA BARABARA.
Barabara hizi ni za muda mrefu,kuna nyengine zimeahidiwa na serikali ya mapinduzi kwa takriban inafika miaka 10 sasa lakini kutokana na changamoto mbilo tatu hazikuweza kukamilika kipindi icho lakimi serikali imedhamiria ndani ya miezi michache ijayo kuweza kukamilisha izi barabara.
Aidha Mngereza amewatoa hofu wananchi wa maeneo juu ya suala la uharibifu wa vipando pamoja na nyumba zitakazoathirika kutokana na kupisha ujenzi wa barabara hizo ambapo amesema kuwa serikali italisimamia vyema suala hilo katika kuona kila muathirika anapata stahiki yake.
"Tunamshukuru mheshimiwa rais kwa sababu moja kati ya vitu anavyohakikisha anavisisitiza ni pamoja na masuala haya ya kuhakikisha kuwa hakuna mwananchi ambae anakosa haki yake na sisi wizara tunalitekeleza hilo kwa umakini mkubwa kuhakikisha kuwa wananchi hawatoondoshwa bila kupewa fidia kwanza kwa kushirikiana na wenzetu wa wizara ya ardhi pamoja na wizra ya fedha".
Katika hatua nyengine katibu huyo amewataka wakandarasi pamoja na washauri elekezi katika mradi wa ujenzi wa bandari ya Shumba amemtaka mkandarasi mshauri elekezi pamoja na watendaji katika ujenzi huo kuongeza kasi ya ujenzi kwa kuzingatia ubora na wakati uliowekwa wa kukamilika ujenzi huo.
Kwa upande wake afisa mdhamini wizara ya mawasiliano na uchukuzi Ibrahim Saleh Juma amesema kuwa wizara hiyo itasimamia vyema suala la ujenzi wa barabara hizo zilizowekewa mkakati ili kuhakikisha zinawanufaisha wananchi katika shughuli zao kwa kukamilika kwa wakati uliowekwa na kusimamia vyema ujenzi wenye ubora.
Wakizungumza baadhi ya wananchi katika maeneo tofauti ya barabara hizo akiwemo Baraka Ali Mbwana kutoka Kinazini wameeleza shauku zao juu ya ujenzi wa barabaraza hizo ambapo wameiomba wizara hiyo kusimamia na kuzingatia mahitaji muhimu katika ujenzi wa barabara izo ikiwemo uwekwaji wa misingi ya kupitishiwa maji matuta pamoja na kalavati katika maeneo muhimu yanayitumika kwa shughuli mbali mbali.
Kwa upande wake Ramadhan Kiteri mshauri elekezi Mkandarasi Allan Magoma pamoja na Abdalla Salim kaim mkurugenzi shirika la bandari Abdalla Salim Abdalla wamesema kuwa wataendelea kusimamia vyema jukumu hilo la ujenzi wa bandari ya Shumba ili likamilike kwa wakati .
Barabara hizo ambazo zinatarajiwa kujengwa na kampuni ya IRIS maeneo mbali mbali ni Wawi messi Mzambarau mboko ,Mchanga mdogo Mzambarau takao ,Pandani Pembeni ,Micheweni Shumba mjini,Shumba bandarini ,Finya kicha ,Konde Makangale Mnarani ,Kizimbani Uzunguni,,Gando Chaoni ,Gando Chokaani,Bwagamoyo Kele,Uondwe Nyali,Makongeni Kinazini,Barawa Mleteni,Ukutini Mtangani,Mgagadu kwa Otao,Mbuguani Tironi,pamoja na Wesha Mkumbuu.
Mwisho.
Comments
Post a Comment