UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI
Na Amina Ahmed Moh'd ,Pemba.
Pemba UONGOZI wa wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba umesema unaendelea kutambua na kuuthamini n a kuunga mkono mchango unaotolewa na Taasisi ya
" Korea friends of hope international" KFHI kwa wananchi katika shughuli mbali mbali ikiwemo Kuwawezesha kiuchumi na kuwapatia misaada muhimu inayiwasaidia katika maisha.
Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa Wilaya ya Chake chake Abdalla Rashid Ali alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wakulima wakuu wa mazao ya mboga mboga na matunda ikiwemo Tungule,Viazi lishe na matango kutoka mkoa wa kusini Pemba yalioandaliwa na taasisi hiyo huko katika ukumbi wa Tasaf Chake Chake.
Amesema taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia serikali kuimarisha hali za wananchi ikiwemo kuwekeza katika elimu,kilimo na msaada wa vyakula lishe .
Mkuu wa wilaya huyo amewataka wakulima hao kuyafanyia kazi mafunzo hayo ili yaweze kuwaletea tija katika kupata mazao bora yatakayowasaidia kuwawezeaha kiuchumi na kupata lishe inayotokana na vyakula walivyolima.
Katika hatua nyengine mkuu wa wilaya huyo amewataka wazazi na walezi kuendelea kusimamia maendeleo ya watoto katika elimu wanayopatiwa kupitia msaada wa KFHI ili iweze kuwasaidia katika masomo na kuwacha kuwatumia kama nyenzo ya kujipatia kipato kwa kuwatumikisha katika ajira zisizo rasmi kwa maslahi yao.
Hata hivyo ameishukuru taasisi hiyo kwa kuendeleza utaratibu wa kuzisaidia familia maskini msaada wa chakula lishe kila baada ya miezi 3 sambamba na kusaidia gharama za masomo pamoja na matibabu yao.
Aidha amewataka wazazi kuendelea kutoa mashirikiano na kutowavunja moyo watendaji wa taasisi hiyo na kutoa mashirikiano kwa wanafunzi waliopata nafasi ya kwenda Nchini korea kwajiki ya michezo ili waweze kurudi ja ushindi.
Kwa upande wake Sylivia Albath kutoka KFHI amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikisaidia kuleta faraja kwa wananchi wanaoishi katika hali ngumu za kimaisha ambapo jumla ya familia 800 zimefikiwa kutoka shehia mbali mbali ya wilaya hiyo.
Awali akizungumza katika mafunzo hayo afisa kilimo wilaya ya Chake Rashid Muhamed Wema amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuleta mageuzi katika ukulima wa mboga mboga na matunda kwa wakulima wa mkoa wa kusini Pemba.
Licha ya mafunzo hayo kwa wakulima zaidi ya 20 Taasisi hiyo ya Korea friends of hope international" KFHI leo pia imekababidhi msaada wa vipolo vya Mchele kwa familia 800 ambao wanaishi katika mazingira magumu.
Mwisho

Comments
Post a Comment