UMUHIMU WA LISHE BORA KWA MAKUZI YA AWALI YA MTOTO
Lishe bora ni msingi wa afya na maendeleo ya mtoto.
Katika kipindi cha chini ya miaka mitano, mwili na akili hukua kwa kasi kubwa. Tafiti zinaonyesha karibu nusu ya vifo vya watoto hutokana na ukosefu wa lishe bora.
Lishe si hiari bali ni uwekezaji wa maisha ya mtoto na jamii.
JEE KWANINI LISHE BORA NI MUHIMU KWA MAKUZI YA AWALI YA MTOTO?
Ukuaji wa Mwili
Protini, wanga, mafuta, vitamini na madini hujenga mifupa na misuli.
Huimarisha nguvu na uwezo wa mtoto kushiriki michezo.
Maendeleo ya Akili
Chuma, omega-3, vitamini B huendeleza ubongo na uwezo wa kujifunza.
Siku 1,000 za mwanzo ni kipindi cha dhahabu kwa maendeleo ya akili.
Kuimarisha Kinga ya Mwili
Vitamini A, C, D na zinc huimarisha kinga dhidi ya magonjwa.
Lishe duni huongeza hatari ya maradhi ya mara kwa mara.
KUZUIA UTAPIAMLO
Utapiamlo hujumuisha:
Upungufu wa virutubishi
Lishe isiyo sahihi
Lishe kupita kiasi (unene kupita kiasi)
Matokeo:
Kudumaa kwa ukuaji
Matatizo yasiyorekebishika baadaye
AINA ZA VYAKULA BORA KWA WATOTO WA AWALI
Kundi la Chakula Mfano wa Vyakula Umuhimu
Protini Maziwa, mayai, nyama, samaki, kunde Hujenga misuli na viungo
Wanga Uji wa nafaka, wali, viazi, mikate Hutoa nishati ya mwili
Mafuta yenye afya Mafuta ya alizeti, parachichi, karanga Ukuaji wa ubongo na ngozi
Vitamini na Madini Matunda, mboga za majani Kinga na ukuaji wa mifupa
Chakula cha kuongeza damu Spinachi, maini, dengu Huzuia upungufu wa damu
RATIBA YA MILO BORA KWA MTOTO CHINI YA MIAKA 5
Asubuhi:
Uji wa mtama/ulezi/mahindi kwa maziwa
Tunda moja (ndizi, embe, papai)
Mchana:
Wali/ugali + mboga za majani
Kipande cha samaki/nyama/dagaa
Juisi ya matunda safi
Jioni:
Viazi/mikate ya ngano
Mayai/dengu
Mboga za rangi tofauti (karoti, nyanya, pilipili hoho)
Vitafunwa Bora:
Parachichi, karanga, maziwa ya mtindi
Matunda madogo (chungwa, apple)
CHANGAMOTO KWA WALEZI NA WAZAZI
Ukosefu wa uelewa kuhusu lishe sahihi
Umaskini wa familia
Mila na desturi zinazopuuza vyakula fulani
Hitimisho
Lishe bora ni nguzo ya afya na maendeleo ya maisha ya mtoto.
Familia, jamii na serikali zinapaswa kushirikiana kuhakikisha watoto wanapata chakula chenye virutubisho kamili.
Kila sahani yenye lishe bora ni hatua ya kujenga kizazi chenye afya.
📞 255 6859184
📧 aminaahmedmoh@gmailcom
🏷️ MD digital
🔖 #MtotoKwanza
Comments
Post a Comment