WADAU WA KUPAMBANA NA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE NA WATOTO WALIA NA SHERIA NAMBA 7 YA MWAKA 2018 , SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI, WAOMBA KUFANYIWA MABORESHO BAADHI YA VIFUNGU VYAKE.

NA AMINA AHMED MOH’D - PEMBA 

"USIPOZIBA Ufa Utajenga Ukuta  " Ni Msemo Ambao Mara Nyingi unapotumika  Huashiria kuwepo kwa Dosari ya Jambo Fulani ambalo waliowengi Wameshindwa kuona Dosari hiyo  na Dosari hiyo  isipodhibitiwa Mapema huenda Kikaleta Madhara Makubwa Baadae. 

Dosari ambayo inaendelea Kuumiza  Vichwa vya Wadau na Wanaharakati wa Kupambana na Udhalilishaji wa Kijinsia ni Mapungufu ya   Kisheria  katika Baadhi ya Sheria ambazo zinatumika kupambana na  Udhalilishaji. 

 Vifungu  mbali mbali  vya Sheria  hizo Zanzibar ambazo  huenda ikawa ni Moja kati ya Visababishi  vinavyoendelea Kurudisha Nyuma Mapambano Dhidi ya kumaliza Vitendo Vya Udhalilishaji  na kutoa Mwanya kwa wale ambao hutenda Makosa haya bila Aibu kuzidisha  kasi. 

Upelelezi wa kesi za Udhalilishaji Haujawekewa Muda Maalum wa kukamilika  Upelelezi wake, Utolewaji Hukumu tofauti kwa Watuhumiwa ambao wamefanya  Makosa yenye kufanana, Kuwepo kwa Hukumu Ndogo ambayo  imewekwa kwa Mujibu wa Sheria  kwa wanaotiwa Hatiani, Vifungu ambavyo vimetoa hukumu  Kubwa Kwa Wanaotiwa Hatiani  juu ya Makosa haya bila Waathirika wanaofanyiwa Vitendo hivyo kufaidika na Chochote Juu ya Hukumu Hizo zilizowekwa na Sheria. 


NI IPI SHERIA HIYO INAYOUMIZA AKILI ZA WANAHARAKATI WA KUPAMBANA NA UDHALILISHAJI! 

Moja kati ya Sheria  ambayo imebeba vifungu vya Kusimamia Masuala ya Udhalilishaji ni Sheria Namba ( 7 ) ya Mwaka 2018  Sheria Ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Ambayo baadhi ya vipengele Vimekuwa Vikirudisha nyuma Mapambano hayo. 

Kifungu cha 7 cha  Sheria  Namba 7 Mwaka 2018  kimeweka Mamlaka Kwa Mahakama ya Mkoa  kutoa Adhabu ya kifungo Kisichozidi Miaka 14 na Faini  Isiyozidi Milioni  14" . 

  Kifungu cha Adhabu kwa Makosa ya Udhalilishaji, Ulawiti, Kuingilia Kinyume na Maumbile, Kubaka kifungu  109  kifungu  kidogo cha  1 kimesema kuwa "Adhabu kwa Kosa la Kubaka  Ni kifungo Cha Maisha  au Katika Mazingira Mengine yeyote, Adhabu isipungue Miaka 30". 

Hata hivyo Sheria ipo Kimya juu ya kuchukuliwa Hatua za kisheria kwa Waathirika na Familia za Waathiriwa wa Makosa ya Udhalilishaji wanaokataa kutoa ushirikiano kwenye kesi  . 

 Sheria hii ipo Kimya  Juu kucheleweshwa kupewa Mwenendo wa Kesi kwa  kesi ambazo  wakili wa Serikali amekata Rufaa. 

Moja kati ya Maswali Ambayo yanaendelea kukosa Majibu katika Vichwa vya Wananchi  waliowengi ni Suala hili la Kutolewa hukumu Tofauti kwa wale ambao Mahakama imewatia Hatiani kwa Makosa yanayofanana. 

Kukosekana kwa Usawa katika Utolewaji wa Hukumu katika Kesi  za Udhalilishaji umekuwa sio Jambo  Geni katika Masikio ya Waliowengi Unguja na Pemba . 

Vyombo vya Habari Vimekuwa Vikitoa  Siku hadi Siku Kesi Mbali mbali zenye Mfanano na Kosa  sawa  Lakini   Hukosekana Mfanano katika Hukumu zake Zinapotolewa  na Mahakama. 

"Mfano  Kesi  za Ubakaji, Watenda Kosa Wawili Ambao wamehukumiwa  katika Mahakama Tofauti Huripotiwa katika Mahakama Za Mkoa Unguja Na Pemba  huripotiwa  wakiwa wameshatolewa Hukumu tofauti huku wapo ambao huhukumiwa kutumikia Chuo Cha Mafunzo Kwa Kipindi kifupi, na wapo ambao hutumikia kwa kipindi Kirefu la kushangaza wakiwa na Kesi zenye Kufanana. 

  WANANCHI  PAMOJA NA WANAHARAKATI WANA MITAZAMO GANI JUU YA SUALA HILI! 

 " Jamii Imekosa Hofu  Juu ya Hukumu zinazotolewa na Mahakama  zetu Leo Unasikia Fulani Kabaka Mtoto wa  Miaka 11 Kafungwa Miaka 14  na Faini halipi Mwengine  Kalawiti  Mtoto kafungwa Miaka 7 na Faini  halipi  Sababu hatujui lakini Akili zetu zinaamini ni Rushwa kwa vile Makosa yamefanyika  yapo sawa Alisema  Abuu Bakar Zubeir  Ali  Mkaazi wa Chanjaani  Chake Chake. 

 "Binafsi mimi Mpaka  leo sijajua Hatma ya Mtoto Wangu wa Miaka 9  Ambae Alibakwa Mahakama ikamtia  Hatiani Mtuhumiwa na Ikaamuru atumikie Chuo Cha Mafunzo Miaka 14 na faini shilingi Milioni 2 Lakini Mpka Leo hii Mtuhumiwa Yupo chuo Cha Mafunzo  lakini bado faini hatujaipata ni kama  ilitajwa tu kule Mahakamani. ".

" Nilijaribu Kufuatailia juu ya fidia hiyo lakini  nilitakiwa nifungue kesi Mpya ya Madai, Naamini yasingekuwa hayo kama kungekuwa na sheria ambayo ingeweka ulazima wa Kulipa hizi fidia baada ya Mahakama kutoa Hukumu. 
 Alisema Baba  Mzazi wa Mtoto aliefanyiwa Udhalilishaji   Madungu  Chake Chake ambae Jina linahifadhiwa. 

 " Kesi zinaripotiwa Nyingi Wananchi Wameamka  sana kuyaripoti haya Matukio  yanapojitokeza Masuali yamebaki mbona hakuna Mabadiliko   kutokana  hukumu zinazotolewa Bado yanendelea kujitokeza  , Kama hofu imeondoka juu ya baadhi ya watu na kufanya Matendo haya ya kikatili huku sheria zikikaa kimya  au zikiwa zinakinzana hatutofika Popote Kupambana na Udhalilishaji  Serikali na Wadau waangalie kasoro iko wapi kwenye hili. 

"Sina Uzoefu katika Mambo ya Sheria lakini Uzoefu wa kusikia haya Matukio kuripotiwa  Kwa Adhabu tofauti ninao,  nishasikia zaidi ya Mara Moja Mbakaji Wete kagungwa Miaka 30 Chake Chake Chake Miaka 14  Kama tatizo ni ukinzani wa Sheria Tunaiomba Serikali Iliangalie Suala hili. Alisema Abeda Ali Seif   . 

" Haiwezekani Kabisa Na ni udhaifu Mkubwa alietenda kosa  Wete Na Alietenda kosa Chake  hilo hilo wakahukumiwa Tifauti hapo kuna dosari kama sio ya Kisheria bhasi huenda kuna Tumika Rushwa kwa mtazamo wangu ni jambo la Aibu kiukweli. 

" Sisi Kama wadau  wa Kupambana na kupinga   Vitendo vya  udhalilishaji Tunatamani kuona Mabadiko ya Haraka   Na kuwepo Na Sheria Moja tu ambayo itasimamia masuala haya  ya Udhalilishaji  Utitiri wa Sheria  Tumebaini kuwa ni Changamoto inayorudisha nyuma Mapambano haya   kwa sababu kila Mahakama inatoa. 

Hukumu kwa  kufuata sheria Yake    kungekuwa na Sheria Moja juu ya Maswala haya naamini kusingekuwa na hizo adhabu tofauti kwa watenda Kosa wa aina Moja". Ni Maneno ya Fat hiya Mussa  Said Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Zanzibar Ofisi ya Pemba. 

" Tunajitahidi kwa Nguvu zetu Zote Kupambana na Udhalilishaji  Tukiwa kama Wanaharakati ambao Tunaguswa Moja kwa Moja juu ya Suala hiliDosari Ni nyingi zilizomo katika Sheria si hiyo tu Ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na Hata nyengine ambazo zinazasimamia Udhalilishaji zina Mapungufu". 

 "Niseme suala hilo la kuwepo kwa sheria nyingi Ambazo zinasimamia Vifungu vinakinzana ni  Dosari Kuna haja ya kusimamia hili kuona kuna patikana Sheria Moja Tu ya Udhalilishaji. Tatu Abdalla Msellem Mwanaharakati Wa kupambana na Udhalilishaji kutoka Jumuia ya Tumaini Jipya  Pemba. 

 Hassan Hamza  Msellem ambae ni Mwandishi wa habari za Jinsia anasema kuwa  "Tumekuwa Tukipokea lawama nyingi Tunapomaliza kutangaza Taarifa zetu , Jamii imekuwa ikitulaumu Wanasema mbona Fulani kapata Miaka Mingi, mbona  Huyu  Hachukuliwi  Hatua Yule kapewa Miaka kidogo kana kwamba sisi ndio tuliotoa Maamuzi. 

" Wapo kabisa ambao Wanahisi Mahakama hazitendi Haki juu ya Kesi hizi, Wengine kupata Hukumu Ndogo, Wengine kubwa Kesi zenye Kufanana Wanaona kama  Rushwa ndio imetumika  kuwe na ulazima wa serikali kukaa na Wadau na Wanasheria kuangalia hizi Geps kuona zinarekebishwa. 


JEE ! NINI  HUSABABISHA UTOFAUTI HUU WA UTOLEWAJI WA HUKUMU ?. 

 "Mahakimu kuwa na Mamlska Kisheria kutokana  kuwepo kwa Baadhi ya Vifungu ambavyo   Vinatoa Mwanya wa Hukumu   Ndogo ambayo imewekewa Ukomo  na vile Ambavyo Vimetoa Hukumu kubwa Ambayo haijawekewa Ukomo  Endapo Mtu atatiwa hatiani  na Mahakama juu ya  Makosa yote ya  udhalilishaji  ikiwemo Ubakaji".

Ukizani wa  Vifungu hivi vya Sheria Umempa  Mamlaka Hakimu  yeyote wa Mahaka za Mkoa kutumia Moja kati ya vifungu hivi Wakati Wanapofanya Maamuzi ya kutoa Hukumu kwa wanaotiwa  Hatiani Jambo ambalo hupelekea  kukosekana kwa Hukumu sawa kwa Watendaji wa Makosa yanayofanana. 

Licha ya Mamlaka hayo Lakini pia Vifungu vya Adhabu ndani ya Sheria hiyo Pia vimeonesha  Ukinzani Juu ya Mamlaka hayo kutokana na Adhabu Kubwa ambazo  Zimekuwa na Ugumu kutekelezwa kwa Mujibu wa Sheria na kupelekea Kesi za Udhalilishaji kuendelea kuripotiwa Siku hadi Siku bila watendaji wa Makosa hayo Kuingiwa Hofu Alidai  Ali Amour Makame  Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Pemba. 

Kuna  Mahakimu Wengine  wa Mahakama Ya Mkoa (Wanafunga) Wanapeleka  Chuo Cha Mafunzo Miaka 30 , Lakini kuna Wengine Wanapeleka  Chuo Cha Mafunzo (Wanafunga) Miaka 14  ni kutokana na Kufuata  Sheria hii ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kuwa imetoa Uhuru kwa Mahakimu Wa Mahakama za Mkoa  Kufuata Vifungu hivi  Ambavyo vimewapa Mamlaka kisheria Alifafanua  Mwanasheria Huyo. 

NI YAPI MAONI YA WADAU JUU YA SHERIA HII ZAIDI KATIKA  KUTOA ADHABU SAWA KWA WANAOTIWA HATIANI KUFANYA KOSA LA AINA MOJA. 

"Mimi Maoni yangu Mahakama za Mkoa zitoe adhabu sawa  ikiwa Alietenda kosa la Ubakaji atapata adhabu ya Kifungo cha Miaka 30  na Faini  bhasi iwe hivyo kwa wote Mahala Popote  ili kusiwe na ukizani wala Tofauti Alishauri Ali Amour Makame. 

Bora Mahakama zote wafuate kifungu Cha Adhabu  ambacho kimetoza adhabu kuwa Watuhumiwa wote  wa Makosa hayo ya jinai wafungwe Miaka 30 wasitofautiane Aliongeza. 

" Serikali Iweke Sheria ambayo Itaweka ulazima wa kulipwa izi Fidia  Ili waathirika wa matendo haya wapate fidia Kwa sababu zinaishia kusemwa tu hazitolewi  Jambo ambalo halieti Tija yeyote zaidi ya Maumivu ya Kwa Waathirika na hii itawezekana Endapo Kutakuwa na Sheria Moja ya Udhalilishaji ambayo Itaangalia yote haya na kurekebishwa.  Fat hiya Mussa Said. 

Waandishi Wa Habari Wanamchango Mkubwa juu ya Hili Watusaidie kuoneshana kusemea hizo Dosari  ambazo kwa sasa zinaonekana ni ndio lakini Madhara yake ni makubwa na Niendelevu  ili  kupatikane Marekebisho. 

 kwa Kiasi kikubwa  Vifungu vya Sheria hii Vinawapa Nafasi Wanaofanya Makosa kupata Mwanya  Wakuendeleza Makosa yao na ndio maana hayamaliziki katika Jamii Sheria  Bado Hazijawabana, Endapo Maboresho katika Sheria hii na nyengine zitaondolewa zile Dosari ambazo  zimetoa Mwanya   na kupatikana Sheria Moja Madhubuti itakayosimamia Udhalilishaji  huenda Vitendo hivyo vikapungua na Kumalizika Kabisa. 

Mwisho 



Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.