WAANDISHI ,WAMILIKI WA VYOMBO WAHIMIZWA KUANDIKA HABARI ZA MICHEZO KWA WANAWAKE HUKU VIONGOZI WA SERIKALI WAKIASWA KUTEKELEZA KWA VITENDO SERA YA MICHEZO KWA WOTE ILIYOWEKWA NA SERIKALI ZANZIBAR.

.


Na, AMINA AHMED
 PEMBA.
WAMILIKI na waandishi  wa  vyombo mbali mbali  vya habari  wametakiwa kutoa kipaumbele katika kuandika na kutangaza  habari zinazo gusa maendeleo na changamoto   katika sekta   ya michezo kwa wanawake  ili kukuza  ushiriki wa kundi hilo katika michezo kisiwani Pemba.

Kauli hiyo imetolewa na   Mwandishi mwandamizi Zanzibar   Hawra Shamte,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali kisiwani  humo wanaoendelea kushiriki katika mafunzo ya siku 5  ya kujengewa uwezo juu ya kuandika habari za  ushiriki wa michezo kwa wanawake yaliondaliwa na  TamwaZanzibar katika ukumbi wa ofisi  za chama hicho  Mkanjuni Chake Chake .

Amesema bado mchango wa   waandishi na vyombo vya habari  Zanzibar  umekuwa hauridhishi  katika suala la utoaji wa habari zinazogusa michezo kwa wanawake jambo ambalo linaendelea kurudisha nyuma  na kupelekea kukosekana hakasa kwa wanawake  kujiingiza katika michezo  visiwani humo.

Aidha Hawra  ameitaka jamii kuendeleza uwezeshaji wa wanawake na wasichana, katika michezo mbali mbali  ikiwa ni pamoja na kuwacha mila potofu na mitazamo hasi  juu ya ushiriki wao katika michezo .

Mwandishi huyo mwandamizi akatumia fursa hiyo kuwaomba viongozi na watendaji wa sekta za Michezo  kuifanyia kazi sera ya  Michezo  iliyowekwa  na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Michezo kwa wote ( "Sport for All " )yenye lengo la kuweka usawa wa kijinsia katika michezo.

Kwa Upande wake Mratibu wa chama cha waandishi wa habari Tamwa Zanzibar Ofisi ya Pemba Fat hiya Mussa Said amewataka waandishi hao kuwa waandishi wa mabadiliko katika kuwasaidia wanawake visiwani humo kuitumia haki hiyo ya ushiriki wao  katika michezo mbali mbali ili kuweza kujipatia maendeleo  wanayoyakosa kutokana na kutokushiriki ipasavyo  katika michezo mbali mbali.

Mafunzo hayo ya siku Tano kwa waandishi hao kisiwani humo ni katika utekelezaji wa  mradi wa  kukuza usawa wa Kijinsia katika Michezo (Cohort Gender and Sports) ambao umeanza mwezi March mwaka  2024 na kutarajiwa kukamilika February 2025  ambapo zaidi ya waandishi wa habari 20 Unguja na Pemba wamepatiwa mafunzo hayo ya kujengewa uwezo katika uandishi wa habari za michezo kwa wanawake  .

Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.