MBINU BORA ZINAHITAJIKA KUHAMASISHA JAMII

NA FATMA SULEIMAN- PEMBA. 


KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo bi  Fatma Khamis Rajab amewataka wadau wa lugha ya kiswahili kubuni mbinu bora na katika kuhamasisha jamii na kupata wadau wengi ili kuinyanyua zaidi lugha hiyo pamoja na  kuunga mkono juhudi za raisi wa Zanzibar katika kukikuza kiswahili ndani na nje ya nchi.

Ameyasema hayo wakati akiahirisha Kongamano la 6 la Kiswahili la Kimataifa liloambatana ziara maalum ya kutembelea sehemu za kihistoria huko Mnara wa Kigomasha Shehiya ya Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Aidha Katibu mtendaji BAKIZA Bi Saade Mbarouk ametumia fursa hiyo kuwaasa vijana kujitoa katika kujifunza kiswahili kwani Baraza lina mpango wa kuanzisha mafunzo ya kiswahili kwa wageni jambo litakalosaidia kupata fursa hasa kwa vijana.
 
Akitaja mchango wa mabaraza ya kiswahili Konsolata Mushi Katibu Mtendaji BAKITA amesema mabaraza yameweza kuleta tija kwani yanasimamia maendeleo ya matumizi ya lugha hiyo kikanda, Kitaifa na Kimataifa kwa kutoa fursa za  kuwafunza wageni.


Magdalena Macha mmoja wa washiriki wa kongamano amesema amejifunza mambo mengi kupitia ziara hiyo kwani amejua historia za sehemu tofauti za kihistori ikiwemo, Msitu wa Ngezi Pango la mtoro sambamba na Mnara wa Kigomasha Uliojengwa Mwaka 1904 na kampuni ya Chancy Brother ya Uengereza.

Mnara Kigomasha ni moja ya sehemu za kihistoriazilizomo katika Shehiya ya Makangale ambapo wenyeji na wageni hupata fursa ya kutembelea lengo kujifunza mbambo tofauti.

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI