Shamra shamra kuelekea siku ya Rushwa

Na Fatma Suleiman Pemba. 


Tarehe 9 Disemba duniani kila mwaka huadhimisha siku ya Kupambana na Rushwa   ambapo serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kupitia ZAECA inaungana na Mamlaka nyengine  katika kupinga  Vitendo hivyo vya Rushwa na Uhujumu uchumi. 

Katika kuelekea siku hio zaeka  Mkoa wa Kusini  Pemba imefanya matembezi  yaliyokuwa na lengo la uhamasishaji wananchi juu ya kupinga vitendo vya Rushwa na Uhujumu Uchumi. 

Katika matembezi hayo yaliyoanzia benk Chake Chake hadi Uwanja Gombani yaliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Chake Abdalla Rashid Ali ambapo vikundi vya Mazoezi  na  wananchi pia walishiriki. 
 
Akizungumza mara baada ya matembezi hayo Mkuu wa Wilaya ya chake chake Abdalah Rashid Ali amesema matembezi hayo ni muhimu saba kwani yanaunga mkono jitihada za serikali za kupambana na rushwa visiwani hapa


Kaimu kamanda wa zaeka mkoan WA kusini Pemba amesema wamejipanga kuhakikisha wanafikia ma lengo ya kupambana na rushwa kwa kuzuia kufanyika kwa Matendo ya rushwa ikiwa ndio mpango wa kwa za wa mamlaka hiyo. 


Akizungumza kwa niaba ya wanavikundi vya   mazoezi ya viungo ameuomba uongozi wa zaeka kujitahidi kusimamia ipasavyo majukumu Yao Ili kuhakikisha wanaicha jamii kuwa salama .

Kamimu kamanda wa ZAECA Mkoa wa kaskani pemba Nassor Hassan Nasiir amewaambia wananchi kuwa maendeleo bila ya Rushwa na Uhujumu Uchumi inawezekana hivyo ni vyema wananchi kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo hivyo .

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI