Wadau na Serikali Tuungeni Mkono Kujikomboa na umasikini
Na UWEISIYA KHAMIS - UNGUJA.
UMOJA wa Kikundi Cha Akina MamaJambo Nia kinachojishughulisha na Ushonaji wa Mazulia, Vipochi, Kamba za Usumba, Mikoba ya Ukili, Pamoja na Mashuka, Kilichopo Shehia ya Kiungoni Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja Wameiomba Serikali Pamoja na wadau wa Maendeleo Kuwasaidia Kupata Soko la Uhakika la kuuzia Bidhaa zao pamja na Elimu itakayowasaidia kuongeza ujuzi katik Kazi zao wanazozizalisha.
Wakizungumza na Mwandishi wa Habari aliefika katika Ofisi zao zilizopo Mtaa wa Sheba Makunduchi baadhi ya akina Mama wa Umoja wa Kikundi hicho Akiwemo Fatma Ali Makame Amesema kukosa Soko la uhakika pamoja na Elimu ya Uzalishaji kunapelekea kurudisha nyuma harakati zao za Maendeleo kutokana na Kutegemea kuendesha maisha na familia zao kila siku kupitia Kazi wanazozizalisha.
AKINA MAMA KIKUNDI CHA JAMBO NIA - MAKUNDUCHI
Amesema Kupitia Shughuli wanazozizalisha katika kikundi hicho wameacha utegemezi na huendesha shughuli zao ikiwemo kuwasomesha watoto, pamoja na kukidhi mahitaji yao mbali mbali.
Aidha Fatma Ambae pia Ni Mwenyekiti wa kikundi hicho Amesema kuwa licha ya Changamoto hizo kikundi cha Jambo Nia kimekuwa kimbilio kwa akina mama wengi na kusaidia majukumu Mengi ya familia katika Majumba yao ikiwa ni pamoja na ulipaji wa ada na ukataji wa Sare za watoto Skuli, na Madrsa.
Akizungumza juu ya changamoto hiyo Afisa Ushirika Wilaya ya Kusini Unguja Salum Abdalla Salum Amesema Changamoto za Soko Mtaji na Elimu zinaendelwa kupatiwa ufumbuzi na Serikali ikiwemo Kujemgewa Masoko maakum ya kuuzia biashara zao.
Aidha Afisa huyo amewataka wanakikundi hicho kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja na kuomba Mikopo kuoitia wizara ya uwezeshaji wananchi kiuchumi Zanzibar il kuweza kuondokana na tatizo la Mtaji.
Ushirika wa akina Mama hao Jambo Nia ulioanzishwa Mwaka 2007 umekuwa ukipata fursa mbali mbali za kutangaza Biashara zao katika Sehemu za Maonesho huku jumla ya akina mama 42 wakiendelea kunufaika na kikundi hicho kinachozalisha bidhaa mbali mbali za Mikono.
Mwisho.
Comments
Post a Comment