MKURUGENZI WA MASHTAKA ZANZIBAR AFANYA ZIARA KISIWANI PEMBA.
Na AMINA AHMED MOH’D.
Mkurugenzi wa mashtaka Zanzibar Mgeni Jeilani Jecha Amewataka watendaji wa Ofisi hiyo kisiwani pemba kufanya kazi na Kusimamia majukumu yao kwa kutenda haki na kufuata sheria ikiwa ni pamoja na kutojihusisha Katika vitendo vya rushwa .
Ametoa ombi hilo Alipokuwa akizungumza na wafanya kazi wa Ofisi hiyo Madungu Chake Chake pemba katika Ghafla maalum ya kuzungumza na kujitambulisha kwa ikiwa ni siku chache mara baada ya kuapishwa kuongoza nafasi hiyo.
Amesema Ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ndio iliyobeba dhamana ya nchi katika kuchunga kusimamia na kutoa haki bila upendeleo hivyo ni vyema kuiendeleza sifa hiyo kwa kutokujihusisha na vitendo visivyofuata maadili ambavyo vitapelekea kuondoa uaminifu huo kwa wananchi.
Akizungumza katika ghafla hiyo Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Mwanamkaa Abdul Rahman Muhammed amewataka watendaji na wafanya kazi wa ofisi hiyo kuendelea kutoa mashirikiano kwa kiongozi huyo ili kuongeza ufanisi katika kusimamia na kuongoza vyema majukumu aliyopewa na serikali.
Awali wakitoa neno la shukurani kwa niaba ya wafanya kazi wa ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka pemba Mwanasheria dhamana kisiwani humo Ali Haidar Muhammed pamoja na wakili wa serikali kutoka ofisi hiyo wamesema wataendelea kutekeleza na kusimamia majukumu ya uendeshaji kupitia, kutoa ushauri kupokea malalamiko kwa vyombo husika, sambamba na kuendeleza mashirikiano kwa kufany kazi kwa bidii.
Ziara ya mkurugenzi huyo kisiwani pemba imekuja ikiwa ni siku chache Rais wa zanzibar kumteuwa ndugu Mgeni jeilan jecha kuwa mkurugenzi mkuu ofisi ya Mkurugenzi mashtaka zanzibar sambamba na kumuapisha mnamo tano mwezi huu.
Mwisho
Comments
Post a Comment