PEMBA PRESS CLUB YATOA NENO KWA WAANDISHI WA HABARI.
Na AMINA AHMED MOH’D.
WAANDISHI wa Habari Kisiwani Pemba wameaswa kufuata maadili ya uandishi wa habari kwa kufanya kazi zao wakiwa makini hasa wanapotumia mitandao ya kihamii ili kuepusha migogoro .
Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti Mstaafu wa Club ya waandishi wa habari Pemba PPC Said Moh'd Ali alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano mkuu maalumu ulioandaliwa na Club hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba Chachani Chake Chake.
Alisema iwapo waandishi watafuata maadili na kutumia taaluma yao ipasavyo kutaepusha migogoro katika jamii ambayo inaweza kuchangia uvunjifu wa amani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu hiyo Bakar Mussa Juma Amewataka waandishi wa habari ambao hawajawa wanachama kujiunga na club hiyo ili kuwasogeza karibu na wenzao.
Akisoma maazimio ya club hiyo kwa mwaka 2023 imeweka mikakati ya kuboresha shughuli za club hizo kwa maslhi ya jamii.
Mkutano huo pamoja na mambo mengine umejadili mambo mbali mbali ikiwemo maazimio ya UTPS Sambamba na kukabidhi utambulisho maalum wa kutumiwa na waandishi wa habari wapya waliothibitishwa na Club hiyo.
Mwisho
Comments
Post a Comment