Tutaendela kudhibiti utoro wa skuli za msingi
Na AMINA AHMED MOH’D - PEMBA
Uongozi wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba Umesema utaendelea kulisimamia vyema suala la utoro wa wanafunzi wa skuli za msingi kwa kuendelea kukemea ajira za watoto wilayani humo ili lisiendelee kujitokeza na kuathiri maendeleo ya elimu kwa watoto na kupelekea kukosa haki yao ya msingi kwa kukatisha masomo
Ameyasema Hayo Mkuu wa wilaya ya Micheweni Mgeni khatib Yahya Alipokuwa akizungumza na habari hizi juu ya maendeleo yaliofikiwa katika kuwarejesha skuli wanafunzi watoro wa skuli za msingi zilizomo katika skuli mbali mbali za wilaya hiyo.
Amesema moja kati ya sababu iliyopelekea kuwepo kwa utoro wa wanafunzi wa skuli za msingi ktika baadhi ya skuli wilayani humo ni pamoja na ajira za watoto pamoja kukosa mashirikiano kwa waza jambo ambalo kwa sasa limepunguwa baada ya kuliwekea mikakati maalum.
"Tatizo kubwa la utoro kwa wanafunzi wa skuli za msingi Wakati naingia hapa mwaka 2020 ilikuwa linasababishwa na watoto kutumikishwa kwa ajira mbali mbali, uchimbaji kokoto, kupara samaki jambo ambalo ilinilazimu nikaze buti kulisimamia ili lisiwepo na nashkuru kwa sasa limepunguwa na watoto waliowengi kwa sasa wamerudi skuli. "
Aidha Mkuu wa wilaya hiyo amesema kuwa kwa sasa utayari wa wazazi katika kudhibiti suala hilo umeongezeka tofauti na ilivyokuwa awali.
" Wazazi wameamka katika wilaya yanhu kuna wengine wao ndio wananipa taarifa za watoto wanapowaona wanatumikishwa na hii imekuja baada ya kuweka mkakati kuwashirikisha na kujadiliana kwa pamoja katik kudhibiti suala la utoro wameitikia wito tunafanya kazi kwa pamoja lengo letu limekuwa moja kuona kila mtoto anahaki yake ya kusoma nashukuru nimeweza kuwabadilisha mitazamo yao katika suala hili na sasa tunasaidiana kwa pamoja ".
Alindelea kusema kuwa kwa sasa maendeleo ya wanafunzi waliorejeshwa skuli ni mazuri huku wengine wakiwa tayari wameanza kufanya mitihani yao ya ya madarasa mbali mbali.
" Watoto waliorudishwa skuli maeneo mbali mbali walikuwa wanaangaliwa na kuwekwa madarasa kwa mujibu wa hali ya ufaham wa masomo yao ulivyokuwa wapo ambao walikuwa madarasa ya mitihani wengine madarasa ambayo si ya mitihani na wote wanaendelea vyema na masomo bila ya kuwa na vikwazo".
Hata hivyo mkuu wa wilaya huyo amewataka wazazi na walezi pamoja na waalimu kuendelea na mapambano hayo kwa kuhakikisha wanafunzi walifanikiwa kurejeshwa skuli hawatoroki tena na wale ambao bado wapo mitaani kuwatolea taarifa ili waweze kurudishwa skuli kupata haki zao.
"Watoto Tusiwamamie vyema wazazi tusiwatumikishe kwani wajibu wa kutatua changamoto za watoto ni sisi wazazi pia tufuatikie watoto kwa ukaribu zaidi , walimu tusimamie wajibu wetu kama serikali ilivyituamini kwa kuwasimamia na kuwalinda wanapokuwa skuli ili waweze kupata elimu itakayosaidia wao baadae.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu wilaya ya micheweni mkoa wa kaskzini Pemba bi Asya............. amesema kwa sasa suala la utoro kwa wanafunzi wa skuli za msingi wilayani humo umepungua kwa kiasi kikubwa tofauti na awali na hii imetokana na juhudi za mkuu wa wilaya hiyo kufuatilia na kutoa mashirikiano ya karibu katika kudhibiti suala hilo.
"Utoro upo lakini ulipo sasa ni ule wa wiki siku mbili mwanafunzi hajaja tofauti na ile drop out kabisa haonekani bila taarifa mwaka miezi tunamshukuru mkuu wetu wa wilaya kwa suala hili anatusaidia sana kudhibiti utoro usiendelee.
Jitihada za mkuu wa wilaya huyo katika kuwarudisha skuli wanafunzi watoro zinaendelea vyema ambapo awali kabla ya kuwa mkuu wa wilaya hiyo suala hilo lilikuwa kubwa katika wilaya hiyo ambapo zaidi ya wanafunzi elfu saba katika maeneo mbali mbali walikuwa nje ya skuli ambapo kwa sasa zaidi ya wanafunzi elfu moja wamerejea skuli huku mpango wa serikali ni kuwatafuta na kuwarudisha wanafunzi elfu tatu wa skuli za msingi kwa kipindi cha miaka mitatu ndani ya wilaya hiyo.
Comments
Post a Comment