WAZIRI TAMISEMI AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI WENGINE KUONDOLEWA WANAOSABABISHA UPOTEVU WA MAPATO.



WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa Serikali za mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mh Masoud Ali Mohammed, ameagiza kusimamishwa kazi na wengine kuondolewa, wasimamizi wakuu wa mapato na usafi katika Manispaa na Mabaraza ya miji.

Akizungumza katika kikao maalum Afisini kwake Vuga, amesema hatua hiyo ya kuondolewa na kusimashwa kazi kwa wasimamizi hao ni kutokana na serikali kotoridhishwa na hali ya usafi wa mji, na upotevu wa mapato katika mabaraza ya miji Pemba.

Agizo jengine la Serikali ni kuondolewa waendesha bodaboda katika maeneo ya michenzani na kuhamishiwa eneo la maegesho maduka mapya darajani Souk, sambamba na kuhamishiwa katika soko la welezo  wafanyabiashara ndogo ndogo maeneo michenzani na mwembetanga.

Aidha waziri Masoud ameagiza kwa kamati za ulinzi na usalama za wilaya kusimamia Opersheni maalum za kupambana na kuwadhibiti wahalifu wanaondesha vitendo vya uporaji na kuwajeruhi wananchi wasio na hatia.

Katika kikao hicho kilichowashirikisha wakuu wa mikoa, Wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa manispaa, mabaraza ya miji na wenyeviti wa waendesha boda boda na wafanyabiasha ndogondogo, waziri ameeleza kuwa hatua zilizochukiwa na serikali zimelenga kuimarisha hali ya usafi na usalama katika nchi.

Nae mkuu wa mkoa mjini magharibi, ambae anakaimu mkoa wa kusini na kaskazini Unguja, Idrisa Kitwana Mustafa, amepongeza hatua ya serikali ya kuongeza nguvu katika suala la usafi kwa kuratibiwa na Idara maalum za SMZ.
Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI