WADAU MBALI MBALI WAJADILI RASIMU YA KANUNI ZA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR ZSSF JUU YA FAO LA FIDIA YA KUUMIA KAZINIILI KUFANYIWA MABORESHO (SKIMU)
NA- AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.
OFISA Mdhamini Ofisi ya Rais kazi, Uchumi Na Uwekezaji Pemba Dk Fadhila Hassan Abdalla amefungua Mkutano maalum wakujadili rasimu ya Kanuni za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Zssf juu ya Fao la Fidia ya Kuumia kazini (SKIMU) Ambao umeshirikisha wadau kutoka Taasisi Mbali mbali.
Katika Ufunguzi huo Mdhamini Huyo Amewataka Wadau hao kujadilia na kutoa Mapendekezo yao ambayo yatasaidia kuboresha na kuongeza ufanisi na uboreshwaji wa huduma bora kwa Wafanyakazi wanapopata dharura hizo za kuumia kazini.
Alisema kuwa Lengo la Serikali la kuwajali watumishi wa umma litazidi kufikiwa iwapo wadau hao wataweza kujadili kwa pamoja na kutoa Mapendekezo ambayo yataboresha huduma hiz za dharura ambazo zimekuwa kilio kikubwa kwa wafanyakazi na watumishi ambao wamekuwa wakikosa haki hiyo ya kulipwa Fidia.
Awali Akizungumza na wadau hao Kaimu Mkurugenzi wa Zssf Pemba Said Maalim Said Amesema kuwa Mfuko huo utaweza kusimamia majukumu yake ya kuondoa usumbufu unaowapata wafanyakazi kwa kusimamia upatikanaji wa Fidia hiyo kwa Muda na wakati Stahiki iwapo wadau hao Wataweza kutoa Maoni ya pamoja katika kanuni hiyo.
Wakitoa maoni Yao juu ya kanuni hiyo baadhi ya wadau hao Akiwemo, Juma Ali Makame kutoka Wizara ya Afya kitengo cha Usalama kazini, Saida Abdalla Bakari kutoka Shirika la Bima Zanzibar, Sifuni Ali Juma kutoka mwamvuli wa Asasi za kiraia Pemba Pacso, Wameomba mfuko huo kurekebisha mapungufu katika baadhi ya kanuni hizo ikiwa ni pamoja Kuweka mbinu mbdala za kulinda na kuzuia Ajali, kutolewa fidia ndani ya kipindi cha ugonjwa, Kuiweka sambamba na kuweka mchanganuo ambao utaonesha kima cha mwanzo na ukomo wa fidia hizo Sambamba na kuiweka Kanuni hiyo kuwanufaisha Wafanyakazi wa Taasisi binafsi.
Mkutano huo Uliofanyika Katika ukumbi wa ZSSF Tibirinzi Chake chake Pemba Umekusanya wadau kutoka wizara ya Afya, Jeshi la Polisi, Wadau kutoka Wizara ya Kazi uwezeshaji, Wadau wa sheria kutoka Wizara katiba na Sheria, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Ofisi ya Wakfu na mali ya amana, shirikisho la Vyama vya Wafaya kazi pamoja na wakala wa matukio ya huduma Za kijamii Zanzibar ambapo jumla ya kanuni yenye vipengele nane juu ya rasimu hiyo ya ya Mafao ya Kuumia kazini ( SKIMU).
Mwisho.
Comments
Post a Comment