RASIMU YA KANUNI YA HIFADHI YA JAMII ZSSF SEKTA ISIYO RASMI WADAU WATOA MAONI YAO
Na Amina Ahmed Moh’d, Pemba
KAIMU Mkurugenzi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Pemba Said Maalim Said Amefungua Mkutano wa Siku moja ambao umejadili Rasimu ya kanuni ya Hifadhi ya Jamii kwa Sekta isiyo juu ya Kuchangia katika Mfuko wa hiari ambao umewashirikisha wadau mbali mbali kutoka Sekta isiyo rasmi kiswani humo.
SAID MAALIM SAID - K/ MKURUGENZI ZSSF PEMBA
Akizungumza katika Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa ZSSF Tibirinzi Chake Chake Kaimu huyo amesema kuwa ZSSF itaendelea kupokea na kuyafanyia kazi mapendekezo ya wadau hao kwa lengo la kuimarisha Kanuni hiyo ambayo itakapokamlika itakuwa na manufaa zaidi kwa wadau wa sekta hiyo isiyo rasmi.
Amesema Serikali inatambua Mchango mkubwa unaotolewa na sekta hiyo jambo ambalo limepelekea Kuanzisha kwa Mfuko wa uchangiaji wa hiari ili kuweza kuwasaidia kufaidika na hifadhi inayotolewa.
"ZSSF imetayarisha hii kanuni ili kuona vipi itasaida kuboresha na kuwapa fursa wenzetu ambao hawapo katika mfumo rasmi waweze kufaidika katika sekta hii, hivyo kutoa kwenu, Michango itakayosaidia kuboresha kutasaidia kuwawezesha Kuchangia katika mfuko wa hiari ambao utawasaidia kunufaika na kupata faida mbali mbali kma wadau wa sekta Binafsi".
Amesema Lengo la Serikali ni kuwezesha watumishi wa Sekta isyo rasmi kuingia na kujiunga katika Mfuko wa kuchangia kwa hiari Wa ZSSF na kuweza kufaidika katika mambo mbali mbali.
"Serikali inatambua Mchango wa Wadau binafsi katika Maendeleo ya Taifa, Mh Rais anasema kila siku Jinsi gani tutaweza Kuwainua wenzetu wa sekta Zisizo rasmi ambao zaidi ya Asilimia 60 waajiriwa wake ni wengi jambo ambalo limepelekea kuwaangalia kwa jicho la karibu zaidi kwa vile wanafanya kazi kubwa kwa Serikali".
Kwa upande wake Mtendaji wa Mfuko wa Hiari ZSSF Rajab Haji Machano amesema kuwa lengo la Kukusanya Maboresho kutoka kwa Wadau hao ni kutekeleza Ahadi ya Serikali juu ya kutoa Hifadhi ya jamii kwa watu wote na kuweza kufaidika na mfuko Huo.
"Kama ambavyo wenzetu ambao ni wafanyakazi waliomo katika sekta Rasmi ambao wanatambulika na Mfuko huu na kufaidika nao katika mambo mbali mbali ikiwemo kupata Pencheni ya ustaafu, Mikopo ya Elimu na faida nyengine mbali mbali ndivyo ambavyo tunataka sekta isiyo rasmi nayo iweze kufaidika kutokana na kazi kubwa wanayoifanya.
Akipokea Maoni ya maboresho kutoka kwa wadau hao mara baada ya kuwasilisha rasimu hiyo yenye Sehemu 12 Mwanasheria kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF Daud Juma Sleiman Amesema kuwa ZSSF itayafanyia kazi Mapendekezo ya maboresho hayo yaliotolewa ili kuweza kuongeza tija kwa watumishi wa sekta isiyo rasmi.
Wakitoa maoni Yao juu ya kanuni hiyo baadhi ya wadau hao Akiwemo, Fatma Maruzuku Khamis, Asila Omar Sleiman Pamoja na Ulfat Sultan Yussuf wameuomba Ungozina Usimamizi wa mfuko huo wa hiari kuendelea kutoa Elimu kwa vijana Katika Maeneo mbali mbali ili kuweza kufikia malengo yaliokusudiwa katika kuwasaidia wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi.
"Vijana wengi mitaani wamejiajiri wenyewe kwa kufanya shuguli mbali mbali kuna wanaoendesha boda boda wanaouza biashara ndogo ndogo na wengine wengi, Ili kuona na wao wanakuwa wanufaika wa kuchangia mfuko huu wa hiari naiomba ZSSF Iwafikie kuwapa Elimu hii waliwengi huko mitaani hawajui kama kuna fursa hii yenye faida kwao, na wao kuweza kujua lakini pia kuweza kutoa maoni yao wasikose fursa hii "
Kanuni ya Rasimu hiyo ya Hifadhi ya jamii kwa Sekta isiyo rasmi imejadiliwa na kutolewa Mapendekezo ya Maboresho na Wadau mbali mbali kutoka Sekta isiyo Rasmi ikiwa ni pamoja na Wanasheria wakujitegemea, Wajasiriamali, pamoja na wafanyakazi kutoka Sekta mbali mbali zisizo rasmi kisiwani Pemba .
Mwisho
Comments
Post a Comment