ZINA MOLA, USHIRIKA ULIO LETA UKOMBOZI WA MAENDELEO KWA WANAWAKE KIJIJI CHA ZIWANI, FEDHA ZA HAKIBA NA UZALISHAJI WA BIDHAA, BORA KWA MUDA MFUPI TANGIA KUANZISHWA KWAKE.

Na, AMINA AHMED MOH’D - PEMBA      0719859184 

WAJASIRIAMALI WA  USHIRIKA wa Kikundi Cha Zina Mola  kikichopo Pembeni ya Muangaza Ziwani wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba  kinachojishughulisha na Usarifu wa Vibdhaa za Udongo  wamesema Kumekuwa na Mafanikio makubwa katika kujikomboa na Umasikini  Tangia kuanzishwa kwa Ushirika huo Mwaka 2020. 


 Wakizungumza Huko katika Eneo lao maalum la kusarifu  Udongo kwaajili ya kutengeneza bidhaa mbali mbali Baadhi ya Wanaushirika huo  Akiwemo Hamida  Juma Amour wamesema kuwa Wanawake wengi wa  kijiji cha Pembeni ya Mwangaza, kwa Asilimia kubwa wakubwa na wadogo kwa sasa wanajishughulisha na kazi hiyo ya ufinyazi, jambo  Ambalo limezaish  ajira kwao na watu wengine na kujipatia kipato.

"Wanawake wa kijiji hichi hutumia muda wao mwingi kwa ajili ya kufanya kazi hiyo, ambayo huwapatia kipato cha kuendeleza maisha yao ya kila siku binafsi nimekuwa mnufaika wa Ushirika huu Alisema Bi Hamida nimeondokana na Utegemezi. 

Kuwapatia watoto mahitaji yao muhimu ya kielimu na matibabu, kutokana na ubunifu huo bila ya kumtegemea baba ‘mume’ ambae nae ana majukumu menginekwangu ni jambo la kawaida kwa sasa  tangu nimejifunza  usarifu wa udongo kusarifu  vyombo mbali mbali Alisema Mwajuma Khamis Hamad .


Tunanufaika sana na hichi kikundi, licha ya changamoto tunazozipata, lakini tunazichukuwa kama ni fursa kwetu ya kusonga mbele kimaendeleo, kwani inatusaidia kupunguza nguvu ya ukali wa maisha,” anasema Hadia  Muhudini Haji Mwanaushirika kikundi cha Zina mola. 

"Kazi hii ndio inayowaendesha maisha yetu ya kila siku kwa kujipatia mahitaji yetu ya lazima kama vile chakula, kulipia ada na matibabu pamoja na kuweka hakiba zao benki.

" Tunaiona faida ya ufinyanzi, na ndio maana Tunaendelea na kazi hii inatupatia kipato, mbali ya matumizi tuliyonayo lakini Tunahakiba ya zaidi ya shilingi milioni 2.5 benki. Alisema Furaha Heri Juma  Mlezi na Mtunza Fedha wa Ushirika Huo. 

Serikali haiwezi kutajiri Sote kwa kuwa wafanya kazi Serikalini  Ikiwa hii ziwani tu ina wakaazi zaidi ya 800 Tunazitumia Fursa tunapozipata kujikomboa Aliendelea. 

Katika Hatua Nyengine wanaushirika hao wameiomba Serikali kuendelea kuwasaidia kutatua changamoto zao  zinawakabili  katika Ushirika huo  ambazo zimekuwa zikiwarudisha nyuma Kimaendeleo. 

 Mtumwa Amour Juma Alisema kuwa licha ya mafanikio hayo wanayoendelea kuyapata lakini changamoto ya  Ofisi, Usafiri  pamoja na Mashine  imekuwa ikirudisha nyuma harakati  zao. 

"Tunakabiliwa na Changamoto ya usafiri, ambao ni Muhimu katika utafutaji wa Malighafi za kuchomea vyombo vyetu tunavyosarifu  (Magubi-kozi) ambayo mara nyingi yanapatikana katika wilaya ya Mkoani, sisi hulazimika kukodi magari binafsi, hatuna  ofisi wala  Mashine ambavyo ni muhimu katika kufikisha zaidi malengo tuliyoiwekea ya kujikomboa na Umsikini Tunaiomb Serikali itusaidie". 


"Zaidi Mgongo tunaumia kuponda udongo kwa mikono tunatumia kifua kulainisha Serikaki ituangalie kuona mdala wa Matatizo haya kwa wajasiriamali wote Nchini ni kusaidiwa mashine. 

Akizungumzia Suala hili Afisa miradi kutoka chama cha waandishi wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar ofisi ya Pemba Asha Mussa Omar, anasema kuwa kikundi hicho kimefikiwa zaidi ya mara mbili kutatua changamoto Ambazo zilikuwa ndani ya uwezo wao.

Kama ikitokezea wamepata mradi, Tutawaingiza kwenye mchakato, ili nao wafikie ndoto zao kama walivyo wanawake wengine wajasriamali.

‘’Kwa sasa hatuna mradi kwa ajili ya kuwanunulia mashine ya kuchakata udongo, lakini kama wanahitajia uwezeshwaji mwengine wafike ofisini uwezo wetuulikuwa ni kuwezesha kielimu na mitaji mbinu na upatikanaji wa Soko, na kikundi hicho Tulikifikia kama vikundi vyengine ’’anasema.

Kwa Mujibu wa  hotuba ya bajeti ya mwaka 2022/2023 ndani ya baraza la wawakilishi  iliyowasilishwa na Waziri wa Afisi ya Rais Kazi uchumi na uwekezaji Mudrik Ramadhan Soraga alisema, kuwa mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa kushirikiana na taasisi za kifedha, umejipangia kutoa mikopo 2,000 kwa wajasirimali .

Alisema , mikopo hiyo ina thamani ya shilingi bilioni 3 kwa vikundi vya kiuchumi katika sekta zote za kiuchumi, kuangalia fursa mpya ambazo zinaweza kutekelezwa na wananchi.

Aidha katika bajeti hiyo waziri Soraga aliahidi, kuendelea na juhudi za kutunisha fedha ili mfuko uendelee kuwasaidia wajasiriamali wengi zaidi.

‘’Pia kuimarisha mashirikiano na uratibu wa shughuli za mikopo nafuu hapa nchini pamoja na kuimarisha mashirikiano na taasisi zinazotoa mikopo nafuu,’’ alisema.

Jumla ya vyama vya ushirika 1,848 vimesajiliwa na kati ya hivyo Unguja 709 na Pemba 1,139 pamoja na vyama vya uzalishaji na utoaji wa huduma 910, vinavyojishughulisha na utengenezaji sabuni, SACCOS, ukataji miwa, uvuvi, ufugaji kaa, kilimo pamoja na usafi wa mazingira.

Ushirika huo wenye Wanachama Tisa wanawake Nane na mwanaume Mmoja kimekuwa kikitengeneza bidhaa mbali mbali ikiwemo Mikungu, vyetezo,  Mitungi, Vijungu, Majiko,pamoja na Sahani ambazo hutumika kwajili ya matumizi ya Nyumbani. 


                                    MWISHO.

 

  

 

 

 

 



Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

ZSTC YAWAONYA WAUZAJI NA WANUNUAJI KARAFUU KINYUME NA UTARATIBU ULIOWEKWA .

WIZARA YA AFYA YAWAPA UJUMBE HUU VIONGOZI WA DINI KUUFIKISHA KATIKA JAMII