JESHI LA POLISI LAWASHIKILIA WATATU KWATUHUMA ZA WIZI WA SARUJI ZA MIRADI YA SERIKALI USIKU WA MANANE
NA OMAR HASSAN – Unguja
Watu watatu wanashikiliwa katika kituo cha Polisi Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja kwa tuhuma za wizi wa saruji paketi 27 iliyokuwa ikitumika katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwera Pongwe Wilaya ya Kati.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari huko Makao Makuu Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna msaidizi wa Polisi ACP GAUDIANUS FELISIAN KAMUGISHA amesema kuwa Juni 18,2023 majira ya saa 07:30 Usiku Askari Polisi wa kituo cha Polisi Tunguu wakiwa katika doria walifanikiwa kuwakamata watu watatu wakiwa na gari Z.350 HH ikiwa imepakia mifuko hiyo ya saruji ambayo inatiliwa mashaka huwa ni ya wizi.
Aliwataja watu hao kuwa ni Saleh Ali Bakar (25) ambae ni dereva wa gari hiyo ,Seif Khamis Mati (20) na Toteni Soa Ngamamulomo 30 pia ni mfanyakazi wa kampuni ya IRIS wote ni wakaazi wa Jumbi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja ambapo saruji walioiba ni Mali ya kampuni ya ujenzi wa barabara IRIS.
Kamanda KAMUGISHA amekemea na ametoa onyo kwa wananchi wanaofanya vitendo vya hujuma dhidi ya Miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.
Comments
Post a Comment