WANANCHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WASIFIA UWAJIBIKAJI WA DIWANI JIMBO LA CHAMBANI
NA - AMINA AHMED MOH’D, PEMBA 0719859184
MWAKILISHI wa Jimbo la Chambani Bahati Khamis Kombo Amewataka Wanawake Kuongeza Mshikamano na kuwa kitu kimoja ili kuweza kuitetea Zanzibar na Kuongeza Ufanisi katika Maendeleo ya Wanawake Na Watoto.
Akizungumza na Habari hizi katika Ukumbi Wa baraza la Mji Chake Mwakilishi huyo Alisema Maendeleo ya Wanawake Visiwani yanaweza kufikwa Endapo wataendelea kuzidisha mshikamano na kuungana mkono katika kutafuta Fursa mbali mbali ambazo zinaweza kuwa Chachu ya kusaidia wengine.
Alisema Wapo ambao wamekubali kujitoa kwajili ya maendeleo ya Wanawake Wenzao kwa Kutafuta fursa za Uongozi Lakini kutokana na Kuosa Mshikamano kwa Wanaume ambao huendelea kuwalisha dhana potofu baadhi ya Watu Hupelekea Kukosa nafasi hizo na kuendelea kubakia kwa wanaume na kushindwa kuzitumia katika Kupata ufumbuzi wa Masuala yanayiwakabili.
"Kuna Dhana hii ambayo Wanawake wenyewe tumekuwa tukiiamini Kwamba hatupendani Jambo Ambalo Naamini ni njama tu kutumika hii dhana Lakini haina ukweli hivyo Wanawake Wenzangu niwaase Mashirikiano katika Kuona Tunakuwa Wengi Katika Uongozi nyanja mbali mbali ili tujiletee Maendeleo.
Aidha Amewataka Wananchi Wa Jimbo la Chambani Kuendelea Kutoa Mashirikiano katika Kuzipatia Ufumbuzi Changamoto mbali mbali.
"Changamoto Nyingi Wananchi ndio ambao wanazijua Mashirikiano ambayo wananendelea kunipa kaika kuzioatia Ufumbuzi kama ambavto niliwaahidi, Niwatake Wasichoke bali wazidiahe Kuziibua na Kunifikishia Ili kuona tunazipatia Suluhu.
Wakizungumza na Habari hizi Baadhi ya Wananchama wa chama cha Mapinduzi CCM Akiwemo Halima Juma Diwani Wamesema Utendaji wa Mwakilishi huyo katika kusaidia Maendeleo na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa Jimbo la Chambani ni wakupigia Mfano na kuigwa na Viongozi wengine.
"Tunapopokea au kuona taarifa za utekelezaji wa Ahadi Kwa Viongozi wetu katika Majimbo tunakuwa Tunafarijika kwa sababu hiyo ndio nia Thabiti Ya Chama katika Kuona Wananchi waapata Maendeleo, na Miongoni mwa Wawakilishi ambao Wanaiendea haki nafasi yao kwa kusaidia wananchi ni Mh Bahati.
Miongoni mwa Changamoto zilizopatiwa ufumbuzi na Mwakilishi hiyo jimboni kwake ni Pamoja na Maendeleo ya Elimu , Afya, Pamoja na Huduma ya Maji.
Mwisho.
Comments
Post a Comment