WANAWAKE PEMBA WAASWA KUJIKOMBOA KICHUMI KUPITIA BIASHARA YA UREMBO SALUNI.
NA AMINA AHMED MOH’D PEMBA, 0719859184
WANAWAKE Kisiwani Pemba Wameaswa kuzichangamkia Fursa zinazopatikana kupitia Biashara ya Urembo, ili kuweza kujipatia Kipato na kupata fursa za kuwajiri wengine kusaidia Serikali kuondokana na mzigo wa Utegemezi .
Ametoa Ushauri huo Leah Uswage Stephano alipokuwa akizungumza na Habari hizi juu ya Fursa za kujiajiri kupitia kazi ya urembo huko Katika Ofisi yake ya Ususi, na urembo wa akina mama Iliyopo Mtaa Wawi Gereji Wilaya Chake Chake Pemba.
LEAH USWAGE - MJASIRIAMALI BIASHARA YA UREMBO.
Amesema Bado wanawake wengi kisiwani Pemba wamekuwa Wakiipuza fursa inayopatikana kupitia Kazi za Urembo katika Saluni licha ya kuwa na Faida Ambazo zinaweza kuwakomboa kichumi na kuzalisha fursa nyengine za kuondokana na utegemezi.
Wanawake wezangu Moja kati ya Fursa ambayo imekuwa inaweza kutuingizia kipato ni biashara ya urembo kwa akina mama, kutokana na kuwa suala hilo ni la kila siku kwa rika zote Tuichangamkie, Tusiibeze,
" Ususi wa Nywele, Mitindo mbali mbali, kubandika Wigi Kuweka dawa kufanya usafi wa kucha Urembo wa Uso, kushonea Mawigi, Kusuka Mabutu, kuweka Dawa za nywele ,Kuchora na Nyenginezo ni Moja kati ya Biashara ambayo licha ya kuwa na uhitaji mkubwa kwa wakinamama Kisiwani Pemba Lakini bado fursa hiyo hawajaitumia Kuanzisha Saluni na kujipatia Kipato.
Sisi ambao sio wazawa hapa kisiwani Pemba ndio Ambao Tumekuwa Tukilazimika Kuziona hizi fursa, Na tunazitumia ipasavyo, tumeajiri na wengine kutoka nje ya Kisiwa hichi Na wao wanaendesha Familia zao kupitia kazi hizi biashara za urembo lakini wazawa bado hawajaona hii fursa.
Akizungumza kwa upande wake Tina James Mfanya kazi katika Saluni hiyo ya akina mam Amesema kuwa Kazi hiyo imekuwa msaada mkubwa katika kuendesha maisha yake.
"Nakidhi mahitai yangu na wadigo zangu, Natuma Pesa nyumbani Nawasaidia mahitaji mbali mbali Sikubweteka wala sikuogopa kuifata Pemba fursa hii ya Kazi yangu ya Urembo.
Wakizungumza na habari Hizi Baadhi ya wanachi kisiwani Pemba Akiwemo Omar Khamis Mgando, Pamoja na Ismail khatibu Wamesema kuwa Dhana potofu juu ya Biashara ya urembo katika masaluni ndio inayopelekea Wanawake wengi kukosa kuitumia fursa hiyo.
Nao Baadhi ya wanawake waliozungumza na habari hizi khadija Seifu Ridhwan Amesema kuwa mara nyingi amekuwa Anatumia Saluni Kufanya urembo katika nywele zake, na kupata matokeo mazuri.
Kupitia Biashara ya Saluni mfanya biashara huyo Amefanikiwa Kumiliki Mafridge 2 ambayo yanahifdhia samaki katika Duka lake Vitoweo Vya baharini Samaki, kusomesha watoto wake sambamaba na kuendelea kuendesha familia yake kila siku katika mahitaji mbali mbali.
Mwishi
Comments
Post a Comment