WATENDAJI WIZARA YA KILIMO PEMBA WAASWA
Na ALI MASSOUD KOMBO.
AFISA Mdhamin wizara ya Kilimo Pemba, Inginia IDRIS HASSAN ABDULLAH, amewataka watendaji wa wizara yake kuwajibika vyema katika nafasi zao pamoja na kusimamaia nidhamu za wanaowaongoza,ili kufikia malengo ya taasisi.
Afisa mdhamin Inginia Idris ameyasema hayo wakati wa kikao cha kawaida pamoja na wakuu wa maidara na vitengo mbali mbali vya wizara ya kilimo kilichofanyika katika Afisi za wizara hiyo Weni, Wete Pemba.
Aidha IDRIS, amekemea ukataji wa miti ovyo usiozingatia uhifadhi wa mazingira na kuwahimiza watendaji wake kusimamia sheria zilizopo katika kuilinda rasilimali za misitu nchini, sambamba na kupiga vita uvunwaji wa mazao machanga.
Kwa upande wao, watendaji wa wizara hiyo walioshiriki katika kikao hicho walikubali kuwepo kwa mapungu yanayoikabili sekta ya kilimo na hivyo kuahidi kuyafanyia kazi ili kuona Sekta hio inapiga hatua mbele.
Comments
Post a Comment