ELIMU JUU YA ATHARI ZA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA YAFIKA KWA WANAFUNZI SKULI YA SEKONDARI UWELENI
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA
ZAIDI ya Wanafunzi 200 wa Skuli ya Sekondari Uweleni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba wamefikiwa na kupewa Elimu Juu ya Sheria, Na Athari mbaya za Matumizi na Uuzaji wa Dawa za kulevya kutoka kwa Maafisa kutoka Mamlakaya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kisiwani humo Ikiwa ni muendelezo wa Shamra shamra za Kuelekea siku ya Kupiga vita Biashara ya Uuzaji na utumiaji wa Dawa za Kulevya inayoadhimishwa kila ifikapo June 26 Duniani kote.
Akitoa Elimu ya Kisheria kwa Wanafunzi hao Kamanda Wa Wilaya Kutoka Mamlaka hiyo Ahmed Khamis Kombo Amewataka wanafunzi hao kutoa Taarifa kwa Uongozi wa Skuli kwa wazazi, endapo watabaini kuwepo kwa viashiria vya uuzwaji, Uwepo, pamoja utumiwaji wa Madawa hayo katika maeneo yao yaliyoawazungukua ikiwemo maeneo ya Skuli .
Kamanda Ahmed Khamis alisema kuwaambia Wanafunzi hao wakike na Wakiume kuwa " Sheria ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya Zanzibar, ambayo ni sheria namba 8 ya mwaka 2020, 2021,Katika kifungu cha 26 kinaekeza ivi"( Endapo Ndani ya Skuli, ama Taasisi nyengine yeyote au Mazigira ambayo yaeizunguka Taasisi hiyo, ikipatikana Dawa za kulevya, na Endapo watumiaji wa Taasisi hiyo ni watu ambao watakuwa chini ya Umri wa Miaka 18 Adhabu yake itakuwa ni kifungo kisichopungua miaka 30, kwa Wasimamizi au wamiliki wa hizo Taasisi ) "Jee Wanafunzi mtapenda kuona Mwalimu wenu Mkuu anafungwa kwa kuona viashiria bila kutoa Taarifa kwenu kama jibu hapana bhasi niwaase mutoe Taarifa ili Uongozi wa Skuli uweze kutoa Taarifa kwa Mamlaka husika.
Akitoa Mada juu ya Athari ya matumizi na Biashara ya Daawa za kulevya Ali Yussuf Ali ambae ni Afisa Kutoka Mamlaka hiyo Kisiwani humo Pamoja na Mambo mengine Aliwataka wanafunzi hao kuendelea kuchukua Tahadhari juu ya kadhia mbali mbali za kiafya ambazo zinatokana Matumizi ya Dawa za kulevya.
" Dawa ya kulevya ya aina yeyote inakuwa na kemikali ambayo ikiingia katika Mwili wa binaadamu inakwenda kuathiri Mwili wa kiumbe hai na kuharibu mambo yoote ikiwemo fikra mawazo kumbukumbu na mawazo, hata kwa ile ladha tu ni sawa na mtu ambae amewahi kuonja ladha ya embe mbichi au limau hawezi kuisahau tuiwache ili tujiepushe na kupata Athari hizo mbaya".
" Katika mazingira yetu kadhia hizi zipo zimetuzunguka, wapo ambao wanaotumia Madawa haya kutokana na sababu mbali mbali Vijana wazee hata Watoto Wakike n, Muelekeo Umebadilika hawako salama juu ya kadhia hii Madhara yae ni makubwa tuepuke vishawishi ambavyo vitatupelekea Kujiungiza huko. "
Nao Baadhi ya wanafunzi hao waliopatiwa Elimu hiyo Akiwemo Amina Abdalla Shamte, Ramla Halfan Juma, Fathiya Mzee Muhammed, Hasina Muhammed Abdalla pamoja na Adil Muhammed Ali licha ya kupatiwa Elimu hiyi wameiomba Mamlaka hiyo kuwapatia Ufafanuzi kwa baadhi ya maswali yao ambayoyalikuwa yakiendelea kuwaumiza kichwa kwa kukosa uelewa Wa Elimu ya Madawa ya kulevya,ikiwemo namna gani mamlka hiyo inadhibiti uungiaji wa madawa ya kulevya.
Akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa Skuli ya Sekondari Uweleni Mwalimu Msaidizi wa Skuli hiyo Kamis Muhammed Ussi amesema Elimu hiyo juu ya Athari za Madawa ya kulevya iliyotolewa kwa wanafunzi hao itasaidia katika kujikinga na kujiepusha na Ushawishi wa kujiingiza katika kundi hilo.
"Hii ni Mada kabisa ya somo la civics Kwa vile imetolewa kwa uwazi na upana kwa wanafunzi leo kutasaidia kuimarisha na kukuza uelewa wao Juu ya kujikinga na Masuala haya ya Madawa, Tumefarijika na tuiombe mamlakaiendekee kutumbuka kwa elimu hii kila baada ya muda.
Shamra shamra hizo pia zinaendelea kupita katika Maeneo ya Shehia mbali mbali kutoa elimu Ambapo awali, Shehia Ya Bopwe wilaya ya Wete , Skuli ya kengeja, pamoja na Kutembelea kutoa elimu zaidi kwa Familia ambazo zinawatu wenye uraibu zimefikiwa kuoewa elimu Juu ya Athari za Matumizi uuzaji wa Dawa za kulevya kwa kufanya mikutano ya wazi.
Mwisho
Comments
Post a Comment