WANANCHI WAPONGEZA JUHUDI ZINAZOENDELEA KUFANYWA NA SHEHA WAO NI BAADA YA KUPATIWA UFUMBUZI JUU MASUALA YANAYOWAUMIZA VICHWA KILA SIKU KATIKA MAENEO MBALI MBALI YA VIJIJI NA MITAA YAO.
NA AMINA AHMED MOH’D PEMBA
WANANCHI Wa Shehia Ya Wawi wilaya ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba Wamempongeza Sheha wa Shehia hiyo kwa Juhudi mbali mbali anazoendelea kuzifanya kwa wakazi wake ikiwa ni pamoja na Kusaidia kupata Elimu Juu ya Masuala ya Kisheria jambo ambalo awali lilikosekekana na kupelekea Kuongezeka kwa changamoto mbali mbali za kijamii Ikiwemo migogoro .
Wakizungumza na Habari hizi Baadhi ya Wananchi hao Akiwemo Juma Muhammed Tamimu, Fatma Muhammed Abdallah, Raya Khamis Omar pamoja na Khamis Muhammed Khamis wamesema kuwa Jitihada hizo Zimekuwa Chachu ya Wananchi mbali mbali katika Shehia hiyo kuanza kuzitambua Sheria mbali mbali na kuzitumia katika kutatua changamoto zinapojitokeza kwa Uweledi.
"Kikubwa sisi wanajamii tuendelee kushirikiana vya kutosha na sheha wetu tu, Amekuwa mstari wa mbele kuona nakuhakikisha ile migogoro isiyokwisha kutokana na sababu za kutokujua sheria bhasi Haiendelei ni jambo la kiungwana ambalo ametusaidia na hatutolisahau, "
Tulikuwa tu nalalamika kuona baadhi ya wahalifu ambao tunawapeleka polisi usiku asubuhi wameachiwa Migigoro inaanza, lakini hatukuwa tunajua kama kumbe kisheria kuna haki ya dhaman, a hata kama mtu anaweza akawa muhalifu Tusingeyajua hayo kama wanajamii wa kawaida, na kama sio Sheha wetu kufanya kazi kubwa ya kutafuta wanansheria maalum, kuja kutusomesha sheria Mbali mbali,ikiwemo sheria ya Jinai na Sheria ya Madai na kupewa elimu sisi wananchi wake". Alisema Juma Tamimu Mkaazi wa Wawi Mtaa wa Msikiti kibegi.
"Tunampongeza sana sana Mh Sheha wetu Watu wengine wanaona kama hili suala ni dogo lakini kuumiza kichwa na kutaka kujua kipi kinasababisha Changamoto kwa wananchi na kutafuta ( 40 ) wa tatizo linalorudisha nyuma Maendeleo ni jambo la kuigwa na viongozi wengine Kabisa.
"Tumeweza kujua mgawanyiko wa sheria mbali mbali zinazotuhusu, Tulikuwa tunakwenda tu kienyeji enyeji hatufahamu vipi Tufuatilie kesi Zetu lakini Kuoutia yey me tumeweza kujua haki zetu ambazo zinatulazimu kisheria kuzidai kuzitetea na kuzitafuta Tumefarijika sana" Fatma Muhammed Mkaazi wa Shehia ya Wawi.
Khamis Muhammed Khamis Alieleza kuwa "Binafsi Mpka umri huu niliofikia sikuwa na uelewa kabisa juu ya Masuala ya Ardhi nilikuwa naishi kibubusa tu kumbe kuna Sheria ya Ardhi kuna mahali pakupeleka kesi za Ardhi Alichokifanya sheha kwa wananchi ni hazina ya kuishi kwa kutafuta maendeleo ya kwetu wananchi tu sio kitu chengine cha kuleta simtofahamu kikaturudisha nyuma.
"Tulikuwa tunaona vitu sawa sawa tu hatukuwa tunajua kama kuna sheria ya Jinai na Sheria ya madai tulikuwa tunaona tumeshafanyia masuala mbali mbali ikiwemo Udhalilishaji tunaona ni kesi moja tu leo hii watu wa shehia yetu Takiban waliowengi wamekuwa na uelewa wa kutifautisha Izo Sheria pia"Raya Khamis Omar.
Akizungumza na na Mwandishi wa habari hizi sheha wa wa Shehia Hiyo Sharifa Waziri Abdalla amesema kuwa kutokana na vikwazo vingi ambavyo vilikuwa vinaendelea kumkosesha usingizi akiwa kama kiongozi mkuu wa kuisaidia Serikali Kufikia Maendeleo mbali mbali kwa Wananchi wake katika Shehia ya Wawi, alibaini kuwa kukosa Usaidizi wa kutambua na kuzitofautisha Sheria ni moja kati ya Changamoto kubwa ambayo ilikuwa inawakabili wananchi wake.
"Nilipolibaini hilo nikaamua kwa moyo wangu Kujitolea kuisaidia jamii kupata usaidizi wa kisheria, ndipo nilipoamua kumtafuta Msaidizi wa Sheria aweze kunisaidia kutimiza hili, Nikaamua kuranda nae mtaa kwa mtaa kutoa Elimu Kwa Makundi Mbali mbali na kuwaelimisha juu ya Sheria mbali mbali na Msaada wa Kisheria na waliowengi walinufaika na Elimu hiyo. "
" Aidha Niliomba Usaidizi maalumu kutoka Jumuia ya Wasaidizi wa Sheria Chake Chake kuandaa Mafunzo ya Siku 5 Kwa Gharama Zangu Mwenyewe Ambayo yatawasaidia wasaidizi wangu kuzidisha Uweledi katika kusaidia Wananchi kupata ufumbuzi wa kisheria ."
Aidha Bi Sharifa alisema kuwa kwa sasa Wananchi waliowengi wamekuwa wakitoa Mashirikiano mazuri kwa Msaidizi wa Sheria aliepo ndani ya Shehia hiyo katika kupata ufumbuzi wa Masuala mbali mbali.
""Tumewapatia msaada wa kisheria kwa kuwapatia Elimu juu ya sheria mbali mbali ambazo moja kwa moja zimegusa Maisha ya wanajamii, Tumewafundisha sheria ya Ardhi, Sheria ya mtoto, haki na wajibu na Sheria mbali mbali za Madai na Jinai engo ni kuona jamii hi ya wawi ambayo wakaazi wake kwa asilimia kubwa ni wagen wa kuingia na kutoka wanaepukana na mizozo. Alisema Haji Nassor Muhammed Msaidzi wa Sheria Wawi.
Akizungumzia Suala Mkurugenzi wa Jumuia ya Wasaidizi wa Sheria Wilaya ya Chake Chake ambae Pia ni Kaimu mwenyekiti Bodi ya wadhamini Jumuia hiyo Kassim Ali Juma Amesema kuwa" Sheha wa Shehia ya Wawi ni Shehia Pekee kati ya Shehia 32 zilizopo chake chake kufika katika Jumuia hiyo kuomba kupatiwa Usaidizi na msaada kwa wananchi wake
Hakuna Uongozi wa Shehia hata moja Ukiacha Sheha wa Shehia ya Wawi Kuja kuomba Wataalam wa Sheria kuenda kupatiwa Elimu ya Msaada wa kisheria kwa Wananchi wake yeye ni wa kwaza.
Aidha Kassim amewaomba Masheha wa shehia nyengine kuiga Mfano huo katika kuona jamii Ya Chake chake inaondokana na Mizozo mbali mbali ya inayohitaji Msaada wa kisheria.
Shehia ya wawi yenye wakaazi zaidi ya 5000 Awali ilikuwa ikikabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo mizozo ya Ardhi, wizi wa mazao na vitendo vya Udhalilishaj, Mmongonyoko wa Maadili Ambayo hutokana na wananchi waliowengi kushindwa kupata msaada wa kisheria na kutojua sheria mbali mbali kutokana na Mwingiliano wa mara kwa mara wa wageni kutoka nje ya shehia hiyo kwajili ya kufanya shuguli Mbali mbali.
Mwisho
Comments
Post a Comment