MBUNGE AAHIDI KUZIOATIA UFUMBUZI CHANGAMOTO HIZI ZINAZOWAKABILI WANANCHI NDANI YA MUDA MFUPI

Na  - Abdalla Amour  Mbarouk, Pemba.

Mbunge wa bBnge la Afrika Mashariki Tanzania kupitia Chama Cha Wananchi CUF Mashaka Khalfani Ngole ameahidi kuzipatia ufumbuzi baadhi ya kero za skuli ya Msingi Makongeni Mtambwe kusini Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Ahadi hizo amezitoa wakati alipo guswa na kero za skuli hiyo zilizo wasilishwa kwa njia ya Risala iliyo somwa na mmoja ya walimu wa skuli ya Makongeni mbele ya mbunge huyo alipofika skulini hapo katika ziara yake ya Chama kisiwani Pemba.

Katika Risala hiyo imeelezwa kua skuli hiyo imepata mafanikio mengi na makubwa ikiwemo kufaulisha wanafunzi na kuongezeka kwa idadi ya walimu skulini hapo lakini bado inakabiliwa na changamoto kadhaa ambazo hazijapatiwa ufumbuzi  ikiwemo ukosefu wa umeme,uhaba wa madarasa, ukosefu wa huduma ya maji safi, uzio na vifaa vya kisasa kama vile kompyuta na uhaba wa vyoo skulini hapo.
Akihutubia baadhi ya wananchi na wanafunzi waliohudhuria mkutanoni hapo mbunge huyo pekee wa bunge la Afrika mashariki Tanzania kutoka vyama vya upinza kwa tiketi ya Chama Cha wananchi CUF ameahidi kuzipatia sulihisho baadhi ya kero zinazo ikabili skuli hiyo.

Amesema anaahidi kuwasaidia wanafunzi kumi wenye mahitaji Zaid ya sare za skuli kila mwaka kwa mgawanyo wa wanafunzi 5 wa msingi na 5 wa sekondari.
Mbali na sare za skuli pia ameahidi kuipatia umeme skuli hiyo ambapo katika kulikamilisha suala hilo amekabidhi waya wa fitingi hapo hapo kama mwanzo wa kuanza kulikamilisha suala hilo sambamba na kuahidi kuipatia kompyuta mbili 2 skuli hiyo.

"Haya yote niliyo yaahidi kwenu nitayatekeleza atakuja kiyakabidhi katibu wangu au ikiwezekana nitakuja Mimi mwenewe mbunge"alisema mbunge huyo.

Aidha mbunge huyo amewataka wanafunzi kuongeza juhudi za kusoma kwa bidii Ili waweze kuyafikia malengo ya kielimu ili ijekua msaada kwako na jamii wanazo toka.

"Wanafunzi nawataka msome sana na kwa juhudi kubwa Ili mujekua msaada kwa familia na jamii zenu"alieleza Ngole.
Katika ziara yake hiyo mbunge Ngole alikutana na makundi mbali mbali ya wanachama wa CUF ngazi ya matawi na wanamichezo wa Jimbo la Mtambwe akiambatana na katibu Wake Salama Masuud ambaye alikabidhi vifaa vya michezo aina ya jezi pea  8 kwa baadhi ya timu za Jimbo Hilo kwa lengo la kuahamasisha vijana kukiunga mkono Chama Cha wananchi CUF katika Jimbo Hilo.

Nao baadhi ya vijana waliozungumza na mwandishi wa habari hii wamesema wao wanamtazama na kumuunga mkono yule ambaye yupo karibu na wawo na kuajali kama alivo fanya Salama Masuud katibu wa mbunge huyo.

"Tutamuunga mkono anaetujali na sio lazima Chama Fulani kwani Mae deleo kwanza"walieleza vijana hao.

Ziara hiyo ilijumuisha kiongozi wa mipango na uchaguzi wa Chama hicho Jecha Abssi Jecha taifa na mshauri wa mbunge huyo katika mambo ya kisiasa Kapasha Haji Kapasha

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI