Skip to main content

BIASHARA YA KUKU WA KIENYEJI FURSA VIJANA WAASWA KUCHANGAMKIA

"Fursa yeyote hata ya mtaji wa shilingi 200 kiwa ni ya kutauta mwenyewe kijana au mwanamke au ya kupewa ambayo imedhamiria kumkomboa kiuchumi hiyo ni tunu ya kipekee tusiziache  ni Dhahabu. 

" Awali mimi niliona kama sitofanikiwa  kwa sababu nilikuwa na malengo bila uwezo, lakini nilikuwa na dhamira ya dhati juu ya hili suala  mara baada ya kusajiliwa katika  mpango huu  bhasi taratibu mtaji wangu ulianza kukua nilianza na kununua  kuku mmoja pekee  kutokana na uwezo mpka  wakafika 10 leo hii nimekuwa naendesha familia yangu yenye watoto    5 kwa hii shuguli nikiwa na Kuku 100. 

Aidha  Amina Aliwataka wajasiriamali wengine  kujiendeleza na shuguli nyengine za kilimo cha mboga  mboga ambacho kutasaidia kuendesha Shuguli zao za kila siku na kuongeza mapato madogo madogo yatakayosaidia  kuendesha harakati zao za kila siku. 

 Kwa upande wake Seif Salum Hamad ambae ni mume wa Mjasiriamali huyo  amesema kuwa Usimamizi mzuri katika shuguli hiyo unaotolewa na mke wake umepelekea kufungua akili yake, katika kupata Maendeleo ya kiuchumi. 

Sasa kupitia mke wangu nimeamini kuwa, wanawake wakiamua ni wachumi, watafutaji, wawekaji akiba na wanaojali familia,’’anasema kwa furaha.

Anasema " kwa sasa anajiamini kwa kuwa kila shilingi 100, inayotumika katika huduma za lazima pamoja na ada ya mtoto wao anayesoma skuli binafi, basi shilingi 70 ni za mke wake na nguo pia.

‘’Mimi sasa najiamini kama ntapata safari ya kikazi hadi mwezi mmoja, mke wangu anauwezo wa kuiendesha familia n ahata wageni wakitokezea,’’anasema.

Malengo yake ni kuwasomesha watoto wake hadi kufika vyuo vikuu na kuendesha maisha yao kwa shughuli nyengine kama vile kujenga nyumba kubwa ya kisasa.

Aidha Seifu amewashauri wanaume wenzake kushirikiana na wake zao katika kubuni miradi mbali mbali itakayowaondoshea umasikini na kuwaendeshea maisha yao ya kila siku.

Wakizunguzia harakati za mjasiriamli huyo baadhi ya majirani wa  Amina akiwemo Omar Haji Khamis na Fatma Hija Othman wanasema, familia hiyo imeibuka ghafla na leo kuwa mfano wa kuigwa kijijini kwao kimaendeleo.

‘’Kwa hakika jembo na ufugaji kama ukidhamiria haumtupi mtu, maana mfano wa hayo ni Amina na Mume wake, walianza kama utani kufuga kuku 10, leo wanahesabu 100,’’anasema Omar.

Kwa sasa inapofika kipindi cha sikukuu au mtu anapohitaji kuku, imekuwa rahisi wao kufika kwa Amina na kununua kwa ajili ya kukamilisha mahitaji. 

Kwa Upande wake Sheha wa shehia ya Mgogoni Said Hamad Khamis anasema, shehia hiyo ina wakaazi 4,326 ambao wanajishughulisha na shughuli mbali mbali za kijamii na kiuchumi Jambo ambalo anaendela  kujivunia ni kuona baadhi ya wananchi  akiwemo Amina Juma, wanafanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi ambazo zinawasaidia katika maisha yao ya kila siku.

‘’Kwa ninavyomfamu Amina Juma Salum na mume wake, leo nikisikia wanaishi kwenye maisha mazuri kwa sababu ya ufugaji na kilimo, hii ni furaha maana wameyatekeleza kwa vitendo maagizo ya serikali,’’anasema.

“Katika shehia yangu ni mwanamke ninae muamini kati ya wale ambao wanajishughulisha na harakati mbali mbali ili kuhakikisha wanapata maendeleo”, anasema.

Anaiomba serikali iendelee kuongeza nguvu kwa wanawake ambao wanajighulisha na kazi mbali mbali ikiwemo ujasiriamali, kilimo na ufugaji ili waweze kuondokana na utegemezi na hali ngumu za kimaisha.

Wakizungumzia suala hili baadhi ya Wanaharakati Wa kusaidia maendeleo ya Wanawake kiuchumi ikiwemo Fat-hiya Mussa Said TAMWA  Zanzibar wamesema Elimu kwa wanawake, iliyotolewa na inayoendelea kutolewa  inawasaidia  kubuni miradi ya kujiendesha kimaisha, badala ya kutegemea familia kwa kila kitu.

 Kwa Upande wake Mratibu wa TASAF Pemba Mussa Said, anasema wapo walengwa 14, 280 kwa Pemba ambao wanaendelea kupata fedha za kunusuriwa na umaskini 2022 2023.

Walengwa hao wapo kwenye shehia 78, ikiwemo ya Mgogoni, ambapo tayari shilingi bilioni 14. 4 zimeshwafikia.

‘’Mtu kama Amina Juma ndio hasa malengo ya TASAF ya kumtoa mwananchi katika unyonge, na kumleta kwenye taa, ili nae aishi maisha mazuri ambayo tunayahitaji na ndio malengo ya mradi huu  ni mfano wa kuigwa na sisi tunaendelea kujivunia yeye ,’’anasema Mratibu.

Aidha mratibu huyo alisema kuwa zaidi ya walengwa 50,000 kutoka wastani wa walengwa 15 kila shehia, kati ya shehia 78, ambao wamenzisha miradi ya kujikwamua wamefanikiwa katika shehia mbali mbali 

Mratibu Mussa alibainisha kuwa, kwa mwaka 2014/2015 ulipoanza mradi huo  walengwa hao  ambao ni wanwake na familia zenye hali ngumu ya kiuchumi wa kunusuru kaya maskini, waliibua miradi ya kijamii 41, idadi hiyo  iliongozeka mwaka uliofuata kwa kufikia miradi 84.

 Amina Salum Ni mjasiriamali ambae ameanza kwa mtaji wa Shilingi  10000  Fedha za mradi wa kunusuru kaya masikini kwa kuanzisha ufugaji wa kuku wa kienyeji ambapo kwa sasa amekuwa akiendesha  shuguli za familia kwa kuzalisha kuku hao, Mayai ya kienyeji na kuuza kwa watu mbali mbali na kujipatia Soko la uhakika katika biashara hiyo Huku Malengo yake ni kuendelea kuanzisha biashara nyengine Ya Usafiri wa voda boda ili kutoa fursa kwa vijana wengine. 

Mwisho. 


 

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

ZSTC YAWAONYA WAUZAJI NA WANUNUAJI KARAFUU KINYUME NA UTARATIBU ULIOWEKWA .

WIZARA YA AFYA YAWAPA UJUMBE HUU VIONGOZI WA DINI KUUFIKISHA KATIKA JAMII