Posts

Showing posts from October, 2023

UWT TAIFA WAIPONGEZA SERIKALI UTEKELEZAJI ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Image
NA AMINA AHMED MOH'D PEMBA.  MWENYEKITI wa umoja wa wanawake  UWT  Taifa   Mery Pius Chatanda amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Dr. Hussein Ali Mwinyi  ya kujenga miradi mikubwa ya Maendeleo  kwa wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba na kueleza Ilani ya CCM anaekeleza kwa kasi kubwa mno ambayo   haikuwahi kutokea.  Akizungumza kwa nyakati tofauti Mwenyekiti huyo wa UWT  amempongeza Rais  Dkt Mwinyi  pamoja na rais wa Tanzania kwa juhudi   za kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi  na kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo kwa wananchi ndani ya mkoa huo.  Amesema kasi ya  ujenzi wa maendeleo katika miradi  iliyomo ndani ya mkoa huo itasaidia kuongeza zaidi uhai wa chama na jumuia zake  sambamba na kuendelea kuwatumikia wananchi  kwa kuitekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi kwa Asilimia 100.  Kwa upande wake akiwa katika kukagua mradi wa uje...

CHATANDA KISINI PEMBA

Image
MWENYEKITI wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda na Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari pamoja na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji Taifa wawasili katika Mkoa wa Kusini Pemba kwa Lengo la Kuangalia Uhai wa Chama na Jumuhiya zake ,Utekelezaji wa CCM , Kuzungumza na wananchi kuhusu Mmongonyoko wa Maadili . Akizungumza jana katika Ukaguzi wa Mradi wa Uimarishaji wa Bandari  Ya Mkoani Kusini  Mwenyekiti Chatanda amefurahishwa na Utekelezaji wa Mradi huu ambao umegharimu zaidi ya Bilion 6 na kwasasa Utekelezaji umefanya kwa asilimia 100 . Mwenyekiti Chatanda amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  kupitia Shirika la  Bandari limeendelea na kuimarisha Miundombinu na kujenga Bandari za Kisasa zitakazotenganisha shughuli za Abiri ,mizigo ya makontena, Mafuta na gesi. " Utekelezaji wote ni Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi  mwaka 2020-2025 ibara ya ( 167a) ambayo inalengo kubwa la kuendeleeza Miundombinu nchini kwa kufanya Ujenzi ...

ZRA KUDHAMINI MGENI NDONDO CUP MSIMU UJAO WAASWA KUHAMISHA ULIPAJI KODI NA MATUMIZI YA RISITI ZA KIELECTRONIKI.

Image
NA, AMINA AHMED MOHD, PEMBA.  KATIKA kuhamasisha ulipaji wa kodi, kudai risiti za kielectroniki  wakati wa kununua bidhaa  katika maduka mbali mbali Kamishna wa mamlaka ya mapato Zanzibar ZRA  Yussuf Juma Mwenda  akiambatana na wasaidizi wa mamlaka hiyo wamefika katika uwanja wa shaame mata  Wilaya ya Micheweni  kuzungumza na wadau wa mpira wa miguu kutoa elimu juu ya suala hilo.  Kamishna mwenda amewataka  wanamichezo kuendelea kuisaidia serikali suala la risiti za kielectroniki pamoja na ulipaji kodi ili kuendeleza shughuli mbali mbali za maendeleo ikiwemo  uimarishaji wa viwanja vya michezo.  Sisi Peke yetu bila mashirikiano hatutweza kuishinda hii vita  kila mmoja wetu kwa nafasi yake akumbuke kuwa wajibu wake ni kusaodia serikali juu ya suala zima la kodi.  Aidha kamishna ameahidi udhamini  wa mashindano ya kombe la Mgeni ndondo cup linalowakutanisha vijana wa michezo katika wilaya ya mich...

ZRA KUDHAMINI MGENI NDONDO CUP MSIMU UJAO WAASWA KUHAMISHA ULIPAJI KODI NA MATUMIZI YA RISITI ZA KIELECTRONIKI.

Image
NA, AMINA AHMED MOHD, PEMBA.  KATIKA kuhamasisha ulipaji wa kodi, kudai risiti za kielectroniki  wakati wa kununua bidhaa  katika maduka mbali mbali Kamishna wa mamlaka ya mapato Zanzibar ZRA  Yussuf Juma Mwenda  akiambatana na wasaidizi wa mamlaka hiyo wamefika katika uwanja wa shaame mata  Wilaya ya Micheweni  kuzungumza na wadau wa mpira wa miguu kutoa elimu juu ya suala hilo.  Kamishna mwenda amewataka  wanamichezo kuendelea kuisaidia serikali suala la risiti za kielectroniki pamoja na ulipaji kodi ili kuendeleza shughuli mbali mbali za maendeleo ikiwemo  uimarishaji wa viwanja vya michezo.  Sisi Peke yetu bila mashirikiano hatutweza kuishinda hii vita  kila mmoja wetu kwa nafasi yake akumbuke kuwa wajibu wake ni kusaodia serikali juu ya suala zima la kodi.  Aidha kamishna ameahidi udhamini  wa mashindano ya kombe la Mgeni ndondo cup linalowakutanisha vijana wa michezo katika wilaya ya mich...

MAMLAKA YA MAPATO ZANZIBAR ( ZRA) YAWATOA HOFU WANANCHI JUU YA KODI YA MAJENGO ZANZIBAR.

Image
NA AMINA AHMED MOH’D PEMBA.  MAMLAKA  ya mapato Zanzibar ( ZRA ) Imewatoa hofu wananchi kuhusu maneno ya upotoshaji yanayoendelea kutolewa   na baadhi ya wananchi wasiopenda maendeleo  juu ya  ukusanayaji wa kodi ya majengo  ambapo imesema kodi hiyo haitowahusu  wamiliki wa nyumba za kawaida za makazi  kama inavyosambazwa na baadhi  ya watu wachache wasio na uelewa.   Akizungumza na viongozi wa mkoa kusini na kaskazini Pemba Kamshina mkuu wa mamlaka hiyo Zanzibar  Yussuf Juma Mwenda amesema kuwa  majengo ya ghorofa  yanayofanyiwa biashara  pekee ndio ambayo yatahusika na kodi hiyo  ambayo  pia haitowaumiza wamiliki wake  kutokana na unafuu uliowekwa.  "Mitaani kuna maneno uko lakini ukweli haupo ivyo unavyosemwa  mitaani, ukweli ni kuwa kodi hii sio ya wote bali ni ya watu wachache ambao wanamiliki majengo ya ghorofa".   Na wao pia haitowaumiza hiyo kodi kwa sab...

WANAFUNZI TOENI TAARIFA MKIONA VIASHIRIA VYA UDHALILISHAJI

Image
NA, IS-HAK MUHAMED, PEMBA.  WANAFUNZI wa Skuli za Mwambe za Dkt. Samia Suluhu Hassan Sec, Dkt. Hussein Mwinyi Msingi na Mwambe Msingi wamehimizwa juu ya muhimu ya kutoa taarifa pale wanapokubwa na changamoto mbali mbali zikiwemo za viashiria vya vitendo vya kufanyiwa uzalilishaji wa kijinsia. Wito huo umetolewa na Mratibu wa Chama cha Waandishi Wanawake Tanzania, Zanzibar Tamwa Fat-hiya Mussa Said wakati akiwasilisha mada juu ya Changamoto zinazowakabili watoto katika mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la Save the Children na kuwajumuisha wanafunzi wa Skuli hizo. Amesema zipo changamoto nyingi zinazowakumba watoto ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia, kimwili, kingono, kutekelezwa na nyengine nyingi lakini watoto hao wamekuwa wakishindwa kuziripoti jambo ambalo husababisha wafanyaji kuendelea na vitendo hivyo wakitambua kuwa hawaulizwi. Kwa upande wake Afisa Mradi Jumuishi katika Shirika la Msaada kwa watoto la Save the Children John Maftah amesema pamoja na jamii...

MWANAMKE ALIEIFUFUA JUMUYA ILIYOPOTEZA MUELEKEO MUDA MFUPI NA KUFIKIA NUSU YA MALENGO YAKE.

Image
  NA, AMINA AHMED MOH'D- PEMBA.                    SIFUNI ALI HAJI, KATIBU MKUU, PACSO.  KILA aneyepanda mbegu hutarajia mavuno mazuri na pale ambapo mti ukiwa haujashuhulikiwa vizuri basi mazao yake huwa madogo napengine yasiwe na ubora wa kuridhisha wala kuvutia.  Hivyo hivyo huwa kwa  kikundi cha watu kinapoamua kuunda jumuiya au taasisi kwa vile baada ya uzazi huitajika malezi na hio pia sio kazi rahisi. Kazi ya malezi imekuwa na changamoto zisizo hesabika kidoleni kwa taasisi na jumuiya nyingi Zanzibar na unaweza kusema nyengine zipo kwa jina tu.  Hali hii ndio inayopelekea baadhi ya wakati kusikika Msajili wa Asasi za kiraia akitaka kuzifuta  baadhi ya asasi kwa vile shughuli zake hazionekani. Moja ya taasisi ambayo kuwepo kwake kulitetereka na jamii ikawa haioni kwa vitendo shughuli ziliopelekea kuundwa kwake ni ya mwamvuli wa asasi za kiraia Pemba Association for civil  Society PACSO...

WANAFUNZI MWAMBE WATAKIWA KUTOA TAARIFA WANAPOVUNJIWA HAKI ZAO.

Image
NA Is-haka Rubea.                                                                                            WANAFUNZI wa Skuli za Mwambe za Dkt. Samia Suluhu Hassan Sec, Dkt. Hussein Mwinyi Msingi na Mwambe Msingi wamehimizwa juu ya muhimu ya kutoa taarifa pale wanapokubwa na changamoto mbali mbali zikiwemo za viashiria vya vitendo vya kufanyiwa uzalilishaji wa kijinsia. Wito huo umetolewa na Mratibu wa Chama cha Waandishi Wanawake Tanzania, Zanzibar Tamwa Fat-hiya Mussa Said wakati akiwasilisha mada juu ya Changamoto zinazowakabili watoto katika mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la Save the Children na kuwajumuisha wanafunzi wa Skuli hizo. Amesema zipo changamoto nyingi zinazowakumba watoto ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia, kimwili...

WAZAZI WAASWA MASHIRIKIANO KUMLINDA MTOTO.

NA,  IS- HAK  MOHAMED- PEMBA.  WAZAZI NA WALEZI katika Kijiji cha Mtangani, Shehia ya Mtangani Wilaya ya Mkoani Pemba wameelezwa kuwa jukumu la kumlinda mtoto na haki zake lipo ndani ya milki yao, hivyo ni vyema kuwa na mashirikianao mazuri kufanikisha suala hilo . Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mradi Jumuishi Save the Children Pemba Micheal Mwalupale wakati akizungumza katika kongamano la kijamii juu ya haki za mtoto huko Mtangani. Amesema kumlinda mtoto ni kuhakikisha anapata elimu, huduma za matibabu na haki zote za mtoto zinazingatiwa Nao baadhi ya watoa mada kwenye mdahalo huo wamesisitiza juu ya haja ya wazazi na jamii kwa ujumla kulipa kipaumbele suala la ulinzi na haki za watoto wao zinapatikana. Kwa upande wao baadhi ya wanajamii wa kijiji cha Mtangani wameeleza changamoto zilizokuwepo upatikanaji wa haki za mtoto kijiji hapo hata hivyo jamii imeonekana kupata mabadiliko kufuatia elimu wanayopatiwa mara kwa mara.

MAFUNZO YA SIKU NNE JUU YA UTETEZI WA HAKI ZA BINAADAMU KWA WADAU MBALI MBALI YATOLEWA

Image
Na AMINA AHMED MOH’D- PEMBA  WAANDISHI wa habari Kisiwani Pemba wameshauriwa kuendelea kutumia kalamu zao kutoa elimu kwa jamii kufahamu juu ya haki za binadamu. Ameyasema hayo Mratibu wa Mwevuli wa Asasi za Kiraia Pemba PACSO Mohd Najim kwenye mafunzo ya kubadilishana mawazo uliowashirikisha waandishi wa habari na wadau wa Haki zaBinaadamu Meneja wa mradi wa uwezeshwaji wa kisheria na upatikanaji wa haki (LEAP)ii Gmaliel Sunu amesema bado kuna uwelewa mdogo kwa jamii juu ya kudai haki zao za binaadamu kwenye vyombo husika. Akiwasilisha mada ya Haki za Binaadamu Mratibu kutoka Shirika la Msaada wa Kisheria na Haki za Binaadamu Siti Habib amesema miongoni mwa haki hizo binaadamu ni pamoja na haki ya kuishi, haki ya kupata elimu, haki ya kumiliki ardhi na haki ya kuabudu. Aidha amewataka waandishi wa habari kuendelea kutimiza wajibu wao wa kufanya utetezi kwa wananchi kwa kupaza sauti lengo kupatikana haki pale yanapotokezea matukio kwenye jamii. Mwache Juma A...

WATU WENYE ULEMAVU WALIA NA SERIKALI NA WADAU KUTOKUWASHIRIKISHA KATIKA MASUALA YA KUTOA MAAMUZI.

Image
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.  WATU wenye ulemavu wa akili kisiwani Pemba wameiomba Serikali pamoja na wadau kuwaunga mkono katika shughuli zao  wanazozifanya ili waweze kujipatia kipato na kujikomboa na umaskini.  Wakizungumza kwa  nyakati tofauti baadhi ya watu hao wamesema licha ya kujishughulisha na shughuli mbali mbali lakini bado serikali na wadau wamekuwa wakilisahau kundi hilo  katika kuwaendeleza  kiuchumi kama yalivyo makundi mengine ya watu wenye ulemavu.   "Najishughulisha na kilimo cha miche ya mivinje, miti ya kudumu na mboga mboga , Nishaepeleka barua wizara yakilimo juu ya kuja kunitembelea walau kuniongezea maarifa katika kilimo changu hicho lakini hakuna hata mmoja aiwahi kuja huku watu wakiiba miche na wengine wakitia ngo'mbe katika mashamba yangu ".  Fursa za mikopo hazitufikii kama walemavu wengine tumekuwa tukiachwa nyuma  na jamii lakini na hata serikali  katika mambo mengi, inatuona kama sisi  hatu...

Wanafunzi wafunzwa kutumia zoom, kuwasiliana na viongozi

Image
                                                                                              NA IS-HAKA RUBEA, PEMBA.  KUWEPO kwa jukwaa la kuwasiliana mtandaoni kumeelezwa kutawasaidia watoto katika kuwasilisha changamoto zao ili ziweze kuchukuliwa hatua kwa haraka na walengwa ikiwemo masuala yao ya kudai haki zao za kimsingi. Hayo wameyaeleza wanafunzi wa Skuli za Samia Suluhu Hassan na Mwambe Wilaya ya Mkoani Pemba, wakati wakizungumzia mafunzo ya kuwasiliana Mtandaoni(Zoom Meteeng) yaliyotolewa na Shirika la Save Tha Chidren Tanzania kwa wanafunzi hao ikiwa ni katika kujenga jukwaa la kuwasiliasha maoni ya watoto kupitia mikutano ya Mtandaoni. WaKizungumza baadhi ya wanafunzi hao wamesema kuwa kupitia kupitia njia hiyo ya matumizi ya...

KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR ATETA NA WANAFUNZI KOJANI.

Image
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.  WANAFUNZI  wa Skuli za Sekondari kisiwani Pemba  wametakiwa kuthamini juhudi zinazofanywa na serikali katika kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za elimu katika skuli mbali mbali  ikiwa ni pamoja na kutumia huduma za maktaba kujisomea vitabu mbali mbali vilivyotolewa .  Ametoa ushauri huo katibu mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya amali  Zanzibar Khamis Abdalla Said  Alipokuwa akizungumza  na wanafunzi wa madarasa ya Sekondari Kojani Mkoa wa Kaskazini Pemba  alipofika  kisiwani humo na kufanya ziara ya kustukiza kuangalia  maendeleo ya wanafunzi mapema leo asubuhi.  Amesema licha ya serikali kuendelea kuboresha na kuweka mazingira rafiki  kwa wanafunzi  lakini bado wanafunzi wamekuwa wakikosa kuzithamini juhudi hizo  na kupelekea kupatikana ufaulu usioridhisha kutokana na kushindwa kuzitumia fursa hizo za kujisomea vitabu  vya masomo mbali mbali.  "Serikali im...

SHEHA MADUNGU AIOMBA SERIKALI KULIPATIA UFUMBUZI SUALA HILI KUNUSURU WATOTO KUJIINGIZA TENA KATIKA TABIA HATARISHI

Image
            NA AMINA AHMED MOH’D - PEMBA.  SHEHA  wa Madungu, eneo liliopo katikati ya mji wa Chake Chake,Pemba,  ameitaka serikali  kuangalia  vyema utowaji  vibali  vya kuendesha   michezo  ya  video ili kudhibiti   kuporomoka kwa maadili  na tabia za watoto.            MAFUNDA HAMAD RUBEA - SHEHA MADUNGU     Aliishauri serikali kuweka masharti maalum  ya uendeshaji wa biashara hiyo na kufuatiliwa utekelezaji wake. Katika mahojiano maalum, Sheha wa Madungu,  Mafunda Hamad Rubea alisema juhudi za kuondoa athari za michezo hio kwa watoto zinazochukuliwa na uongozi kwa kushirikiana na wananchi  wa shehia hiyo bado hazipata ufanisi mkubwa. Alisema wamiliki bado hawajakubali kufunga biashara hiyo kwa madai wanatambulika kisheria kama walipa kodi, lakini ukweli ni kwamba biashara hii inachangia kuharib...

MAGANYA AWATAKA VIONGOZI WA CCM KUSINI KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WANANCHI NA KUZIPATIA UFUMBUZI

Image
NA AMINA AHMED MOH’D.  WANA chama wa chama  cha Mapinduzi mkoa wa  kusini Pemba   wamempokea kwa vifijo na nderemo  mlezi mpya wa  Chama hicho  mikoa miwili ya Pemba Fadhil Rajab Maganya  aliewasili kisiwani humo kwa ziara maalum ya kujitambulisha   ikiwa ni mara ya kwanza  tokea  kutangazwa kushika nafasi  hiyo.          FADHIL RAJAB MAGANYA - MLEZI CCM MIKOA MIWILI YA PEMBA.  Akiungumza kwa nyakati tofauti  na wanachama wa chama cha Mapinduzi  wilaya ya  Mkoani pamoja na  Chake chake  mlezi huyo amewataka  kuendeleza mashirikiano   katika kuimarisha chama na jumuia zake ikiwa ni pamoja na kubuni miradi mbali mbali ya maendeleo.  Amesema  mashirikiano kati ya wanachama na viongozi ikiwemo kutatua changamoto , kutekeleza ilani ya chama ndio nyenzo pekee itakayosaidia  kuleta maendeleo kwa wananchi.  ...

WAKULIMA WA KARAFUU WAIOMBA SERIKALI YA AWAMU YA NANE KUWAANGALIA ZAIDI

Image
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.  WAKULIMA  wa zao la karafuu kisiwani  Pemba wameiomba Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar Kuwasaidia kupata mikopo  itakayosaidia  kuAimarisha  kilimo cha zao hilo na kusimamia mashamba ya zao hilo  ha ili kuweza kupata mavuno mengi msimu unapowadia.  Wakizungumza na  habari hizi maalum baadhi ya wakulima   hao waliofika katika banda la kuuzia karafuu Madungu Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba   Akiwemo  Ayoub Muhamed pamoja na  Hamad Habibu Sultan Habibu   wamesema  kuwa licha ya Kujishughulisha na zao  hilo   bado manufaa kwa wakulima yamekuwa madogo kutokana na kuvuna  mazao kidogo  kutokana na ukosefu wa fedha za kusimamia  na kuendeshea shughuli za kilimo hicho.  Walisema kuwa   Licha ya zao hilo kuwa ni miongoni mwa mazao yenye tija kwa taifa lakini bado wakulima   wamekuwa wakikosa ...

MIAKA MIWILI YA KAZI: TAMWA YAWASILISHA RIPOTI

Image
NA MASSOUD JUMA.  WADAU wa kupinga vitendo vya udhalilishaji Zanzibar, wamekutana kwa pamoja katika ukumbi wa mikutano wa ZURA, kwa ajili ya kusikiliza ripoti iliyowasilishwa na TAMWA ZNZ juu ya utekelezaji wa mradi wa kutumia jukwaa la habari  kupinga vitendo vya udhalilishaji. Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa bodi ya TAMWA ZNZ Bi Asha Abdi, alisema kuwa mradi huo wa kutumia waandishi na vyombo vya habari kuzuia udhalilishaji ni mradi wa muda mrefu ambao TAMWA ZNZ wanatekeleza kwa mashirikiano makubwa na Shirika la Kitaifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA).  Bi Asha aliongeza kuwa lengo la mkutano huo ni kutathmini maendeleo ya mradi kwa muda wa miaka miwili kutoka ulipoanzia mpaka hii Septemba 2023, ambapo ndio mwisho wa utekelezaji wa mradi huo. “Kwa kweli tulipotoka sipo ambapo tupo hivi sasa, mambo yamebadilika kidogo kutokana na jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na serikali pamoja na wadau wengine, tunashukuru jitihada za serikali pia ka...