MAGANYA AWATAKA VIONGOZI WA CCM KUSINI KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WANANCHI NA KUZIPATIA UFUMBUZI
- Get link
- X
- Other Apps
NA AMINA AHMED MOH’D.
WANA chama wa chama cha Mapinduzi mkoa wa kusini Pemba wamempokea kwa vifijo na nderemo mlezi mpya wa Chama hicho mikoa miwili ya Pemba Fadhil Rajab Maganya aliewasili kisiwani humo kwa ziara maalum ya kujitambulisha ikiwa ni mara ya kwanza tokea kutangazwa kushika nafasi hiyo.
Akiungumza kwa nyakati tofauti na wanachama wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mkoani pamoja na Chake chake mlezi huyo amewataka kuendeleza mashirikiano katika kuimarisha chama na jumuia zake ikiwa ni pamoja na kubuni miradi mbali mbali ya maendeleo.
Amesema mashirikiano kati ya wanachama na viongozi ikiwemo kutatua changamoto , kutekeleza ilani ya chama ndio nyenzo pekee itakayosaidia kuleta maendeleo kwa wananchi.
" Kamati za siasa mkoa wa kusuni Pemba naomba mashirikiano ambayo kwa pamoja yatawaweka karibu na wanachama pamoja na wananchi kwa kusikilza changamoto na kuzipatia ufumbuzi kero na changamoto zao".
"Kukwepa kwepa kutokuwa na mashirikiano ni chanzo cha migogoro na mimi kitu ambacho sikihitaji ni kutatua mgogoro ninanchohitaji ni kuona mafanikio na maendeleo ya kukiimarisha chama ili kupata ushindi 2025".
Aidha mlezi huyo ameupongeza uongozi wa chama hicho Mkoa wa kusini Pemba kwa Mashirikiano mazuri aliyoyapata ambapo amesema kuwa hiyo ni ishara njema ya ya maendeleo kwa Serikali inayosimamiwa na chama cha Mapinduzi.
Aidha Maganya amesema kuwa ataendelea kuitumikia vyema nafasi hiyo ililengo lililokusudiwa la kuimaraisha na kuongeza nguvu katika chama hicho liweze kufikiwa.
Awali akitoa salam za chama mwenyekiti wa CCM mkoa huo Yussuf Ali Juma ameahidi mashirikiano kwa mlezi huyo ambapo amesema uongozi na wanachama utaendelea kusimamia na kutekeleza maagizo yote yaliotolewa yenye lengo ya kukisogeza mbele zaidi chama hicho
.
Nae kwa Upande wake Katibu wa chama hicho mkoa huo Ramadhan Hassan Rajab amemshukuru mlezi huyo kwa kufanya ziara hoyo maalum ndaninya mkoa huo ambapo wamesema chama na jumuia zake kitaendelea kumuunga mkono katika kusimamia majukumu aliyokabdihiwa.
Ziara hiyo licha ya kutembelea na kuzungumza wanachama wa wilaya mbili zilizomo ndani ya mkoa huo lakini pia mlezi huyo alitembelea na kukagua ujenzi wa milango ya maduka ya chama cha Mapinduzi iliyopo Chachani, Gombani pamoja na kutembelea kaburi la Aliekuwa Makamu wa rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Dk Omar Ali Juma Wawi pamoja na kumuombea dua ambapo ziara hiyo ya siku mbili kusini imefikia tamati na kuelekea Kaskazini pemba kwajili ya shughuli hiyo ya kujitambulisha.
Mwisho.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment