MAFUNZO YA SIKU NNE JUU YA UTETEZI WA HAKI ZA BINAADAMU KWA WADAU MBALI MBALI YATOLEWA

Na AMINA AHMED MOH’D- PEMBA 
WAANDISHI wa habari Kisiwani Pemba wameshauriwa kuendelea kutumia kalamu zao kutoa elimu kwa jamii kufahamu juu ya haki za binadamu.

Ameyasema hayo Mratibu wa Mwevuli wa Asasi za Kiraia Pemba PACSO Mohd Najim kwenye mafunzo ya kubadilishana mawazo uliowashirikisha waandishi wa habari na wadau wa Haki zaBinaadamu

Meneja wa mradi wa uwezeshwaji wa kisheria na upatikanaji wa haki (LEAP)ii Gmaliel Sunu amesema bado kuna uwelewa mdogo kwa jamii juu ya kudai haki zao za binaadamu kwenye vyombo husika.

Akiwasilisha mada ya Haki za Binaadamu Mratibu kutoka Shirika la Msaada wa Kisheria na Haki za Binaadamu Siti Habib amesema miongoni mwa haki hizo binaadamu ni pamoja na haki ya kuishi, haki ya kupata elimu, haki ya kumiliki ardhi na haki ya kuabudu.

Aidha amewataka waandishi wa habari kuendelea kutimiza wajibu wao wa kufanya utetezi kwa wananchi kwa kupaza sauti lengo kupatikana haki pale yanapotokezea matukio kwenye jamii.

Mwache Juma Abdalla miongoni mwa waliopewa mafunzo ameahidi kuyafanyia kazi kivitendo ili jamii kufahamu wajibu wao na sehemu husika za kudai na kupata haki zao.
Mafunzo hayo ya siku nne yameandaliwa na Mwevuli wa asasi wa kiraia Pemba PACSO yanafanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Amali Vitongoji Chakechake Pemba.

Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI