WAZAZI WAASWA MASHIRIKIANO KUMLINDA MTOTO.

NA,  IS- HAK  MOHAMED- PEMBA. 

WAZAZI NA WALEZI katika Kijiji cha Mtangani, Shehia ya Mtangani Wilaya ya Mkoani Pemba wameelezwa kuwa jukumu la kumlinda mtoto na haki zake lipo ndani ya milki yao, hivyo ni vyema kuwa na mashirikianao mazuri kufanikisha suala hilo.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mradi Jumuishi Save the Children Pemba Micheal Mwalupale wakati akizungumza katika kongamano la kijamii juu ya haki za mtoto huko Mtangani.

Amesema kumlinda mtoto ni kuhakikisha anapata elimu, huduma za matibabu na haki zote za mtoto zinazingatiwa

Nao baadhi ya watoa mada kwenye mdahalo huo wamesisitiza juu ya haja ya wazazi na jamii kwa ujumla kulipa kipaumbele suala la ulinzi na haki za watoto wao zinapatikana.

Kwa upande wao baadhi ya wanajamii wa kijiji cha Mtangani wameeleza changamoto zilizokuwepo upatikanaji wa haki za mtoto kijiji hapo hata hivyo jamii imeonekana kupata mabadiliko kufuatia elimu wanayopatiwa mara kwa mara.


Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI