KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR ATETA NA WANAFUNZI KOJANI.
- Get link
- X
- Other Apps
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.
WANAFUNZI wa Skuli za Sekondari kisiwani Pemba wametakiwa kuthamini juhudi zinazofanywa na serikali katika kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za elimu katika skuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutumia huduma za maktaba kujisomea vitabu mbali mbali vilivyotolewa .
Ametoa ushauri huo katibu mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Khamis Abdalla Said Alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa madarasa ya Sekondari Kojani Mkoa wa Kaskazini Pemba alipofika kisiwani humo na kufanya ziara ya kustukiza kuangalia maendeleo ya wanafunzi mapema leo asubuhi.
Amesema licha ya serikali kuendelea kuboresha na kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi lakini bado wanafunzi wamekuwa wakikosa kuzithamini juhudi hizo na kupelekea kupatikana ufaulu usioridhisha kutokana na kushindwa kuzitumia fursa hizo za kujisomea vitabu vya masomo mbali mbali.
"Serikali imekuwa ikijitahidi kuboresha mazingira ya elimu katika skuli zote, kuboresha majengo kuweka vifaa, vya kufundishia ambavyo ni vya kisasa vitabu waalimu lakini bado utumiaji wa maktaba (Library) umekuwa hauridhishi wanafunzi hawaoni iyo fursa . "
" Niwaase wanangu mthamini jitihada zinazofanywa na serikali kwajili ya kuwaandalia maisha bora baadae mzitumie maktaba hizi zilizopo skuli msome vitabu mpate kuongeza ufahamu msiziwache zikaingiwa na vumbi ".
Aidha katibu huyo amewataka wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya kidato cha nne kisiwani humo kuongeza bidii katika masomo ili waweze kupata matokeo mazuri yatakayobadilisha maisha yao na kuzifikia fursa mbali mbali.
Akizungumza Kwa upande wake mwalimu mkuu skuli ya Sekondari Kojani Khamis Amour Khamis ameushukuru uongozi huo uliofika katika skuli hiyo kwa nia ya kutaka kujionea maendeleo ambapo amesema itasaidia kuwa chachu ya mabadiliko kwa wanafunzi katika kuongeza kasi zaidi ya masomo yao.
"Yeye kafanya ziara kutushtukiza lakini hii kwetu sisi ni faraja kuona kuwa kiongozi anajali suala la elimu itasaodia kuongeza hamasa kwa vijana kusoma.
Nao baadhi ya Wanafunzi wamesema matarajio yao ni kupata ufaulu mzuri katika masomo ya sayansi ili kuweza kuwa wataalamu wazuri baadae.
Mwisho.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment