MWANAMKE ALIEIFUFUA JUMUYA ILIYOPOTEZA MUELEKEO MUDA MFUPI NA KUFIKIA NUSU YA MALENGO YAKE.


 

NA, AMINA AHMED MOH'D- PEMBA. 

 

 

              SIFUNI ALI HAJI, KATIBU MKUU, PACSO. 

KILA aneyepanda mbegu hutarajia mavuno mazuri na pale ambapo mti ukiwa haujashuhulikiwa vizuri basi mazao yake huwa madogo napengine yasiwe na ubora wa kuridhisha wala kuvutia. 

Hivyo hivyo huwa kwa  kikundi cha watu kinapoamua kuunda jumuiya au taasisi kwa vile baada ya uzazi huitajika malezi na hio pia sio kazi rahisi.

Kazi ya malezi imekuwa na changamoto zisizo hesabika kidoleni kwa taasisi na jumuiya nyingi Zanzibar na unaweza kusema nyengine zipo kwa jina tu. 

Hali hii ndio inayopelekea baadhi ya wakati kusikika Msajili wa Asasi za kiraia akitaka kuzifuta  baadhi ya asasi kwa vile shughuli zake hazionekani.

Moja ya taasisi ambayo kuwepo kwake kulitetereka na jamii ikawa haioni kwa vitendo shughuli ziliopelekea kuundwa kwake ni ya mwamvuli wa asasi za kiraia Pemba Association for civil  Society PACSO iliyoanzishwa mwaka 2005. 

Kwa zaidi ya miaka 10  PACSO ilikabiliwa na changamoto ya wanachama kwa vile shughuli zake zilitiliwa mashaka na kutoweza kufanya vizuri kuzileta pamoja  taasisi  zisizo za kiserikali  zilizopo Pemba ili kutimiza lengo la kuundwa kwake.

Tabaan, kuanzisha taasisi mpya sio kazi rahisi na hasa ikiwa inahusisha jamii pana na yenye watu wenye malengo na mitazamo tafauti ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Hata hivyo, PACSO ilihimili dhoruba kali lakini mwenendo wake ulikuwa wa kuchechemea na safari yake kuwa ngumu na malengo yake mengi kushindwa kuyafikia.

Lakini hatimaye akatokea mwana mama aliyeitafuta na kuipata njia ya kuifufua na kuiimarisha PACSO na sasa kuwa taasisi imara ambayo kazi zake zinafahamika na kutambulika kisiwani Pemba na nje.

Mwanamke huyu aliyeleta mageuzi katika PASCO na kuthibitisha uwezo wa mwanamke wa kuwajumuisha wana jamii na kuwaongoza kwenye safari ya maendeleo ni  Sifuni Ali Haji ambaye hivi sasa ni katibu mkuu wa huu mtandao wa asasi za kiraia Pemba.

Kutokana na juhudi zake mwamvuli huu uliweza kuvutia wananchama 20 tu kwa zaidi ya miaka 10  wakati lengo lilikuwa kuwaweka pamoja  wanachama  wasiopungua 100  kati ya 264 waliopo kisiwani Pemba.

Hawakukosea wale waliosema "Nyuma ya kila mafanikio yeyote  kuna juhudi za mwanamke ". 

 Miongoni mwa sababu zilizopelekea kutokuaminika ipasavyo kwa taasisi hiyo hapa kisiwani Pemba   ni pamoja na  usimamizi wa awali uliokuwa ukisua sua na kupelekea kupoteza  utendaji mzuri wa kuaminika.

 Kazi haikuwa rahisi  na iliendelea hivyo hivyo kuwa na wanachama wake  20  ambao ni taasisi za kiraia  bila mafanikio yeyote. 

Chini ya uongozi wake migogoro ya wenyewe kwa wenyewe iliyokuwepo kwa muda mrefu ndani ya  asasi ilipata ufumbuzi na kwa sasa unaweza kusema  mafanikio na malengo ya uanzishwaji wa taasisi hiyo yamefikiwa kwa asilimia 50.

Chini ya uongozi wake tasasi ilianzisha  miradi mbali mbali ambayo faida zake zinaonekana na hazihitaji kumurikwa tochi. 

" Kabla ya mimi kushika nafasi ya ukatibu kulikuwa na katibu  mwanamme  ambae aliiwacha nafasi hii mwaka 2015  baada ya kuona  malengo hayatimii mambo hayaendi sawa  mwaka 2015 na akaamua kuondoka ndani ya taasisi".  

 Alisema mara baada ya kushika nafasi ya katibu alifanya utafiti wa kuja mapungufu yako wapi ili asizidi kuikwamisha  taasisi na bada ya hapo ndio akipanga kazi za kufanya, hatua kwa hatua

"Taasisi hakuwa na miradi na tokea kuwa katibu tumefanikiwa kuwa na miradi mitatu ambayo  inasaidia  wananchama  wasio kuwa wanachama pamoja  na wana jamii, Ninafurahia mafanikio tulioyapata’, Bi Sifuni alisema. 

Alisema taasisi hiyo imeweza kusaidia na kuzijengea uwezo jumuiya wanachama kutokana na kuwapatia elimu nahii ndio ilioshajihisha kupata wanachama zaidi’’, aliongeza.

 ‘’Kitu muhimu katika uongozi ni wa taasisi  kuweka mbele maslahi na malengo  ya taasisi ", alieleza.

Alisema kati ya asasi 110 zilizojiunga na mwamvuli huo  30 zimefanikiwa kuandika miradi  ya maendeleo kutokana na kupata elimu ya uwandishi wa miradi. 

WITO WAKE KWA WANAWAKE 

Bi sifuni aliwataka wanawake waliopo Pemba kuzichangamkia fursa zinazotokana na asasi za kiraia katika kujikomboa na kuonesha uwezo wao wa kiutendaji kama yeye alivyothubutu kuleta mageuzi. 

Asasi za kiraia, zikiendeshwa vizuri na kwa uwazi, haziwekewi vizingiti na serikali. 

Lilio muhimu ni kufanya kazi kama ilivyobainishwa katika Sheria ya Jumuiya namba 6 ya 1995 ambayo inatumika kuzitambua, kuzisajili, kuongoza, kuweka masharti, utaratibu, muongozo wa uendeshaji na usimamizi. 

Kupitia sheria hii asasi za kiraia zimegawika  katika makundi ikiwemo ya asasi katika maeneo ya kazi maalumu, eneo maalumu, nchi maalumu, sambamba na mataifa maalum. 

Ashrak  Hamad Ali, ambaye ni Mratibu   Ofisi ya  Msajili wa Asasi za Kiraia upande wa Pemba alisema ofisi hiyo inatambua mchango mkubwa unaofanywa na  taasisi za kiraia Pemba, ikiwemo  PASCO.

"Hivi sasa taasisi nyingi za kiraia (NGO’s) kupitia Pacso zimekuwa na utayari waa kutoa mashirikiano kwa serikali kwa kutambua wao ni kama daraja la kazi za kuuitumikia jamii" .

Alisema baadhi ya taasisi Pemba zilikuwa katika hali ngumu, lakini hivi sasa kwa msaada mwamvuli wa PASCO zinaendeshwa kisheria kama taasisi nyengine. 

KAULI ZA WANACHAMA WA PACSO 

Tatu Abdalla Msellem wa jumuia ya Tumaini Jipya (TUJIPE) alisema mwamvuli umewasaidia  kutambulika uwepo wetu  kisheria na unaendelea kuwasaidia kupata misaada ya kuendeleza shughuli zetu.

Alisema anafurahia kuiona PASCO inaendesha shughuli zake kwa uweledi na ina inazisaidia asasi kupata misamaha katika kodi.

‘’ Tunashukuru, kwa kupitia PASCO, tumekuwa na uhusiano mzuri na serikali na taasisi nyengine katika kutekeleza shughuli mbali mbali", aliongeza Alisema Alawi  Bakar Hamad, Mkurugenzi  wa taasisi ya Popular Inspiring and Relief Organization ( PIRO ) Pemba  ambayo ni  miongoni mwa wanachama waliojiunga na mwamvuli  huo wa PACSO. 

Mwisho. 


Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI