WATU WENYE ULEMAVU WALIA NA SERIKALI NA WADAU KUTOKUWASHIRIKISHA KATIKA MASUALA YA KUTOA MAAMUZI.
- Get link
- X
- Other Apps
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.
WATU wenye ulemavu wa akili kisiwani Pemba wameiomba Serikali pamoja na wadau kuwaunga mkono katika shughuli zao wanazozifanya ili waweze kujipatia kipato na kujikomboa na umaskini.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya watu hao wamesema licha ya kujishughulisha na shughuli mbali mbali lakini bado serikali na wadau wamekuwa wakilisahau kundi hilo katika kuwaendeleza kiuchumi kama yalivyo makundi mengine ya watu wenye ulemavu.
"Najishughulisha na kilimo cha miche ya mivinje, miti ya kudumu na mboga mboga , Nishaepeleka barua wizara yakilimo juu ya kuja kunitembelea walau kuniongezea maarifa katika kilimo changu hicho lakini hakuna hata mmoja aiwahi kuja huku watu wakiiba miche na wengine wakitia ngo'mbe katika mashamba yangu ".
Fursa za mikopo hazitufikii kama walemavu wengine tumekuwa tukiachwa nyuma na jamii lakini na hata serikali katika mambo mengi, inatuona kama sisi hatustahiki kuthaminiwa, hatushirikishwi kutoa maoni, hatushirikishwi tunaoneka hatuna uwezo wa kufikiria tunazidi kurudi nyuma". Omar Said Ali mweneye ulemavu wa akili Vikunguni Chake Chake.
Aidha Omar ameiomba jamii kuepuka kuwaita majina yasiostahiki yenye kuleta mawazo pamoja na kuwabambikizia makosa ambayo hayawahusu, kwa malengo ya kuwasababishia matatizo zaidi.
"Mtu anakuita zezeta, mara anakuita kiguu chechegu, mara kikono upande, mara faza inafika hadi unasingiziwa makosa makubwa ya ubakaji sababu tu unaonekana utakosa mtetezi wa kukutetea tunaumia na tunachukizwa sana serikali itusaidie kupiga marufuku.".
Nae kwa upande wake Salma Ali Haji Kutoka Msuka wilaya ya Micheweni pamoja ma Saumi Khamis Hamad kutoka Konde wamewaomba wadau pamoja na serikali kuwasaidia watu wenye ulemavu wa akili kuepukana na udhalilishaji wanaoendelea kufanyiwa katika jamii ikiwa ni pamoja na kushambuliwa na kupuuzwa wanapofanya shughuli zao .
" Bado jamii haituoni kama ni watu wenye ulemavu wanatulinganisha na watu wenye akili pindi tunapokosea, tukiwa katika harakati zetu za kufanya biashara tunaonekana kama vichekesho ukiwa katika harakati njiani mara tunalengwa mawe bila sababu " Alisema Saum.
" Niliacha skuli baada ya kuona napumbwaza mara hujaolewa , watu wanatuona kama sisi wanawake wenye ulemavu wa akili ni watu wakuolewa, wapo wanatukopa biashara zetu hawatulipi pia serikali itusaide kutuwekea usawa ili na sisi tuepukane na madhila hayo".
Aidha Rashid Habib Salum Kutoka Kengeja ameiomba serikali kuweka masharti maalum kwa watu wenye ulemavu wa akili wanaposhirikishwa kufanya kazi za kijamii ili kuweza kupata haki zao wanaposhiriki katika kazi hizo.
"Tunakuwa tunafanya kazi bila kuchoka wala kuhurumiwa na malipo yetu tunayakosa binafsi nililetwa chake chake kufanya kazi ya ujenzi lakini sijalipwa hata senti wenzangu wamelipwa wanajua sina uwezo wa kusema popote nikaaminika kwa sababu ya uleavu wangu".
"Sisi pia tuna haki ya kuwa na familia lakini jamii hailiangalii ilo unaweza ukawa na familia lakini ukapokonywa kutokana na kukosa kuhudumia. "
Akizungumza juu ya Changamoto hizo zinazowakumba watu hao Halfan Amour Muhammed ambae ni Katibu Jumuia ya watu wenye ulemavu wa akili Pemba amesema taasisi imekuwa ikizipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu kwa kuwapa elimu ya kujitambua na kuweza kuzisemea.
"Changamoto ni nyingi ambazo zinawakabili kama ambazo wamezitaja kudhalilishwa, kuitwa majina mabaya, kukosa fursa za kushiriki na kushirikishwa katika kutoa maamuzi, kuonekana sio watu wa maana katika jamii kutengwa na mengineyo sisi kama Jumuia jambo la kwanza tumekuwa tukiwapa elimu ya kujitambua".
" Tunawajenga waweze kuzisemea wenyewe na kwa sasa ndani ya jumuia tumeanzisha vikundi kwa wanachama vikundi ambavyo ni vya utetezi binafsi hivi kazi yake kubwa ni kuwasaidia wao wenyewe wanachama wetu kuweza kuzisemea changamoto zao zinapowatokea".
" Na jambo hili limefanikiwa kwa kiasi kikubwa wapo ambao wameshapata changamoto na wakaweza kusimama wenyewe kujitetea katika vyombo vya maamuzi mahakamani na wakafanikiwa".
"Aidha amesema jumuia hiyo imekuwa ikifanya mikutano na wanajamii, kutoa mafunzo namna ya kuishi na kuwashirikisha watu wenye ulemavu wa akili kufuatilia wanapopata changamoto ili kuizipatia ufumbuzi".
Hata hivyo Katibu huyo ameiomba serikali pamoja na wadau kuwaangalia vyema watu wenye ulemavu wa akili kwa kutambua haki zao .
"Wadau na Serikali iwaangalie watu wenye ulemavu wa akili kwa jicho la pili, kuwapa mashirikiano, wao ni watu wenye mawazo mazuri pia wanapopewa fursa, haki ya kuwalinda na udhalilishaji kuwapa mashirikiano kutambua haki zao kama watu wengine wenye ulemavu .
Mazungumzo haya maalumu kati ya watu wenye ulemavu wa akili pamoja na mwandishi wa habari hizi ni katika kuelekea siku ya afya ya akili duniani ambayo kikele chake ni oktoba 10 ya kila mwaka lengo ni kusaidia kupaza sauti zao kuona changamoto zinazowakabili zinapatiwa ufumbuzi.
Mwisho
- Get link
- X
- Other Apps
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete