WAKULIMA WA KARAFUU WAIOMBA SERIKALI YA AWAMU YA NANE KUWAANGALIA ZAIDI
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.
WAKULIMA wa zao la karafuu kisiwani Pemba wameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Kuwasaidia kupata mikopo itakayosaidia kuAimarisha kilimo cha zao hilo na kusimamia mashamba ya zao hilo ha ili kuweza kupata mavuno mengi msimu unapowadia.
Wakizungumza na habari hizi maalum baadhi ya wakulima hao waliofika katika banda la kuuzia karafuu Madungu Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba Akiwemo Ayoub Muhamed pamoja na Hamad Habibu Sultan Habibu wamesema kuwa licha ya Kujishughulisha na zao hilo bado manufaa kwa wakulima yamekuwa madogo kutokana na kuvuna mazao kidogo kutokana na ukosefu wa fedha za kusimamia na kuendeshea shughuli za kilimo hicho.
Walisema kuwa Licha ya zao hilo kuwa ni miongoni mwa mazao yenye tija kwa taifa lakini bado wakulima wamekuwa wakikosa msaada katika kuendesha harakati hizo kwa kukosa mkopo kama ilivyokuwa awali jambo ambalo kwa upande wao limekuwa changamoto .
Aidha wakulima hao wameiomba Serikali kuiangalia tena bei ya zao hilo na kuongeza ili kuendana na gharama za ushughulikiaji wa mikarafuu wanaofanya .
wamesema bei wanayoendelea kuuza karafuu kwa sasa haikidhi haja zao kutokana na kutumia gharama kubwa katika kulima zao hilo.
Katika hatua nyengine wakulima hao wameliomba shirika la biashara ZSTC kutowacheleweshea malipo yao wanapofanya mauzo ya karafuu sambamba na kupunguza makato ya tozo .
Akizungumza juu ya maoni hayo yaliotolewa na baadhi ya wakulima hao Afisa dhamana wa shirika la biashara la taifa ZSTC Pemba Abdalla Ali Ussi amesema ugawaji wa miche ya mikarafuu kwa wakulima wote bado haukidhi haja kwa wakulima wote hivyo ni vyema wakulima kuendelea kupanda miche kwajili ya kukuza zao hilo.
Aidha kuhusu suala la fedha kutolewa Kwa wakulima Kwa njia ya benki mdhamini huyo amesema shirika linafanya hivyo kwajili ya usalama wa fedha za wakulima .
Comments
Post a Comment