CHATANDA KISINI PEMBA
MWENYEKITI wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda na Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari pamoja na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji Taifa wawasili katika Mkoa wa Kusini Pemba kwa Lengo la Kuangalia Uhai wa Chama na Jumuhiya zake ,Utekelezaji wa CCM , Kuzungumza na wananchi kuhusu Mmongonyoko wa Maadili .
Akizungumza jana katika Ukaguzi wa Mradi wa Uimarishaji wa Bandari Ya Mkoani Kusini Mwenyekiti Chatanda amefurahishwa na Utekelezaji wa Mradi huu ambao umegharimu zaidi ya Bilion 6 na kwasasa Utekelezaji umefanya kwa asilimia 100 .
Mwenyekiti Chatanda amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Shirika la Bandari limeendelea na kuimarisha Miundombinu na kujenga Bandari za Kisasa zitakazotenganisha shughuli za Abiri ,mizigo ya makontena, Mafuta na gesi.
" Utekelezaji wote ni Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi mwaka 2020-2025 ibara ya ( 167a) ambayo inalengo kubwa la kuendeleeza Miundombinu nchini kwa kufanya Ujenzi mbalimbali wa Miundombinu ya Bandari. "
Hata hivyo Mwenyekiti Chatanda amesema lengo la Uimarishaji wa Bandari ni kuifanya iweze kutoa huduma za Kitaifa na Kimataifa katika kuhakikisha huduma ya Bandari inawanufaisha wananchi kwa ujumla na mimi kama Mwenyekiti nimefurahishwa na Utekelezaji Mkubwa wa Mradi huu.
Mwenyekiti Chatanda amesema nimetembelea Miradi sita katika Mkoa wa Kusini Pemba ambayo yote imekuwa ya kiwango cha juu na Utekelezaji umefanyika kwa ufanisi wa hali ya juu na fedha za Miradi sita zaidi ya Bilion 31 .
"Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefanya kazi kubwa hivyo niwaombe viongozi wa Chama na Serikali kuhakikisha mnafanya Mikutano ya Hadhara na kusemea miradi iliyotekelezwa katika maeneo yenu ili wananchi wajue nini kimefanyika katika Serikali yao."
Aidha nae Makamu Mwenyekiti Mnec Zainab Shomari amesema Ujenzi wa barabara ya wete-chake Unatarajiwa kutumia jumla ya Sh Bilioni 23.6 na Ujenzi kwasasa unaendelea kwa kasi na wananchi wanafurahia Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi .
" Niwaombe wananchi wangu wa Kusini Pemba Mh Rais Dkt Hussein Mwinyi amefanya kazi kubwa ya kuleta Maendeleo katika Taifa letu hivyo Niwoambe kuendelea kusemea kazi na miradi iliyotekelezwa katika maeneo yenu. "
MWISHO
Comments
Post a Comment